Monday, August 4, 2014
PASTOR MIAMBA AJIUNGA NA CHAMA CHA WANANDOA
Pastor Emmanuel Myamba muigizaji maarufu Tanzania amefunga ndoa na mke "Praxceda" visiwani Zanzibar na kuweka historia tena kwa muigizaji aliyefanya harusi iliyokwenda sawa
na hadhi yake.Kwa
mujibu wa ripota aliyekua kwenye eneo la tukio.....ameijuza AMESEMA harusi hiyo itakua miongoni mwa harusi zitakazo weka
historia Visiwani Zanzibara kutokana na zawadi waliyopewa Pastor Myamba
na mkewe ikiwemo gari jipya pamoja na pesa taslimu milioni 250
MWANAMKE AIBUA MSHANGAO BAADA YA KUJIFUNGUA WATOTO KWA STAILI YA KIPEKEE
MKAZI wa Kijiji cha Lupili wilayani
Misungwi Mkoa wa Mwanza, Tecla Kazimili (24), amejifungua watoto wanne,
watatu wa kike na mmoja wa kiume kwa njia ya kawaida katika hospitali
mbili tofauti na siku mbili tofauti.
Katika hospitali ya kwanza, ambayo ni zahanati ya Kijiji cha Lupili Agosti mosi mwaka huu, Tecla alionekana ana ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja ambapo wakati wa kujifungua, alizaliwa wa kiume akiwa na kilo 1.6, lakini kwa bahati mbaya alikufa.
Hata hivyo, wakunga walishuhudia mzazi huyo akiendelea kuwa na dalili ya kujifungua mtoto mwingine, lakini akawa amegoma kupita katika njia.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Marko Mwita, alisema baada ya kutokea kwa hali hiyo, alipigiwa simu kuombwa msaada.
“Baada ya kupokea taarifa hiyo majira ya usiku, nilituma gari la wagonjwa kukimbilia kwenye zahanati hiyo iliyopo umbali wa kilometa 60 na kumleta mama huyo katika Hospitali ya Wilaya kwa huduma zaidi,” alisema.
Alisema alipofikishwa hospitalini hapo, Tecla aliendelea kujifungua mpaka kesho yake hatimaye idadi ya watoto ikafikia wanne.
“Hili ni tukio la kwanza katika hospitali hii ya Wilaya, mtu kujifungua watoto wanne, ni matukio yanayotokea mara chache, lakini tunamshukuru Mungu mzazi anaendelea vizuri huku watoto wake watatu, wote wa kike kila mmoja akiwa na uzito wa kilo mbili,” alisema.
Dk Mwita alisema watoto hao wanahitaji uangalizi na msaada wa hali ya juu, kwani ni rahisi kupata maambukizi. Alitoa mwito kwa jamii kumsaidia mama huyo, kwani watoto hao wanahitaji msaada wa hali na mali kwa kuwa maziwa ya mama pekee hayatawatosheleza.
Akizungumzia historia yake ya uzazi, Tecla alisema watoto hao ni uzazi wake wa nne na katika ule uliopita, watoto wote aliowazaa walifariki dunia katika umri tofauti, lakini wa utoto.
“Kitendo cha watoto kufa baada ya kufikisha umri fulani, kilimfanya mume wangu anifukuze, nikalazimika kurejea nyumbani kwetu ambapo nilipewa ujauzito na kijana mwingine,” alisema.
Alisema wakati anahudhuria kliniki, alielezwa kwamba alikuwa na zaidi ya mtoto mmoja baada ya kutoa taarifa kuwa anaona tabia ya ujauzito huo ni tofauti na uzazi wake uliopita.
“Namshukuru Mungu kwa kunipatia watoto hawa na naiomba Serikali inisaidie kuwatunza ili wakue vizuri kwani peke yangu siwezi,” alisema. Kwa mujibu wa Tecla, aliumwa uchungu kwa siku tatu na alimaliza kujifungua Agosti
Katika hospitali ya kwanza, ambayo ni zahanati ya Kijiji cha Lupili Agosti mosi mwaka huu, Tecla alionekana ana ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja ambapo wakati wa kujifungua, alizaliwa wa kiume akiwa na kilo 1.6, lakini kwa bahati mbaya alikufa.
