SAKATA
la Mkurugenzi wa Kampuni ya Kitalii ya DAGT, Timoth Mroki, kujiua kwa
kujilipua kwa risasi, limeibua mambo mapya kutokana na kuelezwa kuwa
wivu wa kimapenzi.
Habari
zilizopatikana jijini Arusha, zinasema kuwa Mroki (36), alikuwa na
vimada wawili ambao ni wake za watu na kuwa kabla ya kujilipua kwa
risasi na kupoteza maisha, alitoa taarifa kwa wanawake hao (majina
yanahifadhiwa).
Imeelezwa
kuwa Mroki alikuwa akitoka na wanawake hao kila mmoja kwa muda wake,
lakini baadaye siri hiyo ilianza kuvuja na hatimaye vimada kufahamiana,
ikiwa ni pamoja na mkewe kuanza kupenyezewa taarifa hizo.
Mroki,
ambaye pia ni Meneja wa Operesheni na Masoko wa Kampuni ya Tanzania
Bush Camp, alijiua kwa kujipiga risasi Oktoba 25, mwaka huu, saa 1:00,
baada ya kubaini kuwa vimada wake hao wamefahamiana.
Habari
kutoka kwa mtu wa karibu zimesema kuwa, vimada hao baada ya
kufahamiana, walikutana na kufanya mazungumzo kisha kupiga picha pamoja
na kumrushia kupitia simu ya mkononi.
Kugundulika
kwa siri hiyo, kulizusha taharuki kwa Mroki, hivyo kusababisha kuyumba
kwa uhusiano baina yake na vimada hao, akiwemo mmoja ambaye pia ni
mshirika wake kibiashara.
“Hawa
wanawake wana siri nzito kuhusiana na kifo hiki kwa sababu kabla ya
kufanya uamuzi, aliwasiliana nao…kikubwa awali walikuwa hawafahamiani
ila baadaye walikutana na kuungana kuwa kitu kimoja.
“Haifahamiki
ni kwa vipi walijenga urafiki, ila watu wa karibu wanasema walijipanga
kumkomoa ili afilisike kwa kuwa kila mmoja alikuwa na malengo yake,”
alisema mtoa habari wetu.
Kuungana
kwa wanawake hao kumlichanganya Mroki, ambaye tayari uhusiano wake
nyumbani pia ulianza kuwa tete baada ya mkewe kuhisi kuna mambo
yanafanyika kinyume cha utaratibu.
Hata
hivyo, habari zaidi zinasema kuwa miongoni mwa wanawake hao, yupo
aliyejenga uswahiba na mke wa marehemu huku uhusiano wa kimapenzi
ukifichwa chini ya mwamvuli wa biashara.
Chanzo
chetu kimesema kuwa, kutokana na ukaribu huo, familia hizo zimekuwa na
kawaida ya kutembeleana, ikiwa ni pamoja na watoto kukaa kwa siku kadhaa
nyumbani kwa kimada mmoja.
Imeelezwa kuwa kutokana na kugundulika kwa siri hiyo, Mroki alichukua uamuzi wa kujimaliza ili kukwepa aibu mbele ya familia.
“Kugonga
gari si sababu ya Mroki kujiua, ni kutokana na kutingwa na mambo mengi
kichwani, hasa baada ya siri ya kimapenzi kuanza kubainika,” aliongeza
mmoja wa rafiki wa marehemu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema Mroki alijiua kwa
kujipiga risasi kifuani kwa kutumia bastola aina ya KEL –TEC yenye namba HCB21.
Katika taarifa yake, Kamanda Sabas alisema kabla ya tukio hilo, Mroki alikuwa na gari namba T222CMX, aina ya Isuzu Double Cabin, iliyokuwa ikitokea Mbauda kwenda katikati ya jiji.
Hata
hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa kutokana na msongamano wa magari,
Mroki alitanua barabara kukwepa foleni huku akiwa katika mwendo kasi.
Alipofika maeneo ya Shams, aligongana na gari la mizigo, mali ya Kampuni ya Gupta, lenye namba T548 BRL.
Taarifa
ilisema pamoja na kusababisha ajali hiyo, Mroki aliendelea na safari
yake ndipo madereva wa bodaboda walipoamua kumfukuza na kumkamata eneo
la kona ya Nairobi Ngarenaro.
Mroki
aliporejea eneo la tukio na kuulizwa sababu za kusababisha ajali na
kuendelea na safari, alitoa bastola na kufyatua risasi mbili hewani na
ya tatu kumpiga kifuani.
No comments:
Post a Comment