Saturday, December 13, 2014

WAZAZI WA MWOZESHA BINTI YAO KWA NGUVU BAADA YA KUFUMWA AKIFANYA TENDO LA NDOA

Na Baraka lusajo,
   Binti mmoja mkazi wa  kijiji   Lugombo  kata  ya Kandete  Wilayani Rungwe Mkoani  Mbeya  Getina   Karinga  miaka  {24} ameingia katika wakati  mgumu  baada ya kuozeshwa  ndoa  ya mkeka  kwa  nguvu na  wazazi  wake  baada  ya  kufuniwa   na  mwanaume  wakati  akifanya  tendo la ndoa  chumbani  kwao.

  Tukio  hilo  la kushangaza  limetokea  baada  ya  kijana  huyo kwenda  kwa  wazazi  wa  binti  huyo   kwa lengo la  maongezi ya  kawaida   na  kujikuta akiambulia   kipigo  kikali kutoka kwa  mama  mtu baada  ya kufumwa  wakati  akifanya  tendo  hilo chumbani kwa  mama yake  na binti.
 Hata hivyo  kutokana na     hali  hiyo
mama  huyo aliweza  kuangua  kilio kikubwa  baada  ya   vijana hao kuto onyesha  ishara  ya kuacghana  na kitendo  hicho mara baada  ya kufumwa  wakati  wakifanya kitendo hicho  na kwamba  kabla ya  tukio  mama  mtu alifika  na  kuwa muru  kuondoka mara  moja  lakini kutokana  na    wapendanao  kunogewa   na  tendo hilo  walijikuta wakiendelea  kufanya  bila kujari uwepo  wa  mama yao na kupelekea  mama mtu kupatwa  na hasira  na kuchukua   mfagio  na kuwachapa .
 Kwa mujibu  wa  mama  huyo ambaye  hakutaka  kutajwa  jina lake   hadharani  alisema  mnamo  majila ya  sambili za usiku akiwa ametokea  kwenye  shughuri  zake za kawaida  aliweza   kukuta milango ya   nyumba   yake ikiwa wazi  na kuamua  kuingia  lakini baada ya  kumwita  binti  yake  alijibiwa arudi  aliko tokea   , lakini aliamua  kupiga  moyo  konde  na  kuamua  kosogea  zaidi  na kumkuta mtoto wake akifanya  kitendo hicho  na kuamua   kuita watu.
         “Nimeona  aondoke  nyumbani kwangu kwani amekuwa akinidharau  bila kujari  kwamba    mimi ni mama yake  na  hadi kufikia hatua  ya  kufanya  mapenzi  na mwanaume mwingine  nyumbani kwangu kitu ambacho ni dharau  kubwa ,  na mpaka sasa nimemwozesha  na kutoa  baraka zangu  zote  kwani nimechoka   vitendo anavyo nifanyia   kwani  mda  wote amekuwa akifika nyumbani akiwa amelewa  pombe  kupita  kiasi  na  mda mwingine  nimekuwa  nikimfuma  kwa  macho  yangu akiwa  anavuta  bangi na sigara.” Alisema mama mtu.
 Kwa  upande  wa    binti huyo alisema   yuko  tayari  kuolewa  na kijana  huyo   na kwamba   anawashukuru wazazi  wake  kwa  hatua  walio fikia kutokana  na kwamba amekaa miaka  mingi sana akiwa  nyumbani  kwao bila  kuolewa na kwamba sasa  atakuwa  huru  katika  kumpatia mme  huduma yake  muhimu, na  huku mwanaume akifurahia  ndoa  hiyo  kutoikana  na kwamba  muda wote  walikuwa  wakimbania  mwanamke   huyo wakidai anatabia  mbaya  kitu amacho kwake    si kweli..
 Mtendaji wa  kata  hiyo  huruma mwakyusa  mbali  na kukili kutokea  kwa  tukio  hilo  alisema wameshindwa  kuendelea na  kesi hiyo kutokana na kwamba  wazazi  wa  binti  huyo  wamekataa  kumpokea binti  yao  kwa madai  ya kuwachafua na kuamua   kumuodhesha  bila  mahali.

Thursday, December 11, 2014

KIJANA AMPA MIMBA MAMAYE WAHAMA MJI KUOGOPA MANENO

Kijana mmoja nchini zimbabwe katika kijiji cha pote amekimbia kijiji hicho baada ya kujikuta katika matatizo makubwa kufuatia kumtia mimba mama yake mzazi kwa mara ya pili.Ikumbukwe hapo nyuma kijana huyo aliwahi kutenda kitendo hicho ambapo wana kijiji walimsihi kutorudia tena kitendo hicho baada ya kijana huyo kumshawishi mama yake na kuitoa mimba hiyo.Simon Matsvara na mama yake Ethel Vhangare aliamua kuondoka baada ya waumini wa kanisa lao kugundua kuwa mimba hiyo ni batili.Miaka minne iliyopita, wawili hao waliripotiwa na kutozwa faini na viongozi wa kijiji kwa kosa la kutoa mimba.Chifu wa kijiji, Chinamhora alisema kuwa jamii ilikasirishwa na kitendo hicho na kwamba yeye aliamua kuwatuma wafanyakazi wake kuwatafuta wawili hao waliokuwa wameamua kuishi kama mume na mke.“Tunaenda kuwatafuta mpaka tuwapate na wakisha patikana ni lazima wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wanoa jihusisha na vitendo kama hivyo ambavyo havikubaliki katika jamii”Alisema chifu huyo.Imeripotiwa kuwa wawili hao walianza mahusiano yao tangu mwaka 2008 wakati Matsvara alipopewa jukumu la kumuuguza baba yake mzazi mzee Agripah,ambae baadae alikufa.Mama huyo alipata mimba mara ya kwanza, wawili hao walitozwa faini na kuambiwa uhusiano wao ukomee hapo wasije wakarudia tena.Habari ya mimba ya pili ziligundulika baada ya mama huyo kuanza kuwakwepa wahumini wa kanisa lake walipokuwa wakimtembelea nyumbani kwake.Baada ya uchunguzi ndipo walipogundua kuwa mama huyo ni mjamzito wa miezi 5 na ujauzito huo kapewa na mwanae.

Wednesday, December 3, 2014

BILIONEA NIGERIA AMZIKA MAMA YAKE NDANI YA HUMMER


Bilionea Nigeria aliyeiwekea marembo gari la Humeer yenye thamani ya dola 1,000 na kumzika nayo mama yake katika mji wa Enugu nchini Nigeria.
Gari la Hummer lililobeba mwili wa marehemu likiingizwa kaburini

Bilionea akimzika mama yake ndani ya gari la Hummer nchini Nigeria.

ZITTO AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE

MBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni. Mchumba huyoUtambulishio huo wa mchumba wa Zitto ulifanywa na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) wakati wa sherehe ya Harusi yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annex.hali ilikuwa hivi; baada ya Kafulila kutambulisha ndugu zake pamoja na wazazi wake ndipo alianza kutambulisha wageni wengine na kuanza na mchumba mtarajiwa wa Zitto Kabwe aliyemtaja kwa jina la Anna.“Huyu wa kwanza anaitwa Anna anafanya kazi Ubalozi wa Ireland ni mchumba mtarajiwa wa Zitto Zuberi Kabwe, anayefuata kutoka kushoto kwa Anna wote mnamfahamu ndiyo Zitto mwenyewe na anayemfuata ni Mwalimu wangu wa chuo kikuu Kitila Mkumbo na mwisho ni mbunge mwenzangu David Silinde hao ndo walio nisindikiza

Tuesday, December 2, 2014

BASI LAACHA NJIA NA KUTUMBUKIA KORONGONI MLIMA KITONGA

 Basi liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia. Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia. Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa  mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote  wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo.

Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.

RAIS KIKWETE AMWAPISHA CAG MPYA, PROF MUSA JUMA ASSAD IKULU JIJINI DAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitia sahihi yake kwenye nyaraka baada ya kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad nyaraka baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaa  Novemba 02, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuangalia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad akiweka sahihi yake kwenye nyaraka baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na CAG Mstaafu Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 02, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Spika Anne makinda na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 02, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na wafanyakazi wa ofisi ya CAG  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na familia ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.
 (PICHA NA IKULU)

MZEE MSUYA AWASIHI WAKULIMU KUTOOGOPA NENO BIOTEKNOLOJIA


Kutokana na kuwepo kwa maneno yanayowatishia na kuwakatisha tamaa wakulima kuwa mbegu za kisasa ni mbegu za kibioteknolojia na hazifai kwa matumizi ya binadamuu, mzee Msuya amewasihi wakulima kuwabeza watu hao na maneno yao na kutoliogopa neno bioteknolojia kwani hilo ni neno la kisayansi ambalo halibadirishi uasili wa mmea wa aina yoyote ile.
Aliyasema hayo baada ya kuwepo kwa baadhi ya watu kumfuata na kumuuliza siri ya mafanikio yake katika kilimo na anapowaambia kuhusu mbegu za kibioteknolojia huingiwa na mshangao na kuogopa neno hilo
Mzee msuya ni miongoni mwa wazee maarufu katika wilaya ya Vunjo kutokana na juhudi zake katika kilimo na ndio wazee wenye pesa mjini hapo.
mzee huyo ambaye alisema siri ya mafanikio yake aliipata baada ya kukubali kung'oa miche yake ya zamani ya kahawa na kupanda miche mipya aliyoinunua katika taasisi ya utafiti wa kahawa ya TaCRI baada ya kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa kilimo wa taasisi hiyo.
"mtafiti alinishauri nitoe miche ya kahawa yote iliyokuwapo shambani na kunpambia nikanunue miche mipya ya TaCRI kwani ni miche isiyokuwa na maambukizi ya magonjwa yanayosumbua zao la kahawa sikuamini lakini baadaye nikakubali na nikafanya kama nilivyaambiwa na sasa naitwa mchawi hapa kijijini kutokana na mazao ninayoyapata.


wanawake wakimsaidia mzee msuta kuchambua mahindi nyumbani kwake 



Mzee huyo ambaye sasa amekuwa mwalimu wa wakulima wenzake alisema kuwa Tanzania kama nchi nyingine haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia kutokana na utandawazi na maendeleo ambayo yapo duniani kote, kwa kuwa bioteknolojia ni nyenzo muhimu katika kuboresha kilimo, uzalishaji viwandani, kwenye afya, hifadhi ya mazingira pia kukuza uchumi nchini
mzee huyo ambaye alisema alikuwa anapata kilo 250 mpaka 1500 kwa msimu lakini tangu miche mipya ianze kuzaa matunda napata kilo 5000 mpaka 8000 kwa msimu na kwa ukubwa ule ule wa shamba. kitu ambacho akiwaeleza wenzie wanashangaa sana na kutoamini anachowaeleza.

Akifafanua kuhusu neno bioteknolojia alisema kwa madaha  kuwa ni "taaluma ya kutumia michakato ya kibaolojia katika  viumbe hai ili kupata mahitaji na huduma kwa maendeleo na maisha bora ya binadamu" 


 
Msuya ambaye alisema hata sahau jinsi majirani zake walipomcheka na mumuita mpumbavu pale alipoamua kung'oa na kupanda miche mipya. Hata hivyo hakukatishwa tamaa na maneno yake bali alizingatia sana mafundisho aliyoyapata na kuyatendea kazi mpaka alipo fanikiwa na kubadirika kuwa mwalimu wa wengine
"Hivi sasa mimi nafuatwa na wakulima ili niwafundishe mbinu ninazotumia, lakini wengi wanashangaa ninapowaambia kuhusu mbegu mpya na utunzaji wa shamba vizuri wanaofuata ninayowaambia wanaona matunda yake.


 shamba la kahawa la mzee msuya likiwa limechanganywa na zao la migomba

Mzee huyo alisema kuwa anajivunia sana elimu aliyoipata kutoka kwa watafiti kwani wamemfanya kutoka kwenye kilimo cha kutafuta chakula pekee na kuwa mkulima mfanyabiashara kwani mazao anayoyapata kwa sasa yanakidhi mahitaji yake ya chakula na kupata kiasi kikubwa kwa ajili ya kuyauza kwenye makampuni makubwa hapa nchini.
"TaCRI imeniondolea umaskini kwani walinifundisha elimu ya kutumia mbegu bora kwa kila zao ninalotaka kulima pamoja na matumizi ya samadi ya wanyama nilionao nyumbani hivyo kwamgu mimi kila kitu ni faida kwani mashamba yanategemea mifigo kwa mbolea wakati mifugo inategemea kilimo kwa chakula". 

Hata hivyo aliwasii watafiti wote nchini kuwasaidia wakulima ili wapate elimu kuhusu matumizi ya mbegu bora ili kumkomboa mkulima kwani wakulima wengi wanadanganya na propaganda zinazoletwa na wafanyabiashara wengine wa bidhaa zao wakidai kuwa matumizi ya mbegu hizo si salama wakati ni uvumi usio wa kweli kabisa.

TaCRI ni taasisi ya utafiti wa kahawa nchini Tanzania na inafanya kazi  kwa msaada wa nchi za ulaya, hufanya uzalishaji kwa njia ya Tissue Culture ( uzalishaji kwa njia ya chupa) na kuzalisha kwa kutumia vikonya (kupachika mche mmoja juu ya mche mwingine).


Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) iliyopo mkoani Kilimanjaro ilianza kazi rasmi 2001 na imepata mafanikio makubwa katika utafiti wa mbegu mpya chotara za arabika pamoja na ile ya Robusta Aina hizi za miche bora chotara za kahawa zimekuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya kahawa kwa kuwa zina tija ya hali ya juu zaidi ya aina za zamani pia zina muonjo wa hali ya juu kama aina za zamani na hata zaidi, na zina ukinzani na magojwa hatari ya chulebuni (CBD), kutu ya majani (CLR) na mnyauko fuzari (CWD), (CBD) kutegemea aina ya kahawa

Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) iliyopo mkoani Kilimanjaro ilianza kazi rasmi 2001 na imepata mafanikio makubwa katika utafiti wa mbegu mpya chotara za arabika pamoja na ile ya Robusta Aina hizi za miche bora chotara za kahawa zimekuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya kahawa kwa kuwa zina tija ya hali ya juu zaidi ya aina za zamani pia zina muonjo wa hali ya juu kama aina za zamani na hata zaidi, na zina ukinzani na magojwa hatari ya chulebuni (CBD), kutu ya majani (CLR) na mnyauko fuzari (CWD), (CBD) kutegemea aina ya kahawa Kutokana na sifa hizo, aina hizo mpya zinampunguzia mkulima gharama za uzalishaji, kati ya asilimia 50 na hata ukilinganisha na miche mingi ya zamani ambayo mingi imezeeka na kushambuliwa na magojwa kitu ambacho kinasababisa hasara kwa mkulima Pia TaCRI imetoa teknolojia za kuongeza tija na ubora wa kahawa aina mbili zinazotekelezeka za kuzalisha miche mipya bora ya aina hizi chotara ikiwa nipamoja na kutumia vikonyo, kupachika aina mpya juu ya mibuni ya zamani na kuzalisha kitaalamu miche kwa kutumia chupa ikifahamika kwa lugha ya kingereza ’Tissue culture au Somatic embryogenisis.’

Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) iliyopo mkoani Kilimanjaro ilianza kazi rasmi 2001 na imepata mafanikio makubwa katika utafiti wa mbegu mpya chotara za arabika pamoja na ile ya Robusta Aina hizi za miche bora chotara za kahawa zimekuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya kahawa kwa kuwa zina tija ya hali ya juu zaidi ya aina za zamani pia zina muonjo wa hali ya juu kama aina za zamani na hata zaidi, na zina ukinzani na magojwa hatari ya chulebuni (CBD), kutu ya majani (CLR) na mnyauko fuzari (CWD), (CBD) kutegemea aina ya kahawa Kutokana na sifa hizo, aina hizo mpya zinampunguzia mkulima gharama za uzalishaji, kati ya asilimia 50 na hata ukilinganisha na miche mingi ya zamani ambayo mingi imezeeka na kushambuliwa na magojwa kitu ambacho kinasababisa hasara kwa mkulima Pia TaCRI imetoa teknolojia za kuongeza tija na ubora wa kahawa aina mbili zinazotekelezeka za kuzalisha miche mipya bora ya aina hizi chotara ikiwa nipamoja na kutumia vikonyo, kupachika aina mpya juu ya mibuni ya zamani na kuzalisha kitaalamu miche kwa kutumia chupa ikifahamika kwa lugha ya kingereza ’Tissue culture au Somatic embryogenisis.’

Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) iliyopo mkoani Kilimanjaro ilianza kazi rasmi 2001 na imepata mafanikio makubwa katika utafiti wa mbegu mpya chotara za arabika pamoja na ile ya Robusta Aina hizi za miche bora chotara za kahawa zimekuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya kahawa kwa kuwa zina tija ya hali ya juu zaidi ya aina za zamani pia zina muonjo wa hali ya juu kama aina za zamani na hata zaidi, na zina ukinzani na magojwa hatari ya chulebuni (CBD), kutu ya majani (CLR) na mnyauko fuzari (CWD), (CBD) kutegemea aina ya kahawa Kutokana na sifa hizo, aina hizo mpya zinampunguzia mkulima gharama za uzalishaji, kati ya asilimia 50 na hata ukilinganisha na miche mingi ya zamani ambayo mingi imezeeka na kushambuliwa na magojwa kitu ambacho kinasababisa hasara kwa mkulima

Make Money at : http://bit.ly/copy_win