Hii ni
aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma
Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu, Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa
wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu
kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.Timbwili zito likianza
kati ya njemba mmoja anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma
Mtata. Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa
Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo
kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata
kilaji.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani
mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na
mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na
vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.
MUME ATOKA KIDOGO
Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa
usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi
uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua na
kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka mkewe,”
kilidai chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, Zeno akiwa katika
sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia
‘kunyonya’ kilevi kikali. ZACHAPWA
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa makofi
ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe na kumchota
mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa katika hali ya
kuzidiwa na kilaji.
Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili wa
mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa walihofia
yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa mjumbe wa eneo hilo
aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini walimkuta mke wa mjumbe ambaye
aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na
kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi nyumbani kwao
ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza kutifuana tena kabla ya
kuamuliwa na wasamaria wema.
Taarifa tulizozipata wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda
mitamboni juzi, Jumatano, wawili hao walikuwa tayari wameshayamaliza na
wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana msamaha.
No comments:
Post a Comment