Tuesday, September 30, 2014

NABII ALITIKISA KANISA KWA KUFANYA MIUJIZA...MAELFU WAMIMINIKA KANISANI KWAKE


Na Mwandishi Wetu
Nabii wa Kanisa la Holly Ghost Fire lililopo Mbezi Juu – Kwa Temba ameendelea kuwa gumzo jijini Dar kwa miujizo anayoitenda kwa kuwaombea wagonjwa ambao wanapona Live bila King’amuzi.
Vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo mtandao huu vilishuhudia maajabu ya nabii huyo anaejulikana kwa jina Jeremiah Lukiko “ Mzee wa Fire” vilishuhudia muujiza miujiza mbalimbali ya kuwaponya watu wenye ukoma pamoja magonjwa sugu yote.
Kanisa hilo ambalo licha ya kuwa change lakini maelfu yaw a waumini wamekuwa wakimiminika kwa ajili ya kupata huduma bora ya maombi yaliyojaa upako wa ajabu toka kwa mtumishi huyo wa Mungu natayari watu wengi wameanza kuhama makanisa mengi na kukimbia kwake kwa ajili ya kuponywa magonjwa yao.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ibada kumaliza mwishoni mwa juma Mchungaji huyo alisema” Hii ni miujiza ya kutisha Mungu anatenda kazi yake hapa hatuna mzaha na suala la uponyaji hapa hata ukija mgonjwa umebebwa kwenye machera haraka tu moto unafanya kazi yake hivyo natoa uwito kwa watanzania sasa waache kuteseka Mungu amewaleta mkombozi hata kama wamehangauika namna gani na magonjwa lakini hapa kwangu ni mwisho waje na Mungu atawaponya kwa maombi yangu na kwa uharaka zaidi” Alisema Nabii Jarry









Mtumishi huyo alitoa uwito kwa wakazi wa Jiji la Dar na vitongoji vyake kuacha kuteseka na maradhi, au wasiogope nguvu za kichawi, au chuma ulete na wale wenye umaskini wa kurithi pamoja na laana ya kurithi wafike Kanisani kwake awashughulike kwake ni kazi ndogo hiyo maombi pekee yanaweza kubadilisha maisha ya mtu kwa dakika kadhaa.


Na ratiba zinaanza kila siku za Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, ni saa kumi jino na Jumapili ibada inaanza saa tatu asubuhi hasi saa saba mchana na kwa wale wenye mahitaji ya maombi wapige namba ya huduma 0713-976786




































No comments:

Post a Comment