Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya
baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa
usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na
vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na
aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP)
Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara,
Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP)
Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi
(ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa
afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna
msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora
kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa
upelelezi Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu
Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa
mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David
Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma
Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora.
Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora,
aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi
Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa
Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack
Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni
pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki
Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya
Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki
Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni
aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi
(SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,
aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe
Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson
Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha
Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala. Mabadiliko hayo
ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la
Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora
ya usalama.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi
No comments:
Post a Comment