Mwanamke mmoja katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amemfanyia ukatili mume wake kwa kumwagia maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi wilayani hapa, tukio hilo lilitokea juzi,
saa 4:30 usiku, katika mtaa wa Nyamakokoto, mjini Bunda, baada ya
kuzuka ugomvi ulitokana na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) kuchelewa
kurudi nyumbani.
Mwanaume huyo amejeruhiwa vibaya mume wake sehemu mbalimbali za mwili
wake, hali iliyopelekea kulazwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya
Bunda.
Akizungumza na NIPASHE juzi, mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.
Akizungumza na NIPASHE juzi, mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.
Alisema siku hiyo alitoka kazini kwake saa 1:00 usiku na kukuta mke wake
ambaye amezaa naye watoto wanne akiwa hajarejea nyumbani huku watoto
hawajetengewa chakula.
Alisema baada ya kukuta hali hiyo aliamua kuchukuwa fedha na kwenda kununua mboga ili aweze kuandaa chakula cha usiku akijua hawezi kurudi muda huo.
Alisema baada ya kukuta hali hiyo aliamua kuchukuwa fedha na kwenda kununua mboga ili aweze kuandaa chakula cha usiku akijua hawezi kurudi muda huo.
Alisema baada ya kufika saa 4:00 usiku wakati watoto wake wameshabandika
maji ya kupikia ugali, aliamua kwenda kwa rafiki wa mke wake ili
kuuliza alipo mkewe, lakini walisema hawajamuona.
Alisema aliamua kurejea nyumbani na ilipofika saa 4:30 usiku mwanamke
huyo alirejea na baada ya kumuuliza kwanini amechelewa kiasi hicho,
alichukuwa sufuria la maji ya moto na kumwagia.
“Tangu nimuowe na kufanikiwa kuzaa naye watoto wanne sijawahi kumpiga
licha ya kufanya vituko vya mara kwa mara….sasa aliporejea muda wa saa
4:30 na mimi kumuuliza ni kwani amechelewa kiasi hicho na akijua ni mke
wa mtu, hapo ndipo alipochukuwa maji ya moto yaliyokuwa yametengwa kwa
ajili ya kupikia ugali na kunimwagia” alisema.
Mganga wa zamu katika hospitali ya Bunda, Dk. Bakari Ibrahimu, alisema
majeruhi huyo amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa
kifuani na mikononi na kwamba anaendelea na matibabu na hali yake
inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment