Zaidi
ya wanawake 600 wanaotengeneza jumuia ya wakazi katika eneo la women
Noiva do Cordeiro kusini mwa Brazil ambao wengi wao wana umri kati ya
miaka 20 na 35 wanaomba kupelekewa wanaume kutokana na eneo hilo
wanaloishi kutokuwa na wanaume.
Mji
huo ambao idadi ya wakaaji wake wote ni wanawake umeomba angalau
mwanaume mmoja kwenda kuishi katika eneo hilo ingawa atatakiwa kuishi
kulingana na sheria za kike zinazotawala eneo hilo.
Ingawa
baadhi ya wanawake hao wameolewa na wanafamilia lakini waume zao
hufanya kazi nje ya eneo hilo na wanatakiwa kurudi mwisho wa juma tu
(Weekend)
Taratibu
wanawake wengi ambao walikuwa hawajaolewa pamoja na familia zao
walianza kujiunga na jamii hiyo na miongo kadhaa baadae wanaume
walifanya majaribio kadha ya kuingia katika eneo hilo hali amabayo
ilipelekea jamii hiyo ya wanawake kuanzisha sera ya hakuna mwanaume "'no
male' policy."
Mmoja wa wanawake hao aliyefahamika kwa jina la Nelma Fernandes mwenye maiaka 23, anakili kwamba ni vigumu kwa msichana anayejulikana katika hilo eneo na ni mrembo kuacha kuchumbiwa ikiwa mwanaume atamuona ila tatizo ni ukosefu wa wanaume hao.
Anasema
"mwanaume pekee ambao wasichana hutana nao ni wale ambao wameoa au wana
uhusiano wa kindugu,Wote ni binamu.Nimembusu mwanaume muda mrefu sana
uliopita."
Anaongeza kusema kuwa "Wote tunandoto ya kupenda na kuolewa lakni tunapenda kuishi hapa na hatutaki kwenda mjini kutafuta wanaume."
No comments:
Post a Comment