Saturday, November 1, 2014

DENI LA PESA LAASABABISHA MAREHEMU KUGOMBEWA MAHALI PA KUZIKWA


Mtoto mwingine wa marehemu, Hassan Hatibu, akizungumza jambo na mtandao huu.

Ndugu na jamaa wakiwa katika mzozo huo. 
 
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Mohamed Said ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake wa upande wa mama yake kwa kugombea maiti ya mama yake mzazi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mzozo huo umeibuka baada ya kijana huyo kuwagomea ndugu zake kuuzika mwili wa marehemu mkoani Iringa mpaka hapo watakapomlipa shilingi laki tatu kama gharama za matibabu ya marehemu.

ASKOFU GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKE


Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’.
Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya Upako, George David ‘Geor Davie’ yenye makao makuu yake jijini Arusha ndiye aliyetajwa na mahakama hiyo kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ya Pamella ambaye alikuwa ni sekretari wa kiongozi huyo wa dini baada ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ukionesha mapenzi kunaswa kwenye simu ya mwanamke huyo ukitokea kwa Geor Davie.
KIMENUKA! Ndoa iliyodumu kwa miaka 15 kati ya Wiston Lotta (52) na Pamella Geofrey (40) imevunjwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kufuatia ushahidi mzito uliotolewa mahakamani hapo kumridhisha Hakimu Hawa Mghuruta.
Askofu Geor Davie akiwa na wasaidizi wake. Ushahidi uliotolewa na mwanaume ulidai kuwa mgogoro wa ndoa yake ulitokana na mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Askofu Geor Davie. 
Akisoma hukumu ya kesi hiyo Namba 01 ya mwaka 2012, Hakimu Mghuruta alisema kabla ya hukumu, mahakama ilizingatia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mlalamikaji.Mke wa mtu Pamella Geofrey (katikati) anayedaiwa kutoka kimapenzi na boss wake, Askofu George David ‘Geor Davie’. 
Alimtaja mtoto wa kwanza wa wanandoa hao, Sifael Wiston (15) kwamba naye aliieleza mahakama hiyo namna mama yake alivyokuwa akizini nje ya ndoa kwa kukutana na Geor Davie ndani ya gari lake lenye rangi ya silva wakati wa usiku baba yake akiwa safarini. 
Mtoto huyo alianika kwamba, walikuwa wakipelekewa juisi na bajia ndani ya gari hilo lenye pazia kisha wao kufunga vioo kwa muda mrefu huku likionekana kutikisika, ushahidi ambao uliwashangaza waumini wa kanisa la askofu huyo.
Askofu George David ‘Geor Davie’ akitoa huduma ya maombezi kwa waumini. Wiston ambaye alikuwa msaidizi wa Geor Davie, alifungua kesi ya kudai talaka kwa Pamella ili kufikia ukomo wa shauri hilo ambalo lilianza kusikilizwa na Baraza la Usuluhishi wa Ndoa mwaka 2007 lakini ilishindikana kwa vile mkewe alipeleka sababu za uongo kuwa alikuwa akinyanyaswa hivyo kuikimbia nyumba. 
Hakimu Mghuruta ameamuru mali zote yakiwemo magari matatu, nyumba iliyopo Sakina na vitu vingine zibaki chini ya mlalamikaji lakini Pamella anaruhusiwa kwenda kuwasalimia watoto wake. Hata hivyo, mahakama ilimtaka Pamella kutowarubuni watoto hao kiasi cha kuathiri masomo yao

VICTOR MBAGGA MWANAMUZIKI WA INJILI ALIYEPANIA KUWAKOMBOA VIJANA WA TANZANIA .



Ni kijana mwenye makao yake mwanga mkoani kirimanjaro na alianza huduma ya uimbaji mwaka 2002 huku akiwa na nia ya kukiokoa kizazi cha vijana wasiojiweza.
Brother Victor Bagga kama anavyojulikana ameamua kujitolea kufanya kazi ya kumtangaza Kristo kwa watu ili kuwaweka huru waliofungwa kama lisemavyo neon la Mungu.
“ Nina mzigo mkubwa sana  moyoni mwangu wa kutaka wasiojiweza wajue kuwa wanatumaini kwa Yesu na si kwa mwanadamu, wapo vijana wengi sana wanamaisha yakusikitisha kisa hawajui yakuwa Kristo Yesu ndio tumaini kuu 
Kujitambua kwa kijana ni kitu muhimu sana lakini vijana wengi wameshindwa kujitambua kwa kuwa wanaishi nje ya mpango wa Mungu. " Ukishajua umezaliwa ili ufanye nini huwezi kuhangaika sana na dunia ila shetani hataki vijana wajitambue matokeo yake  amewatwisha mizigo mikubwa na ndio wanaoongoza kwa kilio cha maisha magumu." alisema Brother Victor


Pia alisema huwa anatumia kipaji chake cha uimbaji kuwatia moyo watoto watogo na walemavu kwani ni makundi ambayo yamesahaulika sana katika jamii yetu. "ukweli ni kwamba ukifanikiwa kuyafanya makundi haya yakatambua vipaji vyao mapema na wakavitumia kwa usahihi hawatahangaika kutafuta kazi za kuwainua kiuchumi, kwani kipaji cha mtu na elimu ndio njia pekee ya kumuondolea mtu umaskini kuliko kusubiri ajira kutoka kwa mtu mwingine kitu ambaho ni kilio kikubwa kwa vijana.


 



 

Hata hivyo anafurahia kuwa chini ya uangalizi wa kanisa la Mount Zion church kwa mchungajji H. Kimario ambaye amekuwa msaada mkubwa sana kwake katika huduma zake ili kuweza kutimiza maono yake ambayo ni kuwa mwimbaji wa kimataifa na kuweza kusaidia vijana wenye kupoteza mwelekeo wa ndoto zao haswa katika uimbaji na watoto walemavu.
 

 Brother Victor amesema katika huduma yake zipo changamoto ambazo akifanikiwa kuzitatua ataweza kuwahudumia vijana wengi ili nao waweze kuwasaidia wenzao


"Natamani sana huduma hii iwe ya kimataifa na itawezekana ikiwa nitaungwa mkono na watu wote kwani hatuwezi kuuondoa umaskini kwa makundi haya kwakuwa ni watu wasio na kitu na hata maandiko yanasema "asio na kitu hatapewa kitu na hata aliye na kidogo hicho nacho hunyang'anywa hupewa aliyenacho" hivyo nilazima tuwasaidie watu hawa kujua vipaji vyao pia ili viwasaidie wawe na kitu ili wapewe kitu" alisema Victor

Hivyo anaomba kuungwa mkono na watu wote katika kufanikisha maono yake na changamato hizo ni pamoja na vifaa vya Muziki, pesa pamoja na mahali pa kuwatunzia vijana hao kwani wengi hawapo mahali pamoja.

Victor Mbagga kijana mwenye asili ya Tanga ana albam mbili mpaka sasa na  anatarajia kuzizindua zote kwa mpigo mwezi ujao na anatamani sana kama atapata nafasi ya kufanya kazi pamoja na Christina Shusho, John Lisu pamoja na Upendo Kirahilo kwani ndio miongoni mwa waimbaji ambao wamekuwa kivutio sana kwake na kusaidia kukuza kipaji chake cha uimbaji. "ipo siku nitawashirikisha waimbaji hawa katika nyimbo zangu nasubiri kibali toka kwa Mungu tuu" alisema

Yupo tayari kwa mialiko popote duniani ili kuzidi kumtangaza Kristo Yesu. Mpigie +255766480206

 

Friday, October 31, 2014

GADNER. G. HABASH KUSIKIKA EFM 93.7 KUANZIA LEO

Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi 
Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema wameamua kumchukua Gardner kwasababu ni miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye kipaji cha hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho 
“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu”alisema 
Gardner alimaarufu “KAPTENI” alianza kazi na kituo cha Radio Clouds fmna baadaye Times fm ambapo kwa sasa ametua Efm akitanguliwa na wakongwe kama Dj Majey,Dizzo One,Sos B,Denis Ssebo,Maulidi Kitenge,Omari Katanga,Scholastica Mazula na Kanky Mwaigomole.
Taarifa na
Meneja Uhusiano.
Kanky Mwaigomole.

