Kutokana na elimu ya kilimo kutolewa katika Nyanja
mbalimbali watanzania wameonekana kuwa na mwamko wa kutumia mbegu na miche ya
kisasa katika kilimo chao.
Hayo yamesemwa na msemaji wa BRIDEBABLE CONSULTANT LTD ya
jijini Dar Mr Michael Lameck ambopo amesema wananchi wengi wamekuwa na muamko
wa kutumia mbegu bora katika kilimo, hivyo kuwaasa pia kutumia miche ya matunda iliyoboreshwa kiteknolojia zaidi.
msemaji huyo amesema kuwa upandaji wa miche ya matunda iliyo zalishwa kwa kutumia bioteknolojia ya uzalishaji kwa njia ya chupa na uzalishaji kwa kutumia vikonyo huleta tija katika kilimo cha matunda. kutokana na watu kuwa na mwamko wa kula matunda pamoja na juisi za asili hivyo kumekuwa na uhitaji mkubwa wa matunda mijini hivyo amewaasa vijana kuchangangamkia tenda hii kwa kujikita katika kilimo
Ili kuepuka uagizaji wa matunda kutoka nje ya nchi kama ilivyo tunda la tufaa ambalo huletwa nchini kutoka nchi ya Afrika ya kusini amewataka vijana kujiajiri wenyewe katika kilimo kwa kulima matunda ambayo hayahitaji mkulima kuwa shambani wakati wote na hulimwa hata nyumbani kwa faida ya familia.
Bwana Michael akionyesha jinsi miche miwili ilivyounganishwa ili kupata mche mmoja
Bridebable Consultant ni kampuni iliyoko jijini Dar inayouza miche bora ya
matunda kwa wakulima nchini na nje ya nchi kulingana na mahitaji ya mkulima
mwenyewe
Miche hii ambayo imeboreshwa na kituo cha utafiti na kilimo
SUA ni miche ambayo hukua haraka na kuzaa matunda bora na kwa wingi. Miti hii ya matunda ni
miti ambayo huchukua mda mfupi kuanza kuzaa matunda hivyo haimfanyi mkulima
kusubiri mda mrefu kupata manufaa yake.
Bwana Michael alisema miche ya matunda ambayo inapendwa sana
na watu wengi wa jiji la Dar ni pamoja embe aina ya Red Indian, Apple Mango, Alphonso, Cant, embe
sindano na alizeti/dodo,
pia kuna Mapera, Minazi ya mda
mfupi pamoja na machenza.
kilimo cha miti ya matunda yanaweza kupandwa nyumbani na kumnufaisha mtu kwa kula matunda na kutumia miti hiyo kama kivuli nyakati za jua kali, pia miti hupendezesha mazingira iwapo itapandwa katika utaratibu mzuri
Baadhi ya miche inayouzwa na Bridebable
Hata hivyo alisema kampuni yake inauza aina zote za miti japo kuwa kuna aina ya miti huuzwa kwa oda maalumu. hivyo yeyote mwenye mahitaji ya miti nyumbani au shambani kwake wasiliana nao kwa kuwapigia
No comments:
Post a Comment