Monday, September 29, 2014

“MSHINDO NYUMA SASA BASI” SARAH NDOSI



 WADAU WAISUBIRI KWA HAMU CD YAKE INAYOTARAJIWA KUTOKA MWEZI DECEMBER MWAKA HUU
 
Wapenzi wa muziki wa nyimbo za kikristo haswa wale wapendao kusikiliza na kuangalia waimbaji wanaoimba live yaani uimbaji bila ya mshindo nyuma wikiendi hii walipata burudani ya kutosha kutoka kwa mwanadada Sarah Ndosi, aliyefanya live recording katika ukumbi wa kanisa la VCCT mbezi jijini Dar.

Sarah aliyeonekana kuwa ni mzoefu wa uimbaji huo alizikonga nyoyo za mashabiki wake waliofika kushuhudia tukio zima alipo imba nyimbo sita (6) mfurulizo na kuwafanya watu kusimama na kushangilia huku wengine wakishikwa na mshangao wa aina ya muziki ambao mwanadada huyo aliimba.

“Kiukweli dada huyu anastahili tuzo tena ya heshima maana nyimbo anazoimba si za hapa, anaimba nyimbo za mbele (akimaanisha nyimbo zenye hadhi ya kimataifa) na atasaidia nyimbo za kitanzania kujulikana mbele (akimaanisha nje ya tanzania)yaani wanamuziki wangekuwa  wanaimba viwango hivi wanamuziki wakibongo (wanamuziki wakitanzania) wangekuwa mbali sana” alisikika shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Prezzor Fredy Chavala, The king

Hata hivyo watu wengi walipigwa na mshangao pale ambapo mwanadada huyo aliiimba Accapela ya aina yake ambayo kwa hakika iliwafanya watu kuinua mikono yao kuonyesha kwamba wamemkubali na kufurahia burudani waliyokuwa wakiipata ukumbini hapo.
“Aisee Sarah anaimba, hata sikutegemea kama angeimba hivi, mi nilikuja kuhakikisha kama kilichosemwa kuwa ni live ni kweli na kama kweli itakuwaje kwani ni wachache sana wanaweza kufanya hivi na kwa ubora unaotakiwa lakini Sarah ameweza” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mama Junior

Mwanadada Sarah ambaye alionyesha kipaji chake kwa kuanza kuimba kwa kurudisha mikogo ya enzi zile za kuimba kwa kupiga mabiti akiwaongoza waimbaji waliokuwa wakimsaidia katika uitikiaji kilinakshi tamasha hilo.

 
Sanjali na hilo Sarah alitoa zawadi kwa wanafunzi walioibuka kidedea katika shindano la Student Talent Vestival lililoshirikisha wanafunzi wa shule za secondary za jijini Dar es salaam ambaposhule 15 zilishiriki katika mashindano hayo na  mwanadada Ester  alishinda kwa upande wa wadada na Samwel Wilfred mwanafunzi wa Tambaza alishinda kwa upande wa wanaume wakati kikundi kutoka Jangwani kilishinda katika mchuano wa makundi bora.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa ameamua kufanya mashindano hayo ili kuibua vipaji vilivyojificha mashuleni na kupata waimbaji wapya ambao watakuja na radha mpya katika muziki wa Injili ili kuleta changamoto katika tasnia ya muziki wa injili.

“watoto hawa wapo vizuri sana yaani wanajua kuimba kiukweli, wakipata waalimu wazuri wakuwaongoza katika uimbaji wao wanaweza wakaondoa majina ya baadhi wa waimbaji ambao tayari wanafahamika” alisema Sarah
 
Hata hivyo Sarah amesema kuwa mashindano hayo ya kutafuta vipaji mashuleni ni endelevu ambapo amesema kuwa yatakuwa yakifanyika kila mwaka ikiwa mwaka huundio ilikuwa mwanzo wake. Pia amewataka wanafunzi mashuleni kuweka juhudi katika masoyo yao ili kutowakatisha tama waalimu na wazazi katika kuwasapoti katika vipaji vyao. Hakuacha kuwasihi wazazi na waalimu kuwapa nguvu watoto ikiwa wanavipaji kwani hata yeye uimbaji wake aliuanzia akiwa shuleni na ndio imemfanya akafika hapo alipo katika uimbaji.

Sarah Ndosi amesema CD zake zitakuwa tayari sokoni ifikapo mwezi December mwisoni , hivyo amewaomba watu wote kumuunga mkono katika kazi yake hiyo ambapo amesema CD hizo zitauzwa kwa  Tsh 10000 kila moja.
 

No comments:

Post a Comment