MTANGAZAJI MAARUFU BEN KIKO AFARIKI DUNIA

Ben Kiko enzi za uhai wake. ALIYEKUWA mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania, Ben Kiko, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Oktoba 31, 2014 akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Kiko amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

BASI LA SIMBA MTOTO USO KWA SUO NA LORI


Ajali mbaya imetokea eneo la daraja la Wami basi la Simba Mtoto na Lori baada break za Lori kufeli,
Dereva wa Lori amepoteza maisha hapohapo.


Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.

BROTHERS FOR CHRIST WAITAMBULISHA TANZANIA NCHINI MAREKANI KWA KUCHUKUA TUZO

 
 Kama ilivyokawaida kwa mashindano mengine watanzania kuwa wasindikizaji na washuhudiaji wa wengine kuchukua tuzo huku wao wakiambulia patupu, kwao Brothers For Christ imekuwa tofauti baada ya kuchukua tuzo katika mashindano ya PRAYZ FACTOR PEOPLE CHOICE AWARDS nchini Marekani.

Kundi hilo ambalo maskani yake ni Tegeta jijini Dar es salaam lilifanikiwa kuchukua tuzo mbili katika Afro category na International Category na kuwaacha watu kuachwa na mshangao huku wakiwa hawaamini kilichotokea. Tamasha hilo lilifanyika tarehe 22/9/2014 lilifanya nyimbo za B4C kupigwa sana na vituo vya media nchini marekani na kulifanya kundi hilo kujizolea mashabiki wengi nchini humo kitu ambacho ni tofauti na hapa Tanzania.
 
Brothers for Christ walijaribu kutupa kete yao huko baada ya kuona tangazo katika mtandao kuwa kuna mashindano hayo ndipo walipotuma Video yao ya YOTE YAWEZEKANA ili ichaguliwe kuingia katika mashindano hayo.
Waswahili husema  “kama bahati vile” wimbo huo ulichaguliwa katika vipengele viwili ambavyo nao waliwaonyesha wamarekani na wahudhuriaji wote ya kuwa hakika Yesu Kristo anahubiriwa Tanzania kupitia nyimbo.

"Tulipokuwa tumepanda jukwaani watu walionekana kuwa na mshangao wakiwa hawaamini kile kilichokuwa kinatokea baada ya umahili na ustadi tuliouonyesha katika kuimba live, wengi walituuliza tulipotoka tukawajibu Tanzania wakashangaa" alisema Justin Kaego 

Kundi  hilo ambalo liliiwakilisha vyema Tanzania halina jina kubwa nchini lakini limefanya mambo makubwa yakushangaza kwani wapo wanamuziki wakongwe waliowahi kushiriki katika mashindano kama haya na hawakuweza kurudi na tuzo.
Brothers For Christ (B4C) ni kundi la vijana 14 wakiwemo watanzania 8, wakenya 2 na wacongo 4 ambao wameunda kundi hilo likiwa chini ya Dockta Mponzi ambaye pia ni mzee wa kanisa la Mlima wa moto Asseblise of God Mikocheni Dar Ambaye ndiye mlezi wao. Ni vijana wasiojua kuimba kwa kutumia mshindo nyuma, wenyewe husema “ live bila chenga”.  Wapo tayari kwa mialiko ya aina yoyote kwani nia yao kuu ni kukiokoa kizazi cha watanzania kupitia uimbaji. Hivyo wasiliana nao kwa +255767600604 na +255753599542 wapo tayari kwenda popote kwa ajiri ya Kristo Yesu.