Wednesday, November 5, 2014
Tuesday, November 4, 2014
MTOTO WA MIAKA 10 ABAKWA NA MZAZI WAKE
NA Baraka lusajo.
Kamati
ya ulinzi na usalama ya
kijiji cha mwela kata ya kandete
wilayani rungwe mkoani mbeya inamtafuta
geofrey mwasumbi miaka {36}
baada ya kumbaka mtoto wake
mwenye umri wa
miaka {10}.
Wakizungumza na
kituo hiki mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo la kushangaza limejitokeza
wakati mtoto huyo akiwa amejituliza katika makazi yao na kijukuta akivamiwa na baba mzazi kwa kubakwa na kisha kuachiwa maumivu
makali katika sehemu zake za siri.
Kwa upande wa mama mzazi wa
mtoto huyo alisema
,
“ wakati
tukio hili lina tokea nilikuwa
shamba lakini baada
ya kulejea nilikuta mtoto wangu
akiwa anatokwa na damu na huku akishindwa kutembea
ambapo niliamua kumkalisha kitako kwa kumhoji
na badaye akaniambia kuwa alilazimishwa
na baba yake kufanya tendo la ndoa
ambapo niliamua kutoa
taarifa katika uongozi wa kijiji hicho na wao walitoa taafa katika
uongozi wa kata na kisha
kumchukua mtoto na kumpeleka
katika kituo cha afya cha mwakaleli
kwa matibabu zaidi.
Huruma mwakyusa afisa mtendaji wa
kata hiyo mbali na kukili kutokea
kwa tukio hilo alisema
mtuhumiwa alikimbia kwa kutomoea
kusiko julikana mara baada
ya tukio kufanyika
na kwamba juhudi za kumtafuta bado zinaendelea jampo
mtoto huyoamelazwa katika kituo cha afya cha
mwakaleli kwa matibabu.
Diana godwini
mratibu wa dawati la kijinsia kupitia bonde la Mwakaleli mbali na kukili kujitokeza kwa tukio hilo
amesema wametoa taarifa
polisi kwa lengo la kusaidia kumsaka mtuhumiwa.
Aidha gidwini alisema vitendo vya
ubakaji katika maeneo hayo vimeendelea
kuchukua sera mpya kutokana
na uelewa na imani
za kishirikina.
Hata hivyo judi na maalfa za kumtafuta
mganga mkuu wa kituo cha afya
cha mwakaleli Dr edwini
mwakisisya zimegonga mwamba baaada
ya kukosekana ofisini kwake.
RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA LEO
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akiongea na wazee wa mji wa Dodoma leo Novemba 4, 2014
waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani wakati wa Mazungumzo kati ya RaisJakaya Mrisho Kikwete na wazee wa mji wa Dodoma leo Novemba 4, 2014 waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo
‘MTOTO WA NDEGE’ AOKOKA
MTOTO Happiness Lyoba (10)
ambaye aliripotiwa kuwa mwingi wa vituko vya maajabu, ikiwamo kuonekana
akishuka katika ndege huko Zanzibar, ameripotiwa kuokoka katika Kijiji
cha Mkokozi, wilayani Mkuranga, Pwani.
Akizungumza na gazeti hili, mama wa mtoto huyo, Salah Zefania alisema
mwanaye huyo alitoroka tena Septemba 16, mwaka huu na kukamatiwa eneo
la Feri jijini Dar es Salaam, akidai kuwa ameitwa na baba yake.
Baada ya kumkamata na kuanza kurejea naye
kijijini Mkokozi ambako amehifadhiwa na msamaria mwema, alisema alipata
simu nyingi za watu kumpa pole kwa tukio hilo, hali iliyomshangaza kwani
hakuelewa watu hao walipataje habari hizo.
Miongoni mwa simu hizo ni pamoja na ya
Mwinjilisti wa kanisa lao la Kisabato Mbagala aliyemtaja kwa jina la
Jacob Mayala ambaye alihitaji kumuombea mtoto wake. ‘’Ni kweli
Mwinjilisti huyo alifika Mkokozi na kufanya maombi maalumu
yaliyoambatana na kufunga kwa siku kadhaa. Hali ya mwanangu kwa sasa
ninakubaliana nayo maana amegeuka kuwa binadamu ambaye nilimtarajia,
Happiness hakuwa hivi maana alizidisha vituko vya maajabu,” alisema.
Mama huyo amewaomba Watanzania wamsaidie mwanaye kusoma kwani hivi
sasa anajitambua tofauti na huko nyuma.“Mimi kipato changu ni kidogo na
huku niliko ni mbali sana, hakuna shule karibu, kazi yangu ni kilimo cha
mbogamboga na tena hapa ninapoishi nimehifadhiwa tu, ninaomba msaada
ili mtoto wangu aende shule,” alisema mama huyo akidai kuwa Ustawi wa
Jamii ulimshauri kumweka binti yake mbali na maeneo aliyokuwa akiishi.
“Nilishauriwa asirudi Kitunda kwa muda huu
maana huko ndiko alikoanza kupatwa na hali ambayo naamini ilikuwa ni
mapepo,” alisema.
HAPPINES LYOBAKwa upande wake, Happines alisema anahitaji kusoma na kwamba matukio aliyokuwa akiyafanya hakujua yalivyotokea.
Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya mtoto huyu ambaye akili yake imerejea kuwa ya kawaida kufuatia maombi ya kila siku, anaweza kuwasiliana na mama yake
ZITO KABWE AWASWEKA RUMANDE VIGOGO WA TPDC
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na
Polisi kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya
kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu,
wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.
HIVI NDIVYO VIJANA WALIVYOVURUGA MDAHALO UBUNGO PLAZA
Jaji Joseph Warioba akitoa mada.
Mtoa
mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph
Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi
wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam.
Baadhi
ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na
mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea
tunaiunga mkono’.
Mlinzi
wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate
madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na
kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani.
Jaji
Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake
katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba
inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole
akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa
vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph
Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara
baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa.
Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.
Vijana wakiwa na mabango. Mabango yakiwa juu.
Vujo zinaanza.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu.
Baadhi ya viti vilivyovujwa.
Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.
Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi.
Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.
Monday, November 3, 2014
ANGALIA TAARIFA KAMILI KUHUSU VURUGU ALIZOFANYIWA JAJI WARIOBA JANA JIJINI DAR ES SALAAM

Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph
Warioba, jana alifanyiwa vurugu kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa
kongamano la kujadili mambo ya msingi ya kuangaliwa katika Katiba
inayopendekezwa.
Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) na wazungumzaji wakuu walikuwa ni waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Miongoni mwao ni Joseph Butiku, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Palamagamba Kabudi na Humphrey Polepole.
Jaji Warioba alipoanza kuzungumza, ndipo kikundi cha vijana kinachodaiwa kuwa kiliandaliwa dhidi ya kiongozi huyo kilipoanzisha vurugu hizo.
Vijana hao waliingia mapema katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam, lakini baada ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza waliibuka na mabango kisha kusogelea jukwaa alikokuwa amekaa Jaji Warioba na wajumbe wenzake.
Mabango mengi yalikuwa yakifanana kwa maudhui, aina ya wino uliotumika na pia hati ilionekana kufanana kwa kiasi kikubwa.
Mabango sita kati ya hayo, ambayo yalishikiliwa na vijana tofauti yaliandikwa kwa kalamu ya wino mzito mwekundu (marker pen) na matatu yalikuwa na ujumbe uliosomeka; "Katiba inayopendekezwa tumeipokea, tumeielewa na tunaiunga mkono."
Mengine matatu ya maandishi ya rangi ya bluu yalisomeka: "Katiba inayopendekezwa tumeipokea, na tunaiunga mkono."
Mengine yalisomeka “Fedha za Magharibi haziwezi kuibomoa nchi yetu, na Wananchi ndiyo wana maamuzi ya mwisho, Tume mnafanya kazi ya nani?”
Hali hiyo ilivunja utulivu ndani ya ukumbi kutokana waliokuwa na mabango kuendelea kuyainua juu huku kundi lingine likiwafuata kuwanyang’anya na kuyachana.
Hali hiyo pia ilisababisha watu waliokuwa ndani ya ukumbi kurushiana viti na kuwalazimisha wengine kutoka nje kuhofia usalama wao.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Warioba na wenzake walitolewa katika ukumbi wa mikutano na kuingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya usalama wao.
POLISI WAFYATUA MABOMU
Takribani dakika 10 baada ya kuibuka kwa vurugu hizo, polisi walifika katika eneo hilo na kufyatua mabomu ya kutoa machozi yaliyosababisha mamia ya watu waliokuwa katika eneo hilo kukimbia, kuanguka ovyo na wengine kujeruhiwa.
NIPASHE lilishuhudia polisi wakiwa wamewashikilia vijana wawili kwa kuhusishwa na vurugu hizo.
MWANDISHI APIGWA
Baadhi ya watu waliopigwa ni pamoja na Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Paul Makonda na mwandishi wa BBC, Anold Kayanda, ambaye alijeruhiwa kichwani kutokana na vurugu za ukumbini baada ya kurushiwa kiti.
Awali, Jaji Warioba, alisema asilimia 81 ya ibara za Rasimu ya Tume yamo kwenye katiba inayopendekezwa, hata hivyo, maudhui yake yakitazamwa kwa makini mambo mengi ya msingi yametupwa. Aliyataja mambo manne ya msingi yenye kuleta mabadiliko ambayo yalipendekezwa na wananchi yaliyoondolewa kuwa ni tunu za maadili ambazo kwa mujibu wake, zilibadilishwa na kuwa urithi, madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka kutengenisha mihimili ya Serikali na Bunge na Muundo wa Muungano.

Alisema kuna baadhi ya mambo yaliyopo kwenye katiba inayopendekezwa yanatia shaka iwapo yatakuwa katika utekelezaji yakiwamo mgombea binafsi na asilimia 50 kwa 50 ya wabunge wanawake na wanaume.
Kuhusu kura ya maoni alisema ni lazima wananchi waandikishwe kwanza kwenye daftari la kupiga kura huku akiwataka kuwa makini kuyapigia kura mambo ya msingi.
Hata hivyo, mdahalo huo haukumalizika kutokana na hali hiyo na hatimaye kufungwa na Katibu Mtendaji wa MNF, Joseph Butiku.
Baadaye, Jaji Warioba alionekana akiondolewa eneo hilo kutoka chumba maalum alichokuwa amewekwa huku akiwa anasindikizwa na watu wa usalama akiwa mzima na kupanda kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo.
CHANZO:
NIPASHE
Subscribe to:
Posts (Atom)