MKAZI wa kijiji cha Ndala, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Andondile
Mwasamlagila (50) amenusulika kufa baada ya kucharangwa na mapanga na
mtoto wake, Yuda Mwasamlagila kutokana na ulevi wa kupindukia.
Wakizungumza na blog hii, wanafamilia walisema kuwa tukio hilo
lilitokea Agosti 11 mwaka huu majira ya jioni ambapo mzee huyo akiwa
amejituliza katika makazi yake, akivamiwa na kushambuliwa na mapanga na
mtoto huyo.
Walidai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa mzazi huyo
wakati akishambuliwa na kwamba waliposogea karibu walikuta akiwa
hajitambui huku akiwa na majeraha kwenye shingo na sehemu za kichwa.
Kwa mujibu wa wanafamilia hao, walimkimbiza katika kitu cha afya cha
Mwakaleli kwa ajili ya matibabu na kwamba sasa anaendelea vizuri.
Kwamba, wakati majeruhi akipatiwa matibabu, wanakijiji waliamua
kwenda kumsaka mtoto wake aliyesababisha tukio hilo ambapo walimkamata
akiwa amejificha kwenye shimo huku akiwa amelewa.
Kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Iddy Suleiman alikiri kupokea majeruhi huyo, akisema bado anaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment