Wakinamama (kushoto) wakimficha mwenzao (mke wa mtu) aliyenaswa kwenye ghetto la njemba mwenye asili ya Kiarabu, Hemed.
Mji wa
Morogoro umekumbwa na matukio mfululizo ya mafumanizi ambapo baada ya
ticha wa shule ya msingi kufumaniwa na dereva wa bodaboda kisha jamaa
kubondwa kwa kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu vichakani na denti wa
upadri kufumaniwa, mwanzoni mwa wiki hii fumanizi lingine kiboko la
njemba mwenye asili ya Kiarabu limetokea.Kwenye Kata ya Mazimbu mjini
hapa mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Hemed, anadaiwa kunaswa
laivu na mke wa mtu kwenye chumba anachoishi kilichopo Mtaa wa Boma
mjini hapa.
Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo hivyo kufika eneo la tukio ndani ya
dakika sifuri na kunasa tukio hilo likiwa bichi.
Katika fumanizi hilo lililojaza ‘inzi’ (umati), Hemed alidaiwa kuwa
amekuwa na tabia ya kuwarubuni na kumwaga fedha mbuzi kwa wake za watu
na kuserebuka nao ndani ya ‘geto’ lake jambo lililowafanya wenye wake
zao kumwekea mtego ambao ulipofyatuka ukamnasa majira ya saa 3:00
asubuhi.
Akihojiwa na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema
kuwa, jamaa huyo alikuwa na mwanamke mzuri wa umbo aliyetajwa kwa jina
moja la Husna ambaye alikutwa chumbani kwa Hemed.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwenye eneo la tukio, mume wa Husna
aliyejitambulisha kwa jina moja la Siri alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimuaga mke wangu nakwenda Mwanza kwenye shughuli zangu za
biashara. Nikiwa Mwanza nilijulishwa na majirani kwamba mke wangu kila
siku anaacha watoto wetu kwa mama yake na kwenda kulala kwa Mwarabu.
“Ukweli kama mwanaume nilipatwa na hasira, nikatafuta ndege nikarudi hapa (Morogoro).
“Nimeelekezwa kwa Mwarabu na jamaa waliokuwa wamemwekea mtego,
nilipofika nilichungulia dirishani, nikamuona mke wangu na Mwarabu
wakiwa kitandani.
“Nilihisi kupooza mwili na roho ilikuwa inaniuma sana.”
Aliongeza: “Mimi na mke wangu tumefunga ndoa ya Kiislamu, tuna
watoto wawili, mmoja ana umri wa miaka mitano na wa pili ana mwaka mmoja
na miezi saba.
“Cha ajabu mtoto wa pili hadi sasa hatembei. Kwa tukio kama hili nahisi mke wangu amembembenda.”
Kwa upande wake Husna ambaye alisitiriwa na wanawake wenzake
waliokuwa wakimficha, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alimjia juu
mwanahabari wetu na kumtolea maneno ya shombo.
Naye Mwarabu huyo alipohojiwa, pia alimtolea vitisho ‘kamanda’ wetu.
Kufuatia wingi wa watu, wawili hao walifungiwa chumbani lakini raia wenye hasira kali wakavunja mlango na kuwashushia kichapo.
Baadaye viongozi wa Kata ya Mazimbu wakiongozwa na Afisa Mtendaji,
Brioht Sospeter na polisi mmoja walifika eneo la tukio wakawaondoa
wawili hao na kuwapeleka ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.
No comments:
Post a Comment