Wednesday, September 3, 2014

ATAJA SIRI YA KUISHI MIAKA MINGI, KUTOOLEWA NI MOJAWAPO


Mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani ataja siri ya kuishi miaka mingi, kutoolewa ni mojawapo!!
Mwanamke wa Mexicana, Leandra Becerra mwenye umri wa miaka 127 anaetajwa kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ameeleza siri ya kuishi miaka mingi zaidi.
Kwa mujibu wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 45, bibi huyo alimueleza kuwa siri ya ‘yeye’ kuishi miaka mingi ni kula vizuri, kulala kwa muda mrefu na kuishi bila kuolewa. Bi Leandra ambaye alizaliwa August 31, 1887 alikuwa mpiganaji wakati wa mapinduzi ya Mexico mwaka 1910-1919 na alikuwa kiongozi wa kundi la ‘Adelitas’ ambalo lilikuwa linaundwa na wanawake wanaoenda vitani na waume zao.

Bibi huyo ambaye ana wajukuu wengi huku mjukuu wake mkubwa akiwa na umri wa miaka 73, tayari ameshawazika watoto wake watano.
Mjukuu wake aliiambia gazeti la El Hozizonte la Mexico kuwa bibi huyo hivi sasa anatatizo la kubwa la kusikia.
Ameeleza kuwa bibi huyo mara nyingine hulala mfululizo kwa muda wa siku tatu huku akipewa chakula pale anaposhituka. Lakini akiamka hupenda kula mlo kamili kwa uhakika, kuimba, kutaniana na kusimulia hadithi mbalimbali zinazohusu maisha na mapambano ya mapinduzi ya Mexico.
CHANZO:BONGO5

AFUMWA NA MUMEWE AKIFUNGA NDOA KWA MARA YA PILI NA MUME MWINGINE


MWALIMU mmoja wa Shule ya Msingi Makurumla iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Maria Samuel Hoza, amejikuta akiaibika vibaya baada ya mumewe, Bryton Muhanje kumkuta akiwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa nyingine kwenye Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga, Jumamosi iliyopita.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Makurumla, Maria Samuel Hoza akiwa katika harakati za kufunga ndoa yake ya pili.

Gazeti hili lilimshuhudia Muhanje, akiingia kanisani na kwenda moja kwa moja mbele ya altare na kumzuia Padri Richard, ambaye alikuwa amemaliza kufungisha ndoa ya kwanza, asifanye hivyo kwa maharusi wanaofuata kwa vile ni batili.

Chanzo chetu makini cha habari kililidokeza gazeti hili juu ya kuwepo kwa mpango wa mwanamke ambaye yupo katika ndoa, kutaka kuolewa tena na mtu mwingine bila mumewe kujua. Kufuatia habari hiyo, kikosi kabambe cha Oparesheni Fichua Maovu kilifanikiwa kupata namba ya mwanaume huyo na kufanya naye mawasiliano ili kujua ukweli wa madai hayo.
Mume wa Maria Samuel Hoza, Bryton Muhanje (kulia) akitoa pingamizi la ndoa ndani ya Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga.
Muhanje alikiri kupata tetesi hizo, lakini alikuwa akihaha kujua sehemu itakakofanyika harusi hiyo na kwamba timu ya vijana wake ilijipanga kuhakikisha anafahamu eneo hilo.Baadaye aliwaeleza OFM kuwa alikuwa alisikia ndoa hiyo ingefungwa Magomeni, hivyo alikodi pikipiki sita zilizofanya doria katika makanisa yote yaliyopo eneo hilo ili kujua mkewe alikuwa kanisa gani.
Pamoja na hivyo, mwanaume huyo pia alikwenda hadi shule anayofundisha mwalimu huyo na kwa kuwa hawamfahamu, alijitambulisha kama ndugu yake na kwamba alikuwa anaomba kujua kanisa ambalo (mkewe) atafunga ndoa, kwani ameelezwa kuwa lipo Magomeni lakini hakuelewa ni lipi.
“Wanafunzi wa pale wakaniambia siyo Magomeni, bali ndoa inafanyika Kigogo Luhanga, ndipo nilipowasiliana na wenzangu na kuwaeleza habari hiyo, nikaongozana na baadhi ya wanafunzi ambao pia walikuwa wanakwenda kwenye harusi hiyo,” alisema.
Padri Richard akitoka nje ya kanisa hilo mara baada ya pingamizi la harusi kutokea.
OFM ikiwa tayari kwa kunasa tukio hilo, walikuwa wameshatinga kanisani hapo mapema na kushuhudia maharusi watatu tofauti wakijiandaa kufunga ndoa, wakiwemo Maria na mwenzake.
Ratiba ilionyesha kwamba ndoa ya wawili hao ilikuwa ya pili, hivyo mara tu zamu yao ilipofika na Padri Richard kuanza kutoa risala ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia, wote walionekana kuwa na bashasha ya siku hiyo muhimu ya kuungana.

