Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Anthony Lusekelo
‘Mzee wa Upako’ akitafakari jambo. Ishu hiyo iliyojaa utata mkubwa,
ilitokea saa nne usiku maeneo ya Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam
kwenye barabara inayotoka barabara kuu kwenda kanisani kwake.
NI kama kimenuka tu! Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC)
Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ usiku wa
kuamkia Jumatatu iliyopita alizua la kuzua kufuatia kumimina risasi
kadhaa hadharani kwa madai ya kuwatawanya kundi la vijana waliodaiwa
kumvamia na kuziba barabara kwa lengo la kumfanyia kitu mbaya.
MAELEZO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, tukio lilianza kwa Mzee wa Upako
aliyekuwa akipita kwa miguu kukejeliwa na vijana waliomwita Freemason
kauli ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliiona ni ya kejeli kwake.“Baada ya
kuitwa Freemason, yule kijana akiwa na wenzake waliendelea kumkejeli
Mzee wa Upako, akawafuata na kuwauliza mbona mnanitukana, nimewakosea
nini?”
RISASI ZARINDIMA
“Alipoona wale vijana wanazidi kumkejeli huku wakionesha dalili za
kumfanyia fujo ndipo alipotoa bastola yake na kufyatua risasi tatu juu
hali iliyowafanya wale vijana kutawanyika huku na kule.
“Baadhi ya watu walikuwa kwenye biashara zao, nao walitimua mbio,
wengine waliacha biashara, unajua risasi ni risasi tu, mtu akisikia
risasi hawezi kukaa salama hata kama ni mjeshi,” kilisema chanzo hicho.
Moja wapo ya alama zinazoaminiwa kuwa ni za Freemasons MZEE WA UPAKO ATIMUA MBIO
Ilizidi kudaiwa kwamba, kufuatia kimbiakimbia hiyo, Mzee wa Upako
naye alikimbia. Baadaye alirudi eneo la tukio kimachale na kukuta watu
wameanza kukusanyika kujua kulikoni.“Mzee wa Upako alipofika aliagiza
mtu atakayeokota ‘magazini’ ya risasi alizofyatua angempa shilingi alfu
ishirini, vijana wengine wakaingia kazini, wakapata moja, wakapewa chao,
Mzee wa Upako akasema mtu akiokota nyingine aipeleke polisi,” kilisema
chanzo.
MADAI YA WATU
Kuna madai kwamba, vurugu hizo zilipambwa na kijana mmoja anayeitwa
Robert ambapo mtumishi huyo wa Mungu alimkomalia kuwa ndiye aliyekuwa
akiongoza wenzake kumtukana na kumkashifu kwamba yeye ni Freemason na si
mchungaji wa kiroho kama anavyojiita.
MZEE WA UPAKO NA GAZETI LA AMANI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilimtafuta Mzee wa Upako kwa njia
ya simu na alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na
kueleza ‘full’ mkanda.“Ni kweli lilitokea. Ni kwamba, siku hiyo
nilipofika eneo lile kuna vijana wa kihuni walinifuata kwa nyuma,
wakaanza kupigapiga gari langu, wengine wakizuia njiahuku wakidai eti
mimi ni Freemason.
Mfano wa silaha ya moto (bastola) kama ile ya Mzee wa Upako.
“Nilijaribu kuwaambia kwamba mimi ni kiongozi wa kiroho lakini badala
yake wakaanza kuniangushia matusi. Ili kujiokoa nilifyatua risasi hewani
kuwatawanya,” alisema Mzee wa Upako.Alipoulizwa kama anaweza kujua
sababu za watu hao kumvamia na kumwambia yeye ni Freemason, kiongozi
huyo alisema:
“Siwezi kujua, lakini mara baada ya kufyatua risasi na wao
kutawanyika mimi niliamua mwenyewe kwenda Kituo cha Polisi Urafiki (Dar)
kutoa taarifa.“Mimi siwezi kujua sababu za watu hao kunikashifu na
kunitukana labda ukiwapata watakuambia lakini ni watu ambao naamini
wametumwa na mtu f’lani ambaye mimi siwezi kukwambia lakini polisi
watamjua baada ya upelelezi wao,” alisema.
Alipoulizwa alikuwa anatoka wapi usiku huo, Mzee wa Upako akajibu
kwamba alikuwa anawenda kanisani kwake Ubungo Kibangu kwenye shughuli
zake za kawaida za kiroho.
MADAI YA ROBERT
Madai ya upande wa Robert anayedaiwa kuongoza vijana wenzake
kumfanyia vurugu Mzee wa Upako yanasema kuwa, baada ya mtiti huo wa
risasi, yeye alikimbilia Kituo cha Polisi Mbezi, Dar na kufungua
malalamiko yenye Kumbukumbu Na. JMD/RB/11099/2014 KUTISHIA KUUA KWA
RISASI!Hata hivyo, Robert alipopigiwa simu ili kuulizwa kwa undani
hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu na kutumiwa meseji kwa namba
yake ya simu.
No comments:
Post a Comment