Friday, August 29, 2014

KIJANA AFARIKI KWA KULA VIJIKO VIWILI VYA WALI





  Wakazi wa kijiji  cha mpunguiti  kata  ya  luteba wilayani  Rungwe mkoani mbeya  wamelazimika  kuitisha mkutano wa  kimila baada ya mwanachi  mewezao    Dulo mwangwego  miaka   {26} kufariki dunia  ghafla  baada   kula wali vijiko  viwili.
 Wakiiongea   kwa masikitiko  makubwa wanachi hao kupitia katika  mkutano wa  hadhara ulio anza  majila ya saa  kumi na moja  ya alfajili  ambapo waliseesema    wameamua  kuchukua hatua ya kuitisha mkutano wa huo baada  ya   kijana  huyo kufariki  dunia  katika mazingra ya  kutatanisha kwa  kula wali vijiko  viwili.

  Hata  hivyo taarifa za awari kutoka  kwa wananchi  hao zimeeleza kuwa   katika siku za  hivi karibuni   vijana wawili walienda   kufanya kazi   ya kumsaidia  kulima  mwanakijiji mwenzao  Jimu  mwakibwaga kama   kibarua  lakini   baada ya   ya  vijana hao kuonekana  kufanya  kazi viziri  bosi wao Jimu mwakibwaga  aliamua kuwapatia   kilo  nne za  mchele   ambao  waliondoka  nao hadi katika  makazi  yao, lakini   hata  hivyo kijana huyo baada ya kujaribu  kula  vijiko  viwili alijikuta   akianza  kunyong’onyea mwili wake kwa ghafla   kwa  kanza kutokwa na  damu katika sehemu  za puani  ikiwa ni  pamoja  na kutokwa  na damu katika  sehemu  ya haja  kubwa , ambapo   kutokana na hali   hiyo  kuzidi kuchukua nafasi yake aliamua  kuwaita  majilani zake ambao  walimkimbiza katika Hospitali  teule ya  Halmashauri ya Busokelo  itete kwa  matibabu zaidi.
 Hata   hivyo kipindi  hiki  kilifanikiwa  kuhojiana  na  baadhi  ya   ndugu  wa marehemu  juu ya  kisa  hicho  ambapo wamesema  chanzo  cha tukio  hilo   kimekuja  kufuatia  kula  wali ambao alipewa na   mwanakijiji  mwenzake baada ya kumualika kumsaidia  kufanya kazi ya kulima  shamba  ambapo  baada ya kufika  nyumbani  kwake , alipikiwa  chakula  hicho  vizuri  lakini  baada   ya  kujaribu  kula  vijiko  viwili alijikuta akinza kujigalagaza  huku na kule   kwa kutokwa na damu katika sehemu za puani  na  haja  kubwa na ndogo   hali ambayo ilipelekea   kumfikisha  hospitali  ambako aliweza kupoteza  uhai wa maisha  yake wakati  akiendelea na matibabu.
   Kwa upande wake  chifu  wa maeneo hayo  ASajile  Mwambage  alisema hatua  hiyo imekuja  baada ya  kuwepo kwa  maslalamiko kwa  wananchi wake juu ya kifo  cha ndugu yao na kutaka  kuitishwa kwa mkutano wa kimila wakitaka  kujua  hatima  ya kifo  cha  kijana   wao na  ukizingatia  kuwa  hilo  ni  tukio  la pili kujitokeza katika maeneo hayo ambapo  katika siku  za hivi karibuni   mwanakijiji mwenzao   Jueli mwanjwango alifariki  katika mazingra ya  kutanisha  baada ya  kudaiwa  kuchapwa na fimbo  na jilani   yake kutokana   ugonvi wa mifugo.

  Hata   hivyo mkutano huo ulianza  mnamo  majila ya  saa kumi na   moja  ya  alfajili  na kumalizika majila ya  saa mbili za alfaji  na huku  ukiwa na lengo la kutomeza   vifo vya ajabu katika maeneo  hayo.

No comments:

Post a Comment