Na Baraka lusajo
mbeya,
WANANCHI wa
kijiji cha kyimo kata
ya kyimo wilayani Rungwe mkoani Mbeya
wamelazimika kufukia mitalo
ambayo ilikuwa imeandaliwa na idala ya
maji wilayani humo baada
ya wao kukosa huduma hiyo
kwa muda mlefu na kulazimika kutembeya
zaidi ya kilometa {4} katika kutafuta
maji safi na salama
Wakizungumza jana na
wandishi wa habari walipotembelea potembelea kata hiyo mara baada ya kujurishwa uwepo kwa ukosefu wa huduma ya maji kwa muda mlefu walisema kuwa Serikali kupitia
benki ya Dunia {WBC} iliwapatia fedha kiasi
cha Tsh,Mil,299 kwa ajiri ya ujenzi wa tenki lamaji ambalo lilitegemewa kujengwa
katika eneo hilo baada ya wao
kuto kuwa na huduma hiyo kwa muda mlefu
lakini wanashangaa baada ya huduma hiyo kukamilishwa na kuelekezwa katika
kata ya jilani ya lufingo bila wao kunufaika na huduma hiyo na kupelekea
kuchukua uamzi wa
kufukia mitalo ambayo ilikuwa
imeandaliwa na idala ya maji wilayani humo na huku wakishinikiza idala hiyo
kuelekeza maji kwanza kijijini
kwao.
Omari Kajange mkazi wa kata hiyo alisema kuwa Mkuu wa mkoa
huo Abasi Kandoro ndiye aliyewapa taarifa kuwepo kwa mradi huo na kuwa baada ya
kuona mkandarasi amejenga chini ya kiwango walimpatia taarifa na yeye
kumuagiza mkandarasi huyo ajenge upya ndani ya siku 14.
Alisema kuwa mkandarasi huyoaliyejulikana kwa jina moja la
Gulamali alikaidi agizo hilo ikiwa amefikisha zaidi ya miezi mitatu bila
kujenga Tenki hilo na hakuna hatua iliyochukuliwa na wao wakiendelea kukosa huduma
hiyo muhimu kwa kulazimika kutembea zaidi ya kilometa {4} katika kutafuta
huduma hiyo.
Kajange aliongeza kuwa kutokana na Serikali wilayani humo
kushindwa kuchukua hatua waliamua kufanya mkutano mkuu uliowatuhumu
viongozi wa kata hiyo kushindwa kuwajibika na kutaka wapatiwe majibu juu ya
hatua walizochukua kutokana na ukosefu
wa huduma hiyo.
Akijibu hoja hizo diwani wa kata hiyo Frankson Mwaitalage
alisema kuwa ni kweli jambo hilo lipo lakini lipo chini ya mkuu wa mkoa ambaye
tayari ameanza kuchukua hatua juu ya uchakachuaji huo dhidi ya mkandarasi huyo.
Mwaitarage alisema kuwa Sekretalieti ya mkoa ndiyo iliyompa
kazi injinia huyo na kuwa serikali ya kijiji ilitakiwa ipeleke lalamiko hilo
mkoani kupitia kwa mkuu wa wilaya Chrispin Meela na si kwangu.
“mimi mnanionea bule suala hili lipo chini ya mkuu wa
mkoa,mimi sina mamlaka tulichokifanya ni kuukataa mradi huo maamuzi juu ya
injinia huyo yatatolewa na mkuu wa mkoa na maji
yataanza kupatikana mpaka mpale
mladi utakapo kuwa umekabidhiwa na serikali kwa wanachi husika na sivinginevyo ”alisema diwani huyo.
Mwaitolage alimaliza kwa kusema kuwa atamuagiza mwenyekiti
wa kijiji hicho aitishe mkutano mkuu ili mambo yote yawekwe wazi kwa kuwa
tatizo hilo la huduma ya kmaji katika
maeneo hayo lipo kwake na muhtasari wa mkutano huo yatapelekwa kwa mkuu wa mkoa
kwa ajili ya maamuzi zaidi.
No comments:
Post a Comment