MTU
mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata
Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi
baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao
ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.
Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa ni mwizi. Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.
Akiuguza majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda
kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao
walitutilia shaka wakaanza kutupekua.
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita
dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka
wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa
kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,
No comments:
Post a Comment