Hata hivyo, wakunga walishuhudia mzazi huyo akiendelea kuwa na dalili ya kujifungua mtoto mwingine, lakini akawa amegoma kupita katika njia.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Marko Mwita, alisema baada ya kutokea kwa hali hiyo, alipigiwa simu kuombwa msaada.
“Baada ya kupokea taarifa hiyo majira ya usiku, nilituma gari la wagonjwa kukimbilia kwenye zahanati hiyo iliyopo umbali wa kilometa 60 na kumleta mama huyo katika Hospitali ya Wilaya kwa huduma zaidi,” alisema.
Alisema alipofikishwa hospitalini hapo, Tecla aliendelea kujifungua mpaka kesho yake hatimaye idadi ya watoto ikafikia wanne.
“Hili ni tukio la kwanza katika hospitali hii ya Wilaya, mtu kujifungua watoto wanne, ni matukio yanayotokea mara chache, lakini tunamshukuru Mungu mzazi anaendelea vizuri huku watoto wake watatu, wote wa kike kila mmoja akiwa na uzito wa kilo mbili,” alisema.
Dk Mwita alisema watoto hao wanahitaji uangalizi na msaada wa hali ya juu, kwani ni rahisi kupata maambukizi. Alitoa mwito kwa jamii kumsaidia mama huyo, kwani watoto hao wanahitaji msaada wa hali na mali kwa kuwa maziwa ya mama pekee hayatawatosheleza.
Akizungumzia historia yake ya uzazi, Tecla alisema watoto hao ni uzazi wake wa nne na katika ule uliopita, watoto wote aliowazaa walifariki dunia katika umri tofauti, lakini wa utoto.
“Kitendo cha watoto kufa baada ya kufikisha umri fulani, kilimfanya mume wangu anifukuze, nikalazimika kurejea nyumbani kwetu ambapo nilipewa ujauzito na kijana mwingine,” alisema.
Alisema wakati anahudhuria kliniki, alielezwa kwamba alikuwa na zaidi ya mtoto mmoja baada ya kutoa taarifa kuwa anaona tabia ya ujauzito huo ni tofauti na uzazi wake uliopita.
“Namshukuru Mungu kwa kunipatia watoto hawa na naiomba Serikali inisaidie kuwatunza ili wakue vizuri kwani peke yangu siwezi,” alisema. Kwa mujibu wa Tecla, aliumwa uchungu kwa siku tatu na alimaliza kujifungua Agosti
WAKULIMA WAASWA KUFUATA MBINU BORA ZA KILIMO
Hayo yamesemwa na bi Rose Mongi ambaye ni mtafiti na mtaalamu wa ngano na maharage katika kituo cha utafiti na kilimo Uyole mkoani Mbeya ARI. Amesema wakulima wengi hawajapata mazao kama walivyokuwa wakitarajia kutokana na wao wenyewe kutokuzingatia kanuni na njia bora za kilimo ambazo wanatakiwa kuzifuata ili kupata mafanikio makubwa katika kilimo. Japo kuwa kulikuwa na mvua za kutosha sehemu nyingi za nyanda za juu kusini laikini wakulima wengi wamepata mavuno machache kutokana na mfumo wanaoutumia wakulima wenyewe. Pia amesema kuwa wakulima wengi siku hizi wamekuwa wakaidi wa kufuata kanuni hizo kutokana na kuwa na propaganda nyingi katika sekta ya kilimo, akidai kuwa hiyo ni changamoto kati ya changamoto nyingi nambazo zinaikabili sekta ya kilimo Tanzania.
