Wednesday, October 29, 2014

TANZANIA YAKATAA RASMI NDOA ZA JINSIA MOJA KWENYE AGENDA ZA MAENDELEO YA MILENIA


001
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.

“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.

Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.

002
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.

Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo. Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.

Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga. Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
003
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.

“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
004
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
005
Mdau akichangia mada yake.
006
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.

008
009

No comments:

Post a Comment