Na Mwajabu Hoza Kigoma.
WATU sita wamekufa 27 wameokolewa na wengine 11 kulazwa katika
hospitali ya rufaa maweni iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma
baada ya boti walilokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa Tanganyika
mkoani humo.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamishina msaidizi wa
polisi mkoa kamanda Jafar Mohamed alisema tukio hilo limetokea majira ya
saa nne asubuhi katika kijiji cha Kalalangabo kilichopo mwambao wa ziwa
Tanganyika kwenye halmashauri ya wilaya Kigoma.
Kamanda Mohamed alisema chanzo cha tukio hilo ni idadi kubwa ya watu
waliokuwa katika boti hilo na kusababisha kuzama majini mita 200 kutoka
nchi kavu na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye sherehe ya
harusi katika kijiji cha Kigalye kilichopo jimbo la Kigoma Kaskazini
mkoani humo.
Alisema watu waliopatikana ambao ni marehemu ni watu sita wakiwemo
watoto wawili kati ya hao mmoja ametambuliwa kwa jina la Salama Juakali
(37) huku wengine majina yao yakiwa hayaja tambuliwa hadi sasa.
Kamanda amesema hatua za uokoaji zinaendelea sanjari na taratibu za
kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanafikishwa katika vyombo vya
sheria kujibu tuhuma inayowakabili.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa wavuvi katika mwalo wa
Kibirizi uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Sedwe Ibrahimu alieleza idadi
ya watu waliozama majini inasadikiwa kuwa zaidi ya watu 64 ambao
walikuwa wakielekea harusini.
Alisema mitumbwi iliyosababisha ajali ilikuwa miwili ambayo ni maalum
kwa kuvulia samaki na dagaa hivyo ilitumika kusafirishia abiria baada
ya kukodiwa kwa lengo la kuwfikisha maharusi katika kijiji cha Kigalye
wakitokea katika kijiji cha Mwandiga jimbo la Kigoma Kaskazini ndipo
walipokutwa na janga hilo.
Akifafanua kuhusu tukio hilo baada ya kupatiwa tarifa ya kuzama kwa
mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba watu waliokuwa katika magari matatu
aina ya Hiace pamoja bodaboda tatu kiasi ambacho kinaashiria watu hao
walikuwa wengi ukilinganisha na uwezo wa mitumbwi hiyo ambayo hubeba
watu 20 tu wakati wa shughuli za uvuvi.
v
viongozi wa mkoa wa Kigoma wakiangalia kwa makini zoezi la uopoaji wa miili ya watu
Alieleza eneo ambalo walitumia kupakia abiria hao ilikuwa katika
kijiji cha Kalalangabo ambapo si rasmi kwa kupakia abiria kisheria na
hivyo kutakiwa kutumia eneo la kibirizi ambalo limetengwa kisheria.
Baaadhi ya wahanga wa tukio hilo akiwemo Zainabu Issa na Mariamu Juma
(18) ambaye ni bibi harusi alisema chanzo ni baada ya mitubwi hiyo
kukumbwa na wimbi la maji sambamba na idadi kubwa ya watu takribani 80
ambao walikuwa katika mitumbwi hiyo.
Muuguzi wa zamu katika wodi namba tano Haika Masula alisema wamepokea
majuruhi 10 na maiti tatu mwanamke mmoja alitambuliwa kwa jina la
Salama Juakali na watoto wawili waliochini ya umri wa miaka mitano.
No comments:
Post a Comment