Bwana Anthon Elanga msaidizi wa Bi Rose katika utafiti
Rose Mongi mtafiti wa mbegu za ngano na maharage ARI Uyole Mbeya
Bi Rose amesema kuwa wao kama wataalamu wapo kwa ajili ya wakulima ili wawatumie vile watakavyo, "sisi kama wataalamu tunafurahi sana pale wakulima wanapotuita ili tuwaelekeze njia bora za kilimo kwa ajili ya manufaa yao wenyewe kwani sie tupo kwa aajili yao na tumeajiriwa na serikali ili tuwatumikie wao". Pia ametoa wito kwa wakulima kufika kituoni hapo ili waweze kujifunza mengi kuhusu kilimo kwani wakifika mahali hapo waweza kujifunza hata kimatendo na mwisho wa siku kupata manufaa katika kilimo. "Tunataka kuwa na Tanzania yenye wakulima wanaojua nini wanafanya katika kazi zao, kwani kilimo chenye manufaaa bado hakijafanikiwa Tanzania, tunatamani sana tena sana"
Hata hivyo bi Rose alisema japokuwa kuna changamoto ya kuwa na mbegu feki madukani kitu ambacho kinasababisha wakulima kutokuwa na imani na mbegu za madukani, lakini amewahakikishia wakulima kuwa wanauhakika na mbegu wanazozalisha kituoni hapo.
hivyo amewaasa wakulima kuwa waangalifi wanapokwenda madukani kwa kuzitambua nembo halisi katika pakiti za mbegu wanazonunua.
Shamba la ngano
Kituo hiki ambacho kipo mkoani mbeya kimekuwa kikifanya utafiti wa mazao mbalimbali ili kupata mbegu bora kwa ajili ya wakulima. Na pia wamekuwa wakifanya utafiti wa udongo pamoja na magonjwa kwa mimea ili kumuondoa mkulima kutoka kwenye kilimo cha kupata chakula tuu bali wanataka mkulima apate hata mazao ya ziada ili kupata faida zaidi kwa kuyauza mazao hayo.
Bi Rose akichunguza aina ya ugonjwa kwa kutumia darubini
Bi Benadetha Rugumisa yeye ni biotechnology kituoni hapo
Akieleza kuhusu changamoto wanazozipata wakulima Bi Rose amesema kuwa wakulima wamekuwa wakiweka mambo ya imani mbaya hata katika kilimo kitu ambacho amekikemea vikali na badala yake amewasihi wakulima kutofuata maneno ya watu bali wafuate kanuni ambazo wataalamu wa kilimo wamekuwa wakiwafundisha. Ametoa mfano wa wakulima kutoamini juu ya mbegu zinazouzwa madukani kwa kusema kuwa si mbegu nzuri kwa afya za binadamu eti kwasababu tu zimeboreshwa, na badala yake Bi Rose amesema kuwa wao ni watanzania halisi na hawawezi wakafanya kitu kibaya kwa watanzania. Pia amesema hawawezi kutengeneza mbegu mbaya kwani hata wao ni watumiaji wa mbegu hizi hivyo wako makini saana katiaka kutafiti mbegu hizo. Hata hivyo amewasihi sana kutumia mbegu bora zinazouzwa madukani na kuachana na imani mbaya ambayo imewaacha wakulima wengi kuingia hasara kila wanapolima mazao na kuzidi kubaki katiak maisha duni siku zote.
Akifafanua kuhusu uboreshaji wa mbegu alisema kuwa mbegu zilizoboreshwa ni zile zilizochanganywa sifa za mbegu mbalimbali katika mbegu moja ambayo ndiyo iliyoboreshwa kwa kuziunganisha halisia zake {cross}. Na uboreshaji wa mbegu hufanyika kwa njia halisi bila kuongeza kitu kingine chochote ndani yake.
Akiongea kuhusu maharage, Rose amesema kuwa msimu huu wa kilimo uliopita wametafuta sample ya majani ya magonjwa mbalimbali kutoka kila mahali ili kutambua magonjwa shambulizi ya maharage ili waweze kugundua magonjwa sumbufu na mwisho wa siku waweze kudhibiti magonjwa hayo kwa kuzalisha mbegu stahimilivu wa magonjwa hayo ama kwa kutafiti dawa ambayo itadhibiti magonjwa hayo.
Mwisho amewasihi wakulima kutumia maonyesho ya wakulima yajulikanayo kama nane nane amabay hufanyika kila mwezi August {8} kwa manufaa zaidi kwa kuwauliza wataalamu wa kilimo maswali yenye manufaa na kutaka kujifunza kutoka kwao hata kimatendo baddala ya kuyