Saturday, July 11, 2015

RESTLESS YAWAONYESHA NJIA YA KUPITA VIJANA



WENGI WAABADILI MTAZAMO WA URAIA

Vijana wakifuatilia kwa makini mafunzo

Vijana wengi wamekuwa walalamikaji wa mambo na wala si watendaji wa mambo wanayolalamikia, wakati huohuo vijana ndio nguvu kazi katika maendeleo ya jamii lakini si washiriki wa kuleta maendeleo hayo. 

Hayo yalisemwa na Kefar Mbogela ambaye ni mratibu msaidizi wa mradi wa Fahamu Ongea Sikiliza (FOS) ambao upo chini ya taasisi ya Restless Development nchini. Ambapo alisema lengo ni kutengeneza jamii bora ya vijana na kufanya vijana kuwa vioongozi bora katika jamii na wanakuwa wafanya maamuzi katika jamii.

Mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa unalenga kuwahamasisha, kuwaelimisha na kuwafanya vijana kushiriki katika shughuli za kiraia na hasa katika mchakato wa uchaguzi mkuu Tanzania. “Mraadi huu unawataka vijana wajitokeze kushiriki kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura na kugombea kwani ni haki ya kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea kwani kijana huyo  ana sifa za kupiga kura na kugombea pia. Alisema  Kefar

Akiongea kwa hamasa alisema kuwa vijana wengi wamekuwa hawashiriki katika shughuli za kimaendeleo kitu ambacho kimewafanya vijana hao kujinyima haki ya kimaendeleo kwa kutoshiriki kwao. “matatizo ya vijana wanayajua vijana wenyewe  na mengi yanaweza kutatuliwa na vijana wenyewe iwapo vijana wataashiriki kikamilifu katika nafasi za kuleta maendeleo kwani wao ndio nguvu kazi inayotegemewa katika kuleta maendeleo kuliko makundi mengine ya watu.  



Pia alisema ni vyema vijana wakawajibika kuyatimiza majukumu yao wenyewe badala ya kuendelea kuilaumu serikali huku wakiwa hawajitokezi katika shughuli za kiserikali wakidhani ya kuwa ni jukumu la serikali kufanya majukumu kwa ajiri ya vijana kitu ambacho ni kujidanganya na kuendelea kujicheleweshea maendeleo.

Wakati wa mafunzo hayo vijana walielezwa umuhimu wa vijana kushiriki katika kupanga maendeleo  kuanzia katika ngazi ya mtaa mpaka serikali kiujumla ili kuondoa dhana ya kuwaona vijana ni watu wasiofaa katika jamii kama ilivyo hivi sasa. Hivyo aliwasihi vijana hao kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa kujiandikisha na kupiga kura kwa kuchagua viongozi sahihi.

Nae Bwana Abdul Lukanza ambaye ni afisa uhusiano wa vijana alieleza umuhimu wa nafasi ya vijana katika demokrasia kitu ambacho kiliamsha hisia za vijana wengi na kufanya maswali mengi kujitokeza miongoni mwa vijana hao.

Hata hivyo kitendo hicho kilitoa fursa kwa  Bwana Abdul kuelezea sifa na faida za demokrasia na kuwasihi vijana hao kufikisha elimu waliyoipata kwa vijana wengine ili Kuongeza uwezo na motisha kwa vijana kushiri katika mchakato wakujiandikisha, kupiga kura na kugombea nyadhifa mbalimbali, Kukuza ufahamu wa viongozi katika kazi na ni majukumu yao kuwasaidia wananchi kushiriki kikamilifu katika chaguzi zijazo.

Mafunzo hayo ambayo yalishirikisha vijana zaidi ya 50 kutoka mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Shinyanga yalifanyika mkoani Kilimanjaro, yaliwaacha vijana kuwa na hamu kubwa ya kwenda kutoa elimu hiyo baada ya kutambua kuwa vijana ndio chachu ya maendeleo.
 
“Elimu hii niliyoipata nitakwenda kuwapa vijana wenzangu ili nao fahamu zao ziweze kufumguka kama ambavyo ilivyo kwangu” alisema Salim Muhamed kutoka Manyara.
Wakati huohuo Lilian kutoka Tanga alisema kuwa elimu aliyoipata imemfungu ufahamu mkubwa na kumwezesha kutambua kuwa vijana wengi ni waongeji lakini si watendaji kitu ambacho mwisho wa siku wamebaki kuwa walalamikaji. “ Elimu hii ni lazima iwafikie vijana maana nimegundua kwamba watu wengi wanataka kufanyiwa mambo na si kufanya wenyewe ili kujikwamua kimaendeleo” AlisemaLilan

Restless ni taasisi ya maendeo ya vijana ambayo ilianzishwa mwaka 1985 nchini Uingereza kama SPW (Student Partnerships Worldwide) ambapo kwa tanzania shirika hili lilianza mwaka 1993 mjini Moshi mkoani Kirimanjaro na mwaka 1998 lilihamishia makao yake makuu mkoani Iringa ambapo lilikuwa likikusudia kutoa elimu ya afya ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi ambako ndiko makao makuu ya Restless yapo mpaka sasa.

Mradi huu wa OFS unatekelezwa katika mikoa kumi na nane (18) ya Tanzania Bara ambayo  imechaguliwa kwa vigezo maalumu vya uwakilishi wa kikanda. Mikoa hiyo ni; Mwanza,Kigoma,Manyara, Kilimanjaro,Dar es Salaam, Arusha,Mbeya, Iringa, Dodoma,Shinyanga, Mtwara, Lindi, Simiyu,Morogoro,Geita, Kagera, Tanga na Ruvuma.Katika mikoa yote hii wapo  vijana wakujitolea wanaotoa hamasa na mafunzo kwa mitandao ya vijana iliyoundwa na vijana wenyewe ili kutoa elimu ya uraia kote nchini.
 
Mbali na mradi huu pia Restdi wa lessDevelopmnt wanafanya mradi wa Mwanamke tunu, Vijana tung'are kazini, Dance for life na mingine mingi  kwa ajili ya vijana nchini

Raha ya ngoma uingie ucheze hivi ndivyo waswahili husema wakiwa wanamaanisha huwezi kukisemea kitu ikiwa hukijui na wala hujashiriki. Kwa mantiki hii vijana wanatakiwa kushiriki katika michakato ya kuleta maendeleo ya nchi tukianzia katika kuchagua viongozi

No comments:

Post a Comment