Japokuwa awamu ya tano ya uongozi wa
Raisi John Pombe Magufuli umefanya mabadiriko mengi yanayokonga nyoyo za
watanzania wengi bado kilimo kimebakia kuwa uti wa mgongo wa uchumiTanzania.
Hata hivyo mpaka sasa hajafanikiwa
kuufuta usemi huu ambao umekuwa ukibakia kama ulivyo na ndivyo ilivyo kuwa
kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, kikichangia takribani nusu ya
Pato zima la Taifa na robo tatu ya bidhaa zote zinazouzwa nje ya nchi. Pamoja
na kuzalisha chakula, kilimo vilevile kinatoa ajira kwa asilimia 80 ya
Watanzania.
Sehemu kubwa ya kilimo Tanzania ni cha wakulima wadogo-wadogo
(small-holder farmers) ambao wengi wao hawatumii njia za kisasa na wengine
mpaka leo hawajawahi hata kuzijua.
Takwimu za Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika, zinaonyesha kuwa Tanzania, wakulima wake hulima hekta milioni 5.1
nchi nzima kila mwaka, na kati ya hizo asimilia 85 ni kwa ajili ya mazao ya
chakula ikiwa ni pamoja na mazao ya mbogamboga na matunda, ambayo huzalishwa
kwa wingi karibu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Kilimo cha mboga na matunda kimekuwa
maarufu nchini kwa sasa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji katika soko la
ndani na nje, kuongezeka elimu kwa wakulima na watumiaji, upatikanaji kwa urahisi
wa pembejeo na uwezeshaji unaofanywa na serikali pamoja na taasisi binafsi.
Mikoa ya Kanda ya Kaskazini Arusha, Manyara,
na Kilimanjaro kilimo hiki kimeanza kuwavuta kwa kasi makundi ya vijana na
wanawake ambao sasa ndio wanaonekana kukivalia njuga kilimo hicho hasa kufuatia uelimishaji na
uhamasishaji unaofanywa na Taasisi zinazojishughulisha na utafiti na uuzaji wa
pembejeo zinazohusu kilimo hicho.
Rijk zwaani imekuwa mstari mbele katika
kuwapatia wakulima mafunzo ya kilimo cha mboga na matunda, pia kuwaaunga mkono
wakulima wote wanapata mafunzo kwao kwa kuhakikisha wanapata mazao bora na masoko
ya uhakika ya ndani na nje ya nchi, pembejeo na madawa muhimu na ushauri wa
kitalaamu unaotolewa na maafisa ugani wa shirika hilo.
Mbali na shirika hilo pia AVRDC pia
wamekuwa mstari wambele kuendeleza utafiti wa mbegu mbali mbalii za mbogamboga
na kutoa elimu kwa makundi tofauti tofauti ya wakulima kuhusu kilimo bora cha
mbogamboga na hata wakati mwingine kutoa mbegu bure kwa makundi hayo ili
kuyawezesha makundi hayo.
Licha ya hivyo SEVIA pia ndio limekuwa
shilika la kimbilio la wakulima baada ya wao kujidhatiti katika kutoa mafunzo
yajinsi ya kulima kwa kutumia kilimo cha kisasa ambacho imeonekana ndio njia
pekee ya mkulima kujikwamua kutoka katika kilimo kisicho na tija na kuwa kilimo
cha tija.
Ally Materu (30) ambaye ni mkazi wa Moshi
Mkoani Kilimanjaro, amekuwa akijishughulisha na kazi ya kupanda mlima na
watalii bila kujua kuwa anaweza akafanya shughuli nyingine mpaka alipojiunga na
kikundi cha “kijana jikwamue” ambao hivi karibuni walitembelea Rikj zwaani na
kupata mafunzo ya kilimo ndipo alipotambua kuwa kuna fursa ambayo anaweza
akaifanya na ikampatia kipato kikubwa kuliko hiyo aifanyayo.
“Leo nimetambua ya kuwa nilikuwa
najicheleweshea maendeleo yangu mwenyewe kwa ajiri ya kutegemeo upandaji mlima
wakati kumbe kilimo kinaweza kikanitoa kirahisi nikidhamilia” alisema Ally.
Nae
mwalimu Ole Lengai (29) mkazi wa kijiji cha Olkokola Mkoani Arusha ambaye
alibainisha kuwa kilimo hicho kimekuwa “dawa” ya tatizo sugu la ajira nchini
ambalo linawakabili vijana wengi. “Nilianza kilimo hiki miaka miwili iliyopita,
baada ya kujifunza kwa kutembelea shamba darasa la AVRDC, kwa kweli kiuchumi
hali yangu imebadilika sana kutokana na mazao ninayozalisha kama nyanya, na
aina nyingine tofauti za mboga kuuzika kwa haraka na kuwepo kwa soko la uhakika
hasa baada ya wanunuzi kujua ubora wa mazao yangu alisema Ole.
