Monday, December 1, 2014

WANANCHI WAASWA KUPANDA MICHE YA MATUNDA ILIYOBORESHWA





Kutokana na elimu ya kilimo kutolewa katika Nyanja mbalimbali watanzania wameonekana kuwa na mwamko wa kutumia mbegu na miche ya kisasa katika kilimo chao.

Hayo yamesemwa na msemaji wa BRIDEBABLE CONSULTANT LTD ya jijini Dar Mr Michael Lameck ambopo amesema wananchi wengi wamekuwa na muamko wa  kutumia mbegu bora katika kilimo, hivyo kuwaasa pia kutumia miche ya matunda iliyoboreshwa kiteknolojia zaidi.

msemaji huyo amesema kuwa upandaji wa miche ya matunda iliyo zalishwa kwa kutumia bioteknolojia ya uzalishaji kwa njia ya chupa na uzalishaji kwa kutumia vikonyo huleta tija katika kilimo cha matunda. kutokana na  watu kuwa na mwamko wa kula matunda pamoja na juisi za asili hivyo kumekuwa na uhitaji mkubwa wa matunda mijini hivyo amewaasa vijana kuchangangamkia tenda hii kwa kujikita katika kilimo

Ili kuepuka uagizaji wa matunda kutoka nje ya nchi kama ilivyo tunda la tufaa ambalo huletwa nchini kutoka nchi ya Afrika ya kusini amewataka vijana kujiajiri wenyewe katika kilimo kwa kulima matunda ambayo hayahitaji mkulima kuwa shambani wakati wote na hulimwa hata nyumbani kwa faida ya familia.

Bwana Michael akionyesha jinsi miche miwili ilivyounganishwa ili kupata mche mmoja 

Bridebable Consultant ni kampuni iliyoko jijini Dar inayouza miche bora ya matunda kwa wakulima nchini na nje ya nchi kulingana na mahitaji ya mkulima mwenyewe

Miche hii ambayo imeboreshwa na kituo cha utafiti na kilimo SUA ni miche ambayo hukua haraka na kuzaa matunda bora na kwa wingi. Miti hii ya matunda ni miti ambayo huchukua mda mfupi kuanza kuzaa matunda hivyo haimfanyi mkulima kusubiri mda mrefu kupata manufaa yake.

Bwana Michael alisema miche ya matunda ambayo inapendwa sana na watu wengi wa jiji la Dar ni pamoja embe aina ya Red Indian, Apple Mango, Alphonso, Cant, embe sindano na alizeti/dodo, pia kuna  Mapera, Minazi ya mda mfupi pamoja na machenza.

kilimo cha miti ya matunda yanaweza kupandwa nyumbani na kumnufaisha mtu kwa kula matunda na kutumia miti hiyo kama kivuli nyakati za jua kali, pia miti hupendezesha mazingira iwapo itapandwa katika utaratibu mzuri


 Baadhi ya miche inayouzwa na Bridebable

 Hata hivyo alisema kampuni yake inauza aina zote za miti japo kuwa kuna aina ya miti huuzwa kwa oda maalumu. hivyo yeyote mwenye mahitaji ya miti nyumbani au shambani kwake wasiliana nao kwa kuwapigia

+255 712545052, +255 784 647775 au waandikie  upambamichael@gmail.com


DIAMOND APETA TUZO ZA CHANNEL O AIBUKA NA TUZO 3


diamond  3diamond   19        Mwanamuzi wa kitanzania aitoa kimasomaso inchi yetu baada ya kufanya vizuri katika kinyang'anyiro cha tuzo za muziki Afrika. mwanamuziki Diamond amechukua tuzo 3 kati ya 4 na kuwaacha wenyemajina yao midomo wazi huku awaamini kama mkali wa kitanzania anaondoka na tuzo hizo.   
diamond   20
diamond  2Jumamosi Ya Nov  29 2014 Watanzania na wapenzi wa muziki wa bongo fleva walifuatilia kwa karibu sana tuzo za Video za Channel O zilizofanyika Johannesburg South Africa. Mtanzania mwenzetu Diamond Platnumz alikuwa akiwania tuzo nne kwenye vipengele tofauti.
Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo tatu kati ya 4 alizokuwa anawania. Tuzo alizoshinda ni Most Gifted EastAfrica, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer.
Hizi ni picha za Diamond akiwa na mama yake mzazi, manager wake Bab Tale na Said Fela na Zari kutoka Uganda.
      diamond   4diamond   6diamond   8diamond   9diamond   10diamond   11diamond   13diamond  1
Kiukweli, haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa Mwenyez Mungu na support kubwa mliyonipa iliwezesha Bongo Flavour yetu kuandika Historia mpya kwenye Ramani ya mziki wa Africa…Hii inaonyesha ni jinsi gani Umoja ni nguvu na pia jins gani mziki wetu ukisupportiwa na kupewa kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi… Shukran sana kwa @channeloafrica @channelotv kwa kuniona na kuthamini kipaji changu, My Family, Management, Media zote zilizokuwa zikinisupport, Watangazaji, Wasanii, Wadau na bila kuwasahau wapendwa wangu #TeamWasafi #TeamChibu #TeamPlatnumz #TeaMMondi toka instagram, Facebook, Whatsapp, Twitter na kadharika, wakiongozwa na kamanda langu @kifesi … Nawashkuruni sana sana

MFAHAMU SINGASINGA TAPELI WA ESCROW


POLISI ALIYEUA KIJANA MWEUSI AJIUZULU!


Daren Wilson Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi nchini Marekani amejiuzulu. Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano. 
Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na kuuawa. Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28 aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.
Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo.''

Thursday, November 27, 2014

SHEIKH PONDA ASHINDA RUFAA YAKE

  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushinda rufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande)
 Wafuasi wa Sheikh Ponda.
 Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
  Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya Sheikh Ponda kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mfuasi wa  Sheikha Ponda akitoka Mahakamani.

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam wakati wa kesi ya Ponda.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakiwa wamelizunguka basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakilifukuza basi la Magereza alilokuwa amepanda Sheikh Ponda wakati akielekea mahabusu ya gereza la Keko.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa wakitoka Mahakamani.
 Gari la Polisi.
 Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti.

KAULI YA JULIASI MTATIRO BAADA YA VIONGOZI WA DINI KUCHUKUA PESA WA IPTL


NCHI IMEOZA HADI ALTARENI.... 
Tunapokuwa na nchi iliyooza, viongozi wa dini wako mstari wa mbele kuchukua milungula na hela za rushwa zilizojaa damu na mateso ya kodi za wananchi.Ni aibu mno, sielewi hawa maaskofu wangu wanasimama kwenye altare kufanya nini...ni kufuru na aibu kwa mimi Mkatoliki na wakatoliki wote duniani.
Wakati Bunge linafukuza wezi, ni muhimu na Kanisa Katoliki lifukuze hawa maaskofu walafi na kuwapeleka mahakamani. Kisha kanisa lijivue ushenzi huu, lirejeshe pesa hizi kwa niaba ya watumishi hawa walafi wa fedha na mafisadi.
Shame on you beloved bishops, my bishops...

VIGOGO WALIOTAFUNA MABILION YA ESCROW HAWA HAPA


 Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.

Andrew Chenge (Mb)

Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. 

 Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. 

 Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 

 Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 

 Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

 Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. 

 kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

 Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9 

 Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 

 Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.

Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. 

Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4
 Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow

 Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 

Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. 

 Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
NA HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA KAMATI
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWAJIBISHWE KWA KUUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA - MAPENDEKEZO YA KAMATI YA ZITTO

Filikunjombe: Kamati inashauri kuzitangaza benki za Stanbic na Mkombozi kama asasi za utakatishaji fedha


Filikunjombe: Kamati inasha
uri bodi ya Tanesco ivunjwe na TAKUKURU iwafungulie mashtaka ya rushwa.

Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Naibu waziri wa nishati na madini alisema uongo bungeni naye achukuliwe hatua.

Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo amekuwa akisema uongo mara nyingi.

Filikunjombe: Kamati pia imethibitisha kuwa Waziri wa nishati na madini ndiye alikuwa dalali mkuu wa kuunganisha hawa watu

Filikunjombe: Kutokana na sababu hizo hapo juu, kamati inapendekeza kuwa Waziri wa Nishati na madini avuliwe madaraka yake.

Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali utengeuliwe mara moja na aadhibishwe maana ametumia vibaya madaraka

Filikunjombe: Kamati pasipo mashaka imejidhihirisha kuwa Waziri mkuu alikuwa akijua jambo hili ila hakuchukua tahadhari.

Filikunjombe: alisema Mwalimu Nyerere kuwa kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu.

Kwa vyovyote vile, Waziri mkuu anapaswa kuwajibishwa kwa namna yoyote ile ili kurudisha heshima ya serikali maana ameudanganya umma wa Watanzania kwa kusema uongo na kuitete kampuni hewa ya PAP isiyokuwepo

Filikunjombe: Kamati yetu inaamini kuwa Bunge hili litaitumia vizuri taarifa yetu hii

Mh. Spika anna Makinda amehairisha shughuli za Bunge na kusema kuwa kesho asubuhi serikali itatoa kauli zake.

Baada ya serikali kutoa kauli zake hapo kesho asubuhi, Wabunge wengine watapata nafasi ya kuchangia.