Ukweli ni
kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu
yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.
Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge …
Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu
Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa
dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za
kiusalama.
Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu
aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo
baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge
wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu
ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika
kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali
ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia
Bunge hilo.Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi
amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika
vurugu hizo
No comments:
Post a Comment