Ghafla bila kutarajia, wakati wasaidizi wa padri wakimletea kibakuli chenye pete ya ndoa, Muhanje alijitokeza na kumuomba mchunga kondoo huyo kusitisha zoezi hilo kwa vile anayetaka kufunga ndoa, ni mke wake halali.
Makamanda wa Polisi wakiwa nje ya kanisa tayari ili kutuliza ugomvi.
Akiwa amepigwa na butwaa, padri huyo alilazimkika kwanza kumuuliza bibi harusi kama anamtambua mtu aliyesimama mbele yake, lakini akiwa mkavu alikataa akidai hajawahi kumuona maishani mwake.
Mume akiwa ameongozana na mpambe wake aliyesimamia ndoa yake, alimuomba padri atoe vielelezo kuthibitisha ukweli huo na baada ya kupewa nafasi hiyo, alionesha picha mbalimbali za siku ya harusi yao, nakala ya cheti cha ndoa na akaomba pia aruhusiwe atoe kompyuta yake mpakato ili achezeshe video ya siku hiyo ya Oktoba 29, 2009 alipofunga naye ndoa katika Kanisa la KKT Kimara Korogwe, Dar.

Kwa ushahidi huo, padri huyo alikubaliana naye na kusimamisha zoezi hilo na kuwataka kuongozana kwenda ofisini kwa mazungumzo zaidi. Baada ya mazungumzo marefu ofisini, padri huyo alikubaliana na hoja za mume na hivyo kusitisha zoezi hilo, akidai mwanamke huyo hawezi kuolewa kwa mara ya pili.
Ilifahamika baadaye kuwa Maria, ambaye amezaa mtoto mmoja na Muhanje, alitumia jina la Neema Stanley Hoza katika kusudio lake la kufunga ndoa ya pili.
Baadhi ya wapambe na wanandugu wakirudi makwao mara baada ya ndoa kubatilishwa.
Hata hivyo, wakati kukiwa na sintofahamu ya tukio hilo kanisani, ghafla kikosi cha askari polisi wakiwa katika ‘difenda’ kilitia timu kuhakikisha usalama unakuwepo.Askari hao walisema walipewa taarifa za kuwepo kwa tukio ambalo lingeweza kuhatarisha amani na ili kuhakikisha jambo hilo linatokea, waliondoka na maharusi wa pili baada ya taratibu za kikanisa kukamilika.
Baada ya tukio hilo, Muhanje alisema alimuoa mkewe mwaka huo, baada ya kuwa ameishi naye kinyumba kuanzia mwaka 2005.“Baada ya kukaa naye kwa miaka minne, tukaamua kufunga ndoa mwaka huo wa 2009 na baada ya hapo, yeye akaenda kufanya kazi ya ualimu Lushoto katika Shule ya Shambalai.
Picha ya ushahidi ikionesha ndoa ya halali kati ya Bw. Bryton Muhanje na Mwl. Maria Samuel Hoza.
“Mwanzo tulikuwa na maisha mazuri tu na katika kipindi hicho, nilijitahidi kumfanyia utaratibu wa uhamisho ili aje Dar na kufanikiwa kumleta mwaka 2012 na alipangiwa Shule ya Makurumla.“Baadaye kidogo hali yangu kifedha ikayumba, ndipo matatizo yalipoanza kwani kitendo cha kutegemea hela za mshahara wake katika maisha kikamshinda, akaanza kutafuta visa mbalimbali ili mradi mimi nimpige apate sababu ya kuondoka.
“Alifanya vituko vingi sana, wakati mwingine alifunga mlango na kuondoka na funguo na kwenda kwa dada yake na kulala huko huko, wakati mwingine aliamua tu kuvunja vitu bila kujali hadi mwaka jana mwezi wa nne alipoondoka moja kwa moja kwenda kusikojulikana.“Siku chache zilizopita ndipo nilipopata habari kwamba ana mpango wa kuolewa, ndipo nikaanza kufuatilia ili nijue.

