Tuesday, November 4, 2014

RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA LEO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wazee wa mji wa Dodoma leo Novemba 4, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
 Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani wakati wa  Mazungumzo kati ya RaisJakaya Mrisho Kikwete na  wazee wa mji wa Dodoma leo Novemba 4, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo

‘MTOTO WA NDEGE’ AOKOKA


Stori: Haruni Sanchawa na Denis Mtima
MTOTO Happiness Lyoba (10) ambaye aliripotiwa kuwa mwingi wa vituko vya maajabu, ikiwamo kuonekana akishuka katika ndege huko Zanzibar, ameripotiwa kuokoka katika Kijiji cha Mkokozi, wilayani Mkuranga, Pwani.
Mtoto Happiness Lyoba (10) akisoma Biblia.
Akizungumza na gazeti hili, mama wa mtoto huyo, Salah Zefania alisema mwanaye huyo alitoroka tena Septemba 16, mwaka huu na kukamatiwa eneo la Feri jijini Dar es Salaam, akidai kuwa ameitwa  na baba yake.
Baada ya kumkamata na kuanza kurejea naye kijijini Mkokozi ambako amehifadhiwa na msamaria mwema, alisema alipata simu nyingi za watu kumpa pole kwa tukio hilo, hali iliyomshangaza kwani hakuelewa watu hao walipataje habari hizo.
Mama mzazi wa mtoto Happiness Lyoba , Salah Zefania.
Miongoni mwa simu hizo ni pamoja na ya Mwinjilisti wa kanisa lao la Kisabato Mbagala aliyemtaja kwa jina la Jacob Mayala ambaye alihitaji kumuombea mtoto wake. ‘’Ni kweli Mwinjilisti huyo alifika Mkokozi na kufanya maombi maalumu yaliyoambatana na kufunga kwa siku kadhaa. Hali ya mwanangu kwa sasa ninakubaliana nayo maana amegeuka kuwa  binadamu ambaye  nilimtarajia, Happiness  hakuwa hivi maana alizidisha vituko vya maajabu,” alisema.
Mtoto Happiness Lyoba akiwa na mama yake.
Mama huyo amewaomba Watanzania wamsaidie mwanaye kusoma kwani hivi sasa anajitambua tofauti na huko nyuma.“Mimi kipato changu ni kidogo na huku niliko ni mbali sana, hakuna shule karibu, kazi yangu ni kilimo cha mbogamboga na tena hapa ninapoishi nimehifadhiwa tu, ninaomba msaada ili mtoto wangu aende shule,” alisema mama huyo akidai kuwa Ustawi wa Jamii ulimshauri kumweka binti yake mbali na maeneo aliyokuwa akiishi.
“Nilishauriwa asirudi  Kitunda kwa muda huu maana huko ndiko alikoanza kupatwa na hali ambayo naamini ilikuwa ni mapepo,” alisema.
Mtoto na mama wakisali pamoja.
HAPPINES  LYOBA
Kwa upande wake, Happines alisema anahitaji kusoma na kwamba matukio aliyokuwa akiyafanya hakujua yalivyotokea.

Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya mtoto huyu ambaye akili yake imerejea kuwa ya kawaida kufuatia maombi ya kila siku, anaweza kuwasiliana na mama yake

ZITO KABWE AWASWEKA RUMANDE VIGOGO WA TPDC



01
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.
02Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, akifafanua jambo wakati akiwahoji Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, James Andilile wakati kamati hiyo, ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika jana, Ofisi za Bunge, Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe.
03Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda
04Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kwenda kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.

HIVI NDIVYO VIJANA WALIVYOVURUGA MDAHALO UBUNGO PLAZA



Jaji Joseph Warioba akitoa mada. 
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam.
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani. 
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.
 Vijana wakiwa na mabango. 
 Mabango yakiwa juu. 
 Vujo zinaanza. 
 Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu. 
 Baadhi ya viti vilivyovujwa. 
 Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu. 
 Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi. 
 Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'

Monday, November 3, 2014

ANGALIA TAARIFA KAMILI KUHUSU VURUGU ALIZOFANYIWA JAJI WARIOBA JANA JIJINI DAR ES SALAAM


 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, jana alifanyiwa vurugu kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa kongamano la kujadili mambo ya msingi ya kuangaliwa katika Katiba inayopendekezwa.
Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) na wazungumzaji wakuu walikuwa ni waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Miongoni mwao ni Joseph Butiku, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi na Humphrey Polepole.

Jaji Warioba alipoanza kuzungumza, ndipo kikundi cha vijana kinachodaiwa kuwa kiliandaliwa dhidi ya kiongozi huyo kilipoanzisha vurugu hizo.

Vijana hao waliingia mapema katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam, lakini baada ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza waliibuka na mabango kisha kusogelea jukwaa alikokuwa amekaa Jaji Warioba na wajumbe wenzake.

Mabango mengi yalikuwa yakifanana kwa maudhui, aina ya wino uliotumika na pia hati ilionekana kufanana kwa kiasi kikubwa.

Mabango sita kati ya hayo, ambayo yalishikiliwa na vijana tofauti yaliandikwa kwa kalamu ya wino mzito mwekundu (marker pen) na matatu yalikuwa na ujumbe uliosomeka; "Katiba inayopendekezwa tumeipokea, tumeielewa na tunaiunga mkono."

Mengine matatu ya maandishi ya rangi ya bluu yalisomeka: "Katiba inayopendekezwa tumeipokea, na tunaiunga mkono."

Mengine yalisomeka “Fedha za Magharibi haziwezi kuibomoa nchi yetu, na Wananchi ndiyo wana maamuzi ya mwisho, Tume mnafanya kazi ya nani?”

Hali hiyo ilivunja utulivu ndani ya ukumbi kutokana waliokuwa na mabango kuendelea kuyainua juu huku kundi lingine likiwafuata kuwanyang’anya na kuyachana.

Hali hiyo pia ilisababisha watu waliokuwa ndani ya ukumbi kurushiana viti na kuwalazimisha wengine kutoka nje kuhofia usalama wao.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Warioba na wenzake walitolewa katika ukumbi wa mikutano na kuingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya usalama wao.

POLISI WAFYATUA MABOMU
Takribani dakika 10 baada ya kuibuka kwa vurugu hizo, polisi walifika katika eneo hilo na kufyatua mabomu ya kutoa machozi yaliyosababisha mamia ya watu waliokuwa katika eneo hilo kukimbia, kuanguka ovyo na wengine kujeruhiwa.

NIPASHE lilishuhudia polisi wakiwa wamewashikilia vijana wawili kwa kuhusishwa na vurugu hizo.

MWANDISHI APIGWA
Baadhi ya watu waliopigwa ni pamoja na Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Paul Makonda na mwandishi wa BBC, Anold Kayanda, ambaye alijeruhiwa kichwani kutokana na vurugu za ukumbini baada ya kurushiwa kiti.

Awali, Jaji Warioba, alisema asilimia 81 ya ibara za Rasimu ya Tume yamo kwenye katiba inayopendekezwa, hata hivyo, maudhui yake yakitazamwa kwa makini mambo mengi ya msingi yametupwa. Aliyataja mambo manne ya msingi yenye kuleta mabadiliko ambayo yalipendekezwa na wananchi yaliyoondolewa kuwa ni tunu za maadili ambazo kwa mujibu wake, zilibadilishwa na kuwa urithi, madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka kutengenisha mihimili ya Serikali na Bunge na Muundo wa Muungano.
 
 
Alisema kuna baadhi ya mambo yaliyopo kwenye katiba inayopendekezwa yanatia shaka iwapo yatakuwa katika utekelezaji yakiwamo mgombea binafsi na asilimia 50 kwa 50 ya wabunge wanawake na wanaume.

Kuhusu kura ya maoni alisema ni lazima wananchi waandikishwe kwanza kwenye daftari la kupiga kura huku akiwataka kuwa makini kuyapigia kura mambo ya msingi.
Hata hivyo, mdahalo huo haukumalizika kutokana na hali hiyo na hatimaye kufungwa na Katibu Mtendaji wa MNF, Joseph Butiku.

Baadaye, Jaji Warioba alionekana akiondolewa eneo hilo kutoka chumba maalum alichokuwa amewekwa huku akiwa anasindikizwa na watu wa usalama akiwa mzima na kupanda kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo.
CHANZO: NIPASHE

Saturday, November 1, 2014

ASKARI POLISI WA KIKE MWANZA AMKATA VIDOLE VINNE MFANYAKAZI WAKE KWA PANGA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake. 
Tukio hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.
AKIONYESHA NAMNA ALIVYOJERUHIWA NA MAMA HUYO
Akizungumza na waandishi wa habari kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara.
“Nilipoona hajanilipa mshahara wangu kwa muda wa miezi sita huku kila ni kimwambia ananijia juu na kunitukana matusi basi nilimuomba ruhusa ya kwenda kijijini Oktoba 15 mwaka huu kumuona mama yangu mzazi aliyekuwa anaumwa ili kupata nafasi ya kurudi nyumbani” alisema.
Steven alieleza kuwa wakati akiwa kijijini askari huyo (Mwajili wake) alikuwa akimpigia simu kumtaka arudi Mwanza kuendelea na kazi na kudai kuwa atamlipa malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha Sh 300,000/= zilizokuwa kama deni, Steven alikubali ombi hilo kwa kuomba atumiwe nauli na pesa kidogo ya kumwachia mama yake, jambo ambalo askari huyo alikaa kimya bila majibu.
“Siku ya Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa 4:00 asubuhi alifika kijijini akiwa na askari watatu kwenye gari la Polisi (Difenda) wa Kituo cha Mugumu na kudai kuwa nipo chini ya ulinzi kisha kunifunga pingu, akidai kuwa nilimwibia Deki ya Video na kutoroka nyumbani kwake, walinipandisha kwenye Difenda kunipeleka kituoni “ alisema.
Kijana huyo alieleza kuwa baada ya kufikishwa kituoni Mugumu askari huyo na wenzake walianza kumuhoji huku wakimpa maneno ya vitisho, kijana huyo alipokataa kuwa hakuiba wala kutoroka, Sajenti Fatuma aliamuru kijana huyo kuvulishwa shati alilovaa na kisha akafungwa usoni na kuombwa anyooshe mkono mezani ili apewe 'Sapraizi'.
"Sekunde chache nilihisi kitu kikali kimenipitia kwenye vidole vyangu vinne vya mkono wa kulia na kufuatiwa na maumivu makali, niliusogeza mkono wangu mdomoni kuupoza kwa kuupuliza ndipo nilipo gundua kuwa nimekatwa kabisa vidole vyangu vinne vya mkono wangu wa kulia ikibakia dole gumba tu" kijana Steven alisimulia kwa uchungu.
“Niliangua kilio kutokana na maumizu na sijui vidole vyangu hadi sasa sijui vikowapi, askari wenzake baada ya kuona nimetokwa na damu nyingi walimshauri anipeleke hospitali ya Wilaya ya Mugumu ili nipatiwe matibabu kabla ya kuondoka kuja Mwanza,”alisisitiza.
Steven alisema baada ya kupatiwa matibabu, tulienda kupanda basi ili kuja Mwanza kwa madai kuwa amenifungulia kesi ya wizi wa Deki ya Video na tuliopfika alinipeleka kituo cha Polisi Kati Nyamagana na kuniweka Mahabusu akinituhumu wizi, lakini nilipochukuliwa maelezo nilikana tuhuma za wizi na kueleza ukweli wangu ili kupata msaada.
Huku taarifa zingine kutoka ndani ya jeshi zilizopatikana zilidai kuwa askari huyo alikusudia kufanya ukatili huo kutokana na udanganyifu ambao alifanya kwa uongozi wake akiomba kupatiwa silaha (SMG) kwa ajili ya kuitumia kwenye kazi za nje lakini lengo ikiwa ni kwenda na silaha hiyo kwa ajili ya kumkamata na kumtishia kijana huyo, jambo ambalo uongozi ulimgomea.
JESHI LA POLISI LINASEMAJE
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC), Valentino Mlowola, jana ofisini kwake amethibitisha kuwepo kwa taarifa za tukio hilo na kueleza kuwa tayari Jeshi hilo limechukuwa hatua madhubuti hatua ya awali ikiwa ni kumshikilia askari huyo kwa kufanya ukatili huo kwa kuvunja sheria na kujichukulia sheria mkononi kumjeruhi kijana huyo.
Mlowola alisema pamoja na kijana huyo awali kufunguliwa jarada la kutuhumiwa kufanya kosa la wizi (Jinai) na kudaiwa kutorokea kijijini kwao, bado askari huyo alitakiwa kufuata mfumo wa kiutawala na kisheria uliopo kushughulikia suala hilo badala ya kuamua kujichukulia maamuzi ya kumwadhibu mtuhumiwa kabla ya uthibitisho wa mashitaka yaliyokuwa yamefungulia.
“Nilipopokea taarifa hizi kwa mashangao na masikitiko makubwa na zimenisitua sana, si kitendo cha kiungwana hata kidogo kwa mtu ambaye anatakiwa kufuata taratibu za mfumo wa utawala na sheria katika utekelezaji wa kushughulikia kero na matatizo ya jamii, alitakiwa kutumia busara kwani tayari aliishamfungulia jarada la kumtuhumu kumwibia ikizingatiwa naye ni mzazi wa watoto watano ni lazima anaujua uchungu,”alisema. 
Kamanda Mlowola alieleza kufatia ukatili huo kufanywa na askari wake ameunda timu ya kikosi cha askari kwenda hadi kijijini Magange wilayani Serengeti mkoani Mara ili kufanya uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni pamoja na kufanya mahojiano na familia, wananchi wa kijiji hicho kisha Hospitali ya Wilaya ya Serengeti alipopatiwa matibabu ya awali.
HIVI NDIVYO VIDOLE VILIVYOKATWA NA MAMA HUYO.
“Ili tupate ukweli wa jambo hili tumeunda timu hiyo, kwani kijana Steven tumemhoji ametueleza jinsi askari Fatuma alichomfanyia na kudai hakumwibia, lakini askri wetu pia amehojiwa awali amedai hakufanya kitendo hicho bali wananchi ndo walimfanyia ukatili huo hivyo ni mkanganyiko lakini ukweli utapatikana tu japo kuwa tukio hili halikufanyika Mwanza”alisisitiza.
Mlowola alisema kwamba tayari tunamshikiria askari huyu na kumfungulia jarada la uchunguzi kwa taratibu za kijeshi na ikibainika kutenda kosa hilo tutumfukuza kazi na kumfikisha katika vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua zaidi kulingana na kosa alilofanya, lakini pia kijana Steven naye anashikiriwa kwa tuhuma alizonazo za wizi kufatia jarada lililopo.
“Hatuwezi kuendelea kucheka na kufumbia macho kitendo hiki ni jambo ambalo linamgusa kila mtu hata mimi ni mzazi ukiachana na utumishi wangu wa umma, ntahakikisha jambo hili nalishughulikia kwa umakini na kutoa taarifa kwa umma ili pia kueleza wananchi kuwa tukio hili limefanywa na mtumishi kama mtu si Taasisi ya Jeshi la Polisi na ahidi kutenda haki kwenye hili,”alisisitiza. 
Wito wangu kwa wananchi ni kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuwaadhibu watuhumiwa mbalimbali kabla ya kuthibitika kwa makosa na tuhuma hizo, lakini wazingatie kufuata taratibu za kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili kushughulikia matatizo yao nawaomba waendelee kutoa ushirikiana na kufuata mfumo uliopo badala ya kujichukulia sheria mkononi.

ACHOMWA KISU BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MWALIMU

Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda. 
KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu. 
Habari zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu, akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia ikilala njaa.
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake, alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo. 
Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.
Bw. Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini. Habari zinadai kuwa, baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha huyo alimuwakia Raphael kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi kumwambia? Ugomvi mwingine ukazuka hapo. 
MASHUHUDA SASA
Nao mashuhuda ambao ni majirani wa mwalimu huyo, Juma Hamis na Joyce Joseph, walipozungumza na paparazi wetu walisema siku hiyo walisikia vurugu kutoka ndani kwa mwalimu ambapo walikwenda kushuhudia.
Walisema walimkuta mwanaume huyo akipigana na ticha ambaye alikuwa akiendelea kulalamika kufichwa suala la mwanaume wake kuwa na mke. 
WACHOMANA VISU
“Unaambiwa mzozo huo ulipamba moto, maana yule mke aliyeondoka alidai amemfumania mumewe, mwalimu naye akadai alikuwa hajui.
“Katika purukushani hiyo huku wakipigana wao kwa wao ndipo wakachomana visu. Yaani mwanaume alijeruhiwa vibaya mno.
Mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’ aliyechomana visu na Bw.Raphael Bernard. “Mwanaume alichomwa kisu utumbo ukatoka nje na kama siyo polisi kufika na kukimbizwa hospitalini, sasa hivi tungekuwa tunaimba ‘Parapanda Italia….Parapanda…’ kwani hali ilikuwa mbaya sana,” alisema Joyce kwa masikitiko. 
HOSPITALINI
Baada ya kuzungumza na majirani na mashuhuda wa tukio hilo, mwanahabari wetu alitia gia kwenye pikipiki yake aina ya ‘boksa’ hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mwandishi wetu alizungumza na Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk. Francis Semwene ambaye alikiri kuwapokea majeruhi hao.
“Mwanaume alikuwa amepasuka tumboni hivyo tunaendelea kumpa matibabu, yupo wodi namba moja na mwanamke ambaye naye amechomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake, naye tunaendelea kumpatia matibabu,” alisema Dk. Semwene. 
HUYU HAPA MWANAUME
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu huku polisi wakiwa wamempiga pingu kitandani, Raphael alisimulia kwa maumivu makali:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul. “Mke wangu ni Veronica lbrahim ambaye tumeishi kwa miaka 6 na kujaliwa kupata mtoto mmoja.
“Mwezi wa tano mwaka huu, tuligombana, niliondoka nyumbani, kwa heshima ya mtoto wangu, sikuchukua kitu chochote zaidi ya nguo.
“Mwezi huohuo nilifanikiwa kuingia kwenye uhusiano na Mwalimu Rosemary ambapo baada ya penzi kukolea aliniambia nihamie kwake ili tulifaidi penzi letu tamu yaani mahaba motomoto na niliishi pale miezi mitano.” 
FUMANIZI?
Alipotakiwa kuelezea chanzo cha tukio la fumanizi, jamaa alifunguka: “Hamna. Ticha aliniamsha asubuhi akaniambia nimsaidie kufanya usafi na kumuogesha mwanaye. 
MADAWA YA KIENYEJI
“Nilipomaliza kumuogesha nilitaka kutandika kitanda, nilipoinua godoro niliona madawa ya kienyeji.
“Nilipomuuliza mwenzangu akawa mkali kama pilipili ndipo ugomvi mkubwa ukaanzia hapo.
“Baada ya mzozo mkali, ndugu zake walinivamia, akiwemo shemeji yangu wa kiume, namfahamu kwa jina la baba Dickson. 
MAUMIVU
“Wakati najitetea, nilishika kisu ambapo katika hekaheka ya kunyang’anyana na Rosemary kilinichoma mimi na yeye.” 
TICHA ARUHUSIWA
Mwandishi wetu alifika wodi namba tatu aliyolazwa ticha huyo na kuelezwa kuwa aliruhusiwa baada ya kupata nafuu ya majeraha mengi ya visu aliyoyapata sehemu mbalimbali za mwili wake hasa kichwani.
Baada ya kumkosa ticha huyo wodini, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake, alipobanwa alisema:
”Tukio hili limetokana na ushirikina wa mke wa zamani, alinitishia kuwa nikishika mimba nitajifungulia mdomoni akiapa kunifanyia kitu mbaya.
“Yaani hata sijui nini kimetokea, Raphael, mume wangu kipenzi amenichoma kisu na yeye kujichoma tumboni.” 
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 27, mwaka huu, ambapo Raphael alikwenda kwa mpenzi wake, Rosemary ambako kulitokea ugomvi, wakaumizana kisa wivu wa kimapenzi, hivyo tunamshikilia mwanaume huyo huku uchunguzi ukiendelea,” alisema Kamanda Paul.