“Vijana wengi wanalalamika kuwa hawana
mitaji ya kuanzisha shughuli za kilimo, malalamiko yao hayana mantiki sana
kwasababu vijana wengi wanamiliki vitu vya bei ya juu kama simu, laptop, nguo
za thamani na wakati mwingine wanapatikana sehemu za starehe wakitumia pesa za
kutosha kuanzisha mradi wa kilimo”Alisema Ally.
Kwa mujibu wa Ole, kilimo cha mboga ni
rahisi sana kwa sababu hakihitaji eneo kubwa la ardhi, na pia mazao ya aina
hiyo hukomaa ndani ya mda mfupi na mkulima anakuwa ameshapata fedha za mauzo na
kurudisha gharama zake.
Akijitolea mfano yeye mwenyewe alisema
alihamasika sana baada ya kutembelea shamba darasa na kuona vijana wanaolima
pembezoni mwa shirika la AVDRC na kupata shuhuda kutoka kwao akaamua kukata
shauri ya kuondokana na maisha ya kupoteza mda kwa kukaa vijiweni.
“Nilianza kwa kulima matuta mawili ya
mnafu na baada ya kuuza na kupata faida ndipo nilipoamua kujidhatiti katika
kilimo, hivi sasa nina shamba la hekari moja ambalo nililinunua mwenyewe baada
ya kupata faida ya mboga mboga na sasa nalima nyanya, mnavu pamoja na kabichi
ambapo kilimo hiki kimenifanya mda mwingi kuwa shambani mpaka naambiwa naringa
baada ya kuacha kuhudhuria vijiweni nilikokuwa nikienda kupoteza mda wa
mafanikio haya niliyonayo sasa” aliongeza Ole
Hata hivyo wakulima wote wanalalamikia
sana changamoto ya mbegu feki madukani pamoja na miundo mbinu ya barabara
zisizopitika kabisa kwa gari hivyo wengi kushindwa kufikisha mazao yao katika
masoko kwa muda na hata wakati mwingine imekuwa kikwazo cha kuwafanya wateja
wao kushindwa kuwafikia kiurahisi pale wanapohitaji bidhaa kutoka kwao, hivyo
wanalazimika kila wakati kuwapelekea sokoni
“Kama unavyoona hali ya barabara ni mbaya
sana, hasa wakati wa masika barabara hazipitiki kabisa na hii ni changamoto
kubwa sana kwa sisi wakulima, gharama zinaongezeka na matokeo yake faida pia
inapungua”alisema mmoja wakulima wa nyanya.
”Serikali imesahau maeneo ya wakulima
ambayo yanazalisha mazao ya biashara na chakula, tumelalamikia hali hii kwa muda
mrefu na hata viongozi wetu yaani madiiwani na wabunge wanajua ila hakuna
hatua zilizochukuliwa”. Aliongeza mkulima huyo
Nae Abel kuley wa Rijk zwaan anabainisha kuwa mipango ya taasisi hiyo ni
kuwafikia wakulima wengi zaidi katika maeneo yote ambayo kilimo cha mboga na
matunda kinaweza kufanyika.
“Sasa tunaelekeza nguvu zetu katika maeneo
yote ambayo kilimo kinaweza kufanyika, malengo yetu ni kuwahusisha zaidi vijana
na wanawake ambao ndio waathirika wakubwa wa tatizo la ajira nchini na
tunadhani kwamba sekta hii inaweza kuwa mkombozi wa tatizo la ajira na
kupunguza umaskini,”alisema.
Nae Fekadu Fufa Dinssa kutoka, mzalishaji
wa mbegu (vegetable breeder) AVRDC alisema kwa kushirikiana na serikali
wanaweza kupunguza kabisa tatizo la ajira kama si kulimaliza kabisa ikiwa bei
za pembejeo zitapunguzwa ili kuwapa fursa wakulima wengi kupata nafasi ya
kujihusisha na kilimo bora
Kwa
mujibu wa taarifa ya Gavana wa Benki ya Tanzania, ya mwaka 2014 sekta ya kilimo
imeonekana kupigwa kikumbo na sekta za utalii, dhahabu, viwanda na usafirishaji
wa mizigo nje ya nchi. Kwa mujibu wa takwimu hizo sekta ya utalii iliingizia
Taifa dola za Marekani bilioni mbili, dhahabu dola bilioni 1.7, viwanda dola
bilioni 1.3 na kilimo kinachoingiza dola
milioni 830 kwa mwaka. Hata hivyo bado kilimo kimebakia kuwa uti wa mgongo wa
uchumi Tanzania.