JESHI
la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu
(Michael dada), mkazi wa Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa
kuhusika na matukio ya ubakaji wa vikongwe mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei
alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo kwa kipindi kirefu
kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya ubakaji wa vikongwe na
wanawake na kutokomea kusikojulikana.
Alisema,
William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la
wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko Kiluvya.
Pia kamanda Matei alisema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika katika
matukio ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo hivyo
alikuwa akiwatishia wahusika kwa mapanga.
“Huyu kijana anayejiita Michael dada ni maarufu kwa matukio ya
ubakaji na alilisumbua jeshi letu mara kadhaa kwa kunasua mitego
aliyowekewa leo tumelazimika kumleta mbele yenu waandishi ili mumuone ni
mdogo lakini ametusumbua sana,” alisema.SOMA ZAIDI>>
William alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwa miaka ya hivi
karibuni aliwahi kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha kosa ambalo
lilimsababishia kuhukumiwa miaka 30 jela
Matei alisema kabla kifungo hicho hakijamalizika mwaka 2011 na 2012,
William alikata rufaa na kutolewa ili kuendelea na taratibu nyingine na
tangu hapo hakuonekana hadi polisi walipofanikiwa kumkamata kwa kosa la
wizi wa mifugo.
Hata hivyo William alikana kuhusika na tuhuma zinazomkabili na kudai
yeye sio Michael dada kama anavyoitwa bali ni Michael William na tuhuma
za ubakaji ni za kusingiziwa.
No comments:
Post a Comment