
Mbunge wa
CCM kupitia kadi ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Arusha, Catherine
Valentine Magige . IMEFICHUKA! Madai ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa
wa Geita, Vicky Paschal Kamata kuwatumia meseji za kashfa wabunge
wenzake, Lucy Thomas Mayenga (CCM) na Catherine Valentine Magige
(UVCCM)Mkoa wa Arusha sasa mambo hadharani.Kwa mujibu wa chanzo chetu,
wabunge hao warembo wako katika vita baridi ikiendeshwa chini kwa chini
kwa Cathy (pichani) na Lucy kudai kwamba wamekuwa wakitumiwa meseji
zenye kejeli na kashfa nzito kutoka kwa mheshimiwa Vicky.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, licha ya sababu kutokuwa wazi sana,
lakini madai ni kwamba wana bifu linalokimbilia mwezi wa nne sasa.
“Unajua si rahisi wao kuweka wazi bifu lao, lakini wenyewe watakuwa
wanajua nini kiini, ukifuatilia utagundua kuwa maisha yao yamekuwa ni ya
vikundivikundi, akina Lucy wana kundi lao na Vicky ana la kwake,”
kilisema chanzo hicho.

Mbunge wa CCM kupitia tiketi ya Umoja wa Vijana, Lucy Thomas MayengaKWA NINI VICKY?
Chanzo kiliendelea kuanika kwamba, baada ya meseji zinazodaiwa kukosa
staha kutumwa na asiyejulikana kwenda kwenye simu za mkononi za Cathy
na Lucy, waheshimiwa hao hawakupembua sana mchele, moja kwa moja
wanadaiwa kumtaja hasimu wao kwenye vyombo vya dola kuwa huenda
anahusika na ‘utundu’ huo.
POLISI WAFUATILIA MINARA YA SIMU
Duru za kipolisi zinadai kuwa kufuatia waheshimiwa hao kumlalamikia
Vicky, wana usalama hao walianza kuchunguza mawasiliano yake ambapo
walibaini mambo makuu mawili.
KWANZA, baadhi ya meseji hizo zilionesha kutumwa kwa kupitia mnara wa
simu uliopo maeneo ya bunge. PILI, kuna meseji iliwezeshwa kusafiri kwa
nguvu ya mnara uliopo eneo linaloitwa Uwanja wa Ndege ambapo inadaiwa
Mheshimiwa Vicky ndiko anakoishi.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Geita, Vicky Paschal Kamata SERIAL NUMBER
Pia yapo madai kwamba, polisi hao walikwenda kitaalam zaidi na
kubaini kwa kutumika namba zilizomo ndani ya simu eneo la kuwekea betri
(serial number) ambazo zilionesha kuwa, laini iliyokuwa ikituma meseji
za kuudhi kwa waheshimiwa hao pia imekuwa ikutumia na laini ambayo
polisi walimjua mhusika, ingawa wasemaji wake wamesita kuthibitisha.
POLISI NYUMBANI KWA VICKY
Habari zaidi zinadai kuwa, Jumanne iliyopita, polisi mkoani Dodoma
walifika nyumbani kwa mheshimiwa Vicky na kufanya uchunguzi kama
wanaweza kupata simu yenye laini iliyoripotiwa na akina Mayenga
(pichani) kwamba imekuwa ikiwakashifu kwa meseji lakini hawakufanikiwa
kukuta chochote.
Alipotafutwa Vicky ili kujua undani wa meseji hiyo juzi, simu yake
haikuwa hewani. Kwa upande wake Lucy ambaye alidai kutumiwa meseji za
matusi katika gazeti moja (siyo la Global), naye simu yake iliita bila
majibu, huku Cathy akishindwa kupatikana na kulifanya gazeti hili kuzidi
kuchimba kwa kina sakata hili ili kupata mbivu na mbichi na kuzianika
bila kusitasita.
No comments:
Post a Comment