Thursday, October 2, 2014

MABOMU YA MACHOZI YAENDELEA KUCHUKUA NAFASI YAKE RUNGWE


Wananchi wa    kata    ya lwangwa   Halmashauri  ya  Busokelo wilayani  Rungwe mkoani Mbeya  wameandamana   kuanzia     leo  asubuhi   hadi  katika ofisi za Halmashauri  hiyo    wakishiniza  serikali  wilayani  humo   kuwatoa  watu  walio kamatwa   baada  ya kuhusiwa kuhusika  na kifo cha  Gabriel Mwandemwa  mwenye  umri wa mika  {40} aliye  uwawa na  wananchi   katika  siku za   hivi karibuni kutokana na imani za  kishirikina.
 Wakizungumza  na   yetu rungwe  blog   wakati  wa  mandamano hayo  wanachi  hao   walisema hatua  hiyo ilikuja  kufuatia   jeshi  la polisi wilayani  humo  kuwakamata   baadhi ya wananchi   kwa madai ya  kuhusika na kifo  cha kijana  huyo  aliyefariki dunia siku za hivi karibuni  kutokana  na    vitendo vya  ushirikina. 
 
 Walisema  mnamo majila ya   usiku  wa kuamkia  oktoba   moja  jeshi la polisi  liliwasili kinyemela katika  maeneo hayo  kwa  kuwakamata  baadhi ya  wananchi    bila kushirisha  uongozi wa  maeneo husika   kwa  kufikishwa  kituoni,  ambapo kutokana na hali  hiyo   iliweza kupelekea  wao kama  wanachi kuchukua  hatua  ya  kupinga   kitendo hicho   kwa  kuungana  kwa  pamoja   na kufanya maadamano ya amani  hadi katika  ofisi  ya mkurugezi  wa Halmashauri hiyo  wakitaka kutolewa  kwa ndugu  zao.
   Hata  hivyo jeshi la  polisi liliwasili  eneo  la  tukio   na kisha kunza  kusaidia kuzuia    gasia  hizo   ikiwa  ni pamoja  na kuwatia  hatiani wale  wote ambao walionekana kuanzisha vurugu hizo.
   Diwani wa kata  hiyo Robati Mwaibata alikili kuwapo kwa  adha hiyo  na kusema  mpaka sasa wameshindwa  kuongea  na wananchi wake  kutokana na  vurugu kuendelea kuchukua nafasi  yake.
Alisema    chanzo   cha  tukio hilo ni  baada  ya jeshi la polisi  kuwakamata  baadhi ya  vijana wa  eneo hilo  kwa  tuhuma  za  kuhusika  na  mauji  ya    Gabriel Mwandemwa aliye fariki dunia siku za  hivi karibuni kwa   kukatwa na  mapanga na kisha mwili wake  kuchomwa moto.
 Alisema mpaka sasa wanaendelea  kutuliza gasia  hizo kwa  ushirikiana na jeshi la  polisi  wilayani humo .
 Hata  hivyo     juhudi na malfa za kutafuta mkuu wa wilaya ya rungwe krspini meela ziligonga mwamba   mara  baada  ya    simu yake  kuita bila kupokelewa.
 Siku  za  hivi  karibuni    wananchi wa  kijiji  cha Ikama  Mbande  walimkamata  Gabliel   Mwaibata  walimkamata kwa  kumwachia  kipigo na kisha   kumchoma moto baada ya  kudaiwa  kujihusisha  na vitendo  vya  kishjirikina.

No comments:

Post a Comment