“Nilipokuwa pale kanisani wakati wa kuzuia ndoa, yule mwanaume aliyetaka kumuona mke wangu, alinitishia kuwa atanikomesha, nimeenda polisi kuripoti maana siwezi kujua atafanya nini na nimefungua jalada lenye namba MAG/RB/8452/2014 KUTISHIWA KUUA KWA MANENO.”

Tuesday, September 2, 2014

STAR WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO AWA KIVUTIO MITAA YA KARIAKOO

Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati) akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwaajili ya kununua zawadi Kwaajili ya Wazazi wake.
Mfanyakazi wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa katika matembezi Kariakoo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi kwaajili ya wazazi wake
Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi kwaajili ya Wazazi wake
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao.
Matron wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.

PICHA ZIKIONESHA JINSI SHOW YA DIAMOND ILIVYOVURUGWA NCHINI UJERUMANI

SINCE DIAMOND ALICHELEWA KUFIKA UKUMBUNI WATU WALIKASIRIKA SANA NA KUANZA KUFANYA FUJO KUHARIBU VENUE IKABIDI POLISI WAITWE NA AMBULANCE NA KWAVILE WATU WALIKUWA WANA HASIRA IKABIDI DIAMOND ATOLEWE PALE NA POLICE ESCORT SO NILIVYOELELEWA NIKWAMBA HATA SHOO HAKUWEZA KUFANYA TENA,,HII INASIKITISHA NINA MASWALI MENGI SANA JE PROMOTA NDIO ANA KAZI YA KUMLETA MSANII KWENYE VENUE INAKUWAJE WALIMCHELEWESHA KUJA UKUMBINI?NA HIVI MNAMHARIBIA MSANII REPUTATION YAKE NA BRAND YAKE NA NYIE WENYEWE PIA,,JAMANI ITS TIME FOR CHANGES INTHIS INDUSTRY,,NA SIKU NYENGINE DIAMOND USIKUBALI KABISAA KUCHELEWESHWA WEWE SIO MGENI BALI NDIO STAR WA SHOW AND PEOPLE CAME TO SEE YOU SO UNA POWER KUBWA SANA AU WEKA KWENYE MKATABA WAKO MIMI NAPANDA STAGE MDA HUU NA WAO WATANGAZE ILI WATU WAJUE,,,

NDEGE ILIYOPOTEA IKITOKEA JIJINI MWANZA hii hap



Ndege iliyopotea mapema leo ikitokea Mwanza kuelekea Magadi nchini Kenya, imepatikana huko eneo la Serengeti Mara, na abiria wote watatu wamekufa.

KAPINGA KANGOMA MWENYEKITI MPYA CCM UK - AIBUKA NA USHINDI WA KISHINDO WA ASILIMIA 94.6% YA KURA ZOTE HALALI

.

Aanza kwa kuunda timu itakayounda upya Jumuiya ya Watanzania UK na kuhusisha wadau wote;Azungumzia suala la uraia pacha na Rais Ajaye katika uchaguzi 2015;Kuunda Saccoss ya watanzania UK na Jumuiya ya Wanawake.Na Abraham Sangiwa Itikadi Siasa na Uenezi - CCM – UNITED KINGDOM.

 Mwenyekiti Mpya wa CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma akitoa nasaha na shukrani zake.
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM UK Ndugu Maina Owino akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti Mpya CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma.
 Wajumbe, wanachama wa CCM UK na watanzania waishio uingereza wakimsikiliza Kwa makini Mwenyekiti Mpya wa CCM Ndugu Kapinga Kangoma (hayupo pichani).
 Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Maina Owino akipiga kura yake katika Uchaguzi wa Mwenyekiti Mpya wa CCM UK.
 Kaimu Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela(mwenye koti jeupe) akichukua taarifa ya yanayojili katika mkutano huo pembeni yake ni Ndugu John Lyimo Katibu wa Uchumi na Fedha CCM UK.
  Katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM UK Ndugu Abraham Sangiwa akitekeleza haki yake ya kikatiba kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti Mpya CCM UK.
 Meza kuu ikimkaribisha Mwenyekiti mpya wa CCM UK Ndugu Kapinga Kangoma kuchukua Nafasi yake kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti CCM UK Ndugu Sukwa Said Sukwa, Mwenyekiti mstaafu Maina Owino na Abraham Sangiwa – Itikadi na Uenezi CCM UK.
 Katibu wa CCM Shina la Birmingham Bi. Lilian Barongo ambaye pia anakuwa Katibu mteule wa Jumuiya ya Watanzania UK Akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu wa CCM UK  Ndugu Leybab Mdegela kabla ya kuingia katika ukumbi wa mkutano
 Wanachama, wajumbe na watanzania waliohudhuria mkutano wakipata maankuli ya ukweli.
 Café 12 misosi na vinywaji palikuwa hapatoshi.
Baadhi ya wanachama na watanzania walipatiwa uhakiki kabla ya kuingia ukumbini.


==============
Mkutano mkuu wa wanachama wote CCM UK ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM UK umefanyika katika jiji la Reading siku ya Jumamosi tarehe 30/08/2014 ambapo wagombea watatu walipitishwa na vikao vya awali kugombea nafasi hiyo ni Ndugu Said Surur, Peter Gabagambi na Kapinga Kangoma na kujaa shamrashamra na nderemo na  kuhudhuriwa na wanachama wa CCM UK NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA pia viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM aliyeng”atuka Ndg  Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti  Ndugu Said Sukwa, Kaimu Katibu Ndugu Leybab Mdegela,  Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu Mohamed Upete, Viongozi wa mashina, wajumbe na wanaCCM toka mashina ya CCM UK.

Mkutano huo ulianza kwa  Katibu mwenezi ndugu Abraham Sangiwa kuwashukuru Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni  na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi hapa UK ili kuleta chachu ya mabadiliko ndani na nje ya chama kwa manufaa ya watanzania wote kwa ujumla.

Ndg Sangiwa aliwakumbusha kuwa kujiunga na CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.

Akimkaribisha Mwenyekiti mstaafu Ndugu Maina A Owino, Kaimu Katibu wa CCM UK Ndugu Leybab Mdegela aliwashukuru wanachama wote kwa kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha malengo ya mkutano huo na zoezi la kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM UK na kuwafahamisha wanachama wagombea wawili Ndugu Said Surur na Peter Gabagambi waliopitishwa na vikao vya awali wamejitoa katika kinyanganyiro hicho hivyo mgombea pekee aliyebaki katika nafasi hiyo ni Ndugu Kapinga Kangoma, pia ripoti ya Tawi iliwakilishwa na itasambazwa na viongozi wa mashina kwa wanachama wote.

Katika hotuba yake Mwenyekiti mstaafu Ndugu Maina A Owino aliwashukuru wana ccm na watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano waliompa katika awamu yake ya kwanza ya uongozi tangu kuanzishwa kwa tawi hapa UK ambapo awamu yake imefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wana CCM na watanzania kwa ujumla katika miji mbalimbali hapa UK ; Aidha alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko endelevu, kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na kwamba CCM na serikali yake inaendelea kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM UK Kuwa mchango wao unahitajika na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na kichumi kuanzia na watanzania wanaoishi hapa UK na nyumbani.


Katika hotuba yake ya ushindi Mwenyekiti Mpya wa CCM UK ndugu Kapinga Kangoma aliwashukuru wana CCM UK kwa Imani waliyoionyesha kwake na kumpa kura za ushindi na kusema “hakika kwangu na familia yangu ni heshima kubwa. “
Sasa tuna kila sababu ya kuanza awamu ya pili ya Uongozi wa CCM UK Kuunganisha maisha ya watanzania hapa UK na diaspora kwa ujumla na kutengeneza platform itakayoleta uongozi mahiri kuelekea hiyo awamu mpya, hivyo napenda kuwajulisha kwamba awamu hiyo imeanza leo kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wenu.
Ninaanza kazi yangu kwa kuunda upya Jumuiya ya watanzania hapa UK hivyo CCM UK itaweka uzito wote unaostahili kuhakikisha kuwa tunaunda jumuiya itakayotokana na Watanzania wenyewe na sio kushirikiana na ubalozi.. hatutaki tena kukaa na ubalozi eti kutengeneza jumuiya ya Tanzania hapa UK, uzoefu unaonyesha kuwa tukishakuwa na ubia na ubalozi malengo ya jumuiya yanakuwa sio endelevu..hasa kama anapatikana balozi ambaye hana interest na jumuiya za Kitaanzania; basi inakuwa rahisi sana kuibomoa. Hivyo leo naanza kazi kwa kuunda jumuiya ya watanzania hapa UK, ambayo itafanya kazi ya kuunganisha mikakati na taasisi zingine zenye malengo tofauti na CCM (hapa UK) ili mradi mwisho wa siku waje na jumuiya ambayo haina harufu ya serikali japo watafanya kazi na ubalozi kama wadau pale inakapobidi na terms and conditions will-apply. Hivyo namteua bwana Abdulaziz Jaad kuanza mchakato huo yeye ni msomi mzuri na ana uzoefu wa hapa na kule nyumbani kwani sehemu zote mbili ameshafanya kazi kwenye taasisi mbalimbali nitamsaidia kwenye kila hatua ili afanikiwe na jumuiya ipatikane haraka. Naomba nimtambulishe kwenu ili mtakapomuona analeta mapendekezo kwenye miji yenu msimwangushe ili tuanze rasmi kutumikia kizazi chetu na kijacho; kwa kuanzia atasaidiwa na Hussein Chang’a toka Reading na katibu wa kamati hiyo atakuwa Mwanasheria Lilian Barongo toka Birmingham; wote hao ni wasomi wazuri sana nina hakika watakuja na SCIENTIFIC APPROACH kuhusu suala hilo.

Suala la pili ni kuifanya diaspora kuwa soko au kutumia fursa za sanaa kwa vijana wetu wa nyumbani na wa hapa ili kuendeleza vipaji walivyonavyo kwa kuunganisha soko la UK la music na sanaa zingine na lile la nyumbani. Mfano ni wenzetu wa nchi kama Nigeria na hata Ghana ambapo diaspora zao zimeshiriki katika kutambulisha vipaji vya nchi zao katika masoko ya dunia. Hivyo diaspora ya Tanzania lazima ifanye kazi za kuunganisha masoko ya nchi zetu kwa kuanza kufungua njia za bidhaa mbalimbali ikiwemo sanaa. Nitaunda timu ya vijana wa ccmUK na wengineo ili waanze kuandaa strategy ya mpango huo na timu nyingine ambayo itaanza kujenga mfumo wa kuunganisha mtandao wa masoko ya bidhaa mbalmbali kwa kutumia mtandao wetu hapa UK.

CCM na rais ajaye..
Ndugu wana-CCM-UK na watanzania wenzangu kama mnavyojua kwamba nchi yetu mwaka ujao itaingia kwenye kinyang’anyiro cha kumpata rais mpya baada ya mchapa kazi Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kikatiba..na kwa vyovyote ccm ndio itakayoleta rais mpya..kwani vyama vingine bado vina safari ndefu mpaka kuja kuongoza TZ. Na tukumbuke kuwa rais ndiye muhimili wa mambo yote ndani ya nchi na hivyo akija rais bomu mafanikio yaliyopatikana katika nchi yetu yatapotea...niwakumbushe tu kuwa rais anayemaliza muda wake ametekeleza vizuri sana majukumu yake yaliyomo kwenye ilani ya uchaguzi hivyo chama kinahitaji mtu bora zaidi ya Jakaya ili aweze kuendeleza pale atakapoishia Jakaya kikwete. Na sasa nchi ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza kuuza gesi na labda baadae mafuta hiyo ni changamoto kubwa sana kwa rais ajaye. Sasa kuna makundi mengi yanayojionyesha kuutaka urais wa kupitia chama chetu na wote wanasifa mbalimbali kikubwa sio wao kujinadi maana mtu akijinadi hataji mabaya yake atajisifia na kuonyesha mambo yako safi..kumbe anaficha mambo mengi na ukichukulia watanzania  wa vijijini hawana uwezo wa kuwang’amua na kuwapembua..Hivyo diaspora ya Tanzania tuna jukumu la kusaidia kupeleka  pressure kuhakikisha watu wenye dhambi na wasio na uwezo wasipate nafasi hiyo nyeti. Issue hapa sio tu ufisadi bali pia uwezo wa kuongoza nchi. Maana mtu anamsema mwenzake kuwa ni fisadi as if kipimo tumeshakiweka kwamba kama wewe sio fisadi basi hata kama ni mjinga basi unaruhusiwa kuupata urais wa Tanzania; Hiyo sio kweli;  we need a capable person with integrity. Sisi hapa UK na sehemu zingine za huku ughaibuni tunawajua sana hawa viongozi kwani wanafika sana na tumeshaongea nao mara nyingi. Authenticity zao tunazijua, How reliable they are tunawajua, lakini pia tuna access ya information kuliko wale wa vijijini..hivyo tukinyamaza hatuitendi haki jamii yetu na tunaongeza mzigo kwa watoto wetu hapo baadae waanze tena kupambana na majanga hayohayo ya viongozi wabovu kwani tukiwaacha leo bila ya kuwasema watawaweka na hata watoto wao... hivyo ninaunda idara ya siasa ambayo itaratibu matamko mbalimbali ya kichama yenye lengo la kujenga na sio kumhujumu mtu yeyote.. 

Hope hiyo itasaidia kujenga siasa bora ndani ya chama cha mapinduzi. Nitaboresha idara ya fedha ili kuhakikisha chama kinajitegemea ikiwa ni pamoja kuanzisha SACCOS itakayoanza kujenga mitaji ya biashara na hata baadae kuwa na benki yetu hapa UK maana tunaweza kuwa na skills lakini bila mitaji inabaki kuwa ndoto za alinacha. Pia nitaimarisha idara ya miradi ili iweze kusaidia kuingiza  ideas za watu mbalimbali kwenye uchumi wa chama kwa ubia na watu hao. Hivyo wanachama mnakaribishwa kuleta ideas zenu. 

Nitaboresha pia idara ya wanawake na watoto ili kupata mchango kutoka kundi letu muhimu na mnajua uki-mpromote mwanamke umemsaidia pia mtoto. Hivyo mchango wa jumuiya ya akina mama tunaihitaji sana hapa ccm UK. Sijapata mtu wa kuziba nafasi hiyo nitashauriana na wadau wenzangu kumpata mama atakayefaa kusuka jumuiya hiyo ya chama na kuieneza kwenye kila mji ambao una shina la ccm,,ndo maana sikuweza kukurupuka na jina lolote ili kuleta maana nzuri ya nafasi hiyo. Jina au team nzima ya UWT itafuata baadae.


Mwisho nimalize kwa hoja ya uraia pacha kwani hivi karibuni mheshimiwa rais wa Tanzania amekuwa na nafasi mbalimbali za kuzungumzia diaspora, kwanza kule marekani na hatimaye juzi pale Dar es salaam. Mambo muhimu aliyoongelea ni kuhusu watu wa diaspora kuto kuongelea mambo yetu kwa uzito unaostahili. Japo sikubaliani na mhesh. 

Rais kuhusu dhana ya kuwakataza wana-diaspora kuhoji mambo mbalimbali ya nyumbani kitu ambacho ni haki yetu ya msingi,,lakini naomba pia nimuunge mkono mhesh.Rais kwamba ni kweli Watanzania wa diaspora hatujahamasika vya kutosha na kushiriki kwenye uwanja wa habari muhimu za mambo yanayotuhusu bali tumekuwa wepesi wa kujadili mambo madogomadogo tu.

wengi wetu ni wepesi sana wa kutoa kauli nzito vichochoroni lakini hatufanyi hivyo hadharani. Woga huu lazima tuuache kwani hoja zisipojadiliwa na mzazi zinabaki zikimsubiri mtoto wako akue halafu aje afanye kazi hiyohiyo!!!kwanini tusimalize majadiliano sasa? Hivi sasa kwenye mitandao ya jamii kuna hoja nyingi zinajadiliwa na watu walioko nyumbani wakiituhumu diaspora na kuonyesha kuwa hatupaswi kupewa uraia pacha kwani nchi haitakuwa salama..

lakini hoja za kuhoji mantiki hiyo zinakuwa chache sana kutokea upande wa diaspora. Hivyo nichukue nafasi hii kuwahimiza tuongeze kasi ya kutumia mitandao ya kijamii kwani hoja zinazotuhusu zinaandikwa na watu wengine na hivyo wanapotosha. 

Nawashukuruni sana wote naomba nifunge kikao na turejee kwenye miji yetu salama.

IMETOLEWA NA ABRAHAM SANGIWA IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI CCM TAWI LA UINGEREZA
01.09.2014.
  

WAPIGANAJI WATEKA WIZARA ZA SERAKALI


Wapiganaji nchini Libya wameteka ofisi na majengo ya wizara za serikali mjini Tripoli.
 Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya nchi hiyo.
Watu waliokuwa wamejihami waliwazuia wafanyakazi kuingia katika ofisi za wizara hizo.
Mnamo siku ya Jumapili, wapiganaji hao waliteka makao ya ubalozi wa Marekani.
Libya imekumbwa na vurugu tangu kung'olewa mamlakani kwa hayati kanali Muammar Gaddafi aliyepinduliwa na wanajeshi wa Nato wakisaidiwa na wapiganaji wa kiisilamu mwaka 2011.
Wapiganaji hao wamekuwa wakipigana miongoni mwao wenyewe wakitaka mamlaka.
Maafisa wakuu wa serikali na wabunge walihamia katika mji wa Tobruk, Mashariki mwa nchi hiyo mwezi jana.
Marekani na mataifa mengine yalilazimika kuwaondoa wafanyakazi wao kutoka nchini humo mwezi Julai huku mapigano yakichacha mjini Tripoli.
Benki kuu ya Libya pamoja na kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali ziko mjini humo.
Waziri mkuu Abdullah al-Thinni na baraza lake la mawaziri, walijiuzulu wiki jana ili bunge liweze kuteua serikali mpya.
Uchaguzi huo ulikuwa wa pili tangu kanali Gaddafi kuuawa katika mapinduzi ya mwaka 2011. Matumaini ya uchaguzi huu kurejesha uthabiti nchini Libya ni hafifu mno.