Tuesday, November 4, 2014

MTOTO WA MIAKA 10 ABAKWA NA MZAZI WAKE

NA Baraka lusajo.
Kamati ya  ulinzi  na usalama ya  kijiji cha mwela  kata ya kandete  wilayani rungwe mkoani mbeya inamtafuta   geofrey mwasumbi   miaka  {36}  baada ya kumbaka mtoto wake   mwenye  umri  wa  miaka  {10}.
 Wakizungumza na kituo hiki mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo la kushangaza limejitokeza  wakati mtoto  huyo akiwa amejituliza  katika makazi yao  na kijukuta akivamiwa  na baba mzazi kwa  kubakwa na kisha kuachiwa  maumivu  makali  katika sehemu zake  za siri.
  Kwa  upande wa mama  mzazi wa  mtoto  huyo  alisema  ,
    wakati  tukio  hili lina tokea  nilikuwa  shamba  lakini  baada  ya kulejea nilikuta  mtoto wangu akiwa anatokwa na  damu  na huku akishindwa  kutembea  ambapo  niliamua  kumkalisha  kitako   kwa kumhoji  na  badaye akaniambia  kuwa  alilazimishwa na baba yake kufanya  tendo  la ndoa  ambapo  niliamua  kutoa  taarifa  katika  uongozi wa kijiji   hicho na wao walitoa  taafa katika  uongozi wa    kata  na kisha  kumchukua  mtoto na kumpeleka katika kituo cha afya  cha mwakaleli kwa  matibabu zaidi.
Huruma mwakyusa afisa  mtendaji wa  kata  hiyo  mbali na kukili  kutokea  kwa  tukio hilo  alisema  mtuhumiwa alikimbia kwa kutomoea  kusiko julikana  mara  baada  ya  tukio  kufanyika  na kwamba juhudi za  kumtafuta  bado zinaendelea  jampo  mtoto  huyoamelazwa  katika kituo cha afya  cha  mwakaleli kwa matibabu.

    Diana  godwini  mratibu  wa  dawati la kijinsia   kupitia bonde la Mwakaleli   mbali na kukili kujitokeza kwa tukio hilo amesema   wametoa  taarifa  polisi  kwa lengo la kusaidia  kumsaka mtuhumiwa.
Aidha   gidwini alisema  vitendo vya  ubakaji katika maeneo  hayo  vimeendelea  kuchukua sera  mpya  kutokana  na uelewa   na  imani   za  kishirikina.
  Hata  hivyo judi na maalfa za  kumtafuta  mganga mkuu wa kituo  cha  afya  cha mwakaleli  Dr  edwini  mwakisisya  zimegonga mwamba  baaada  ya kukosekana  ofisini kwake.

No comments:

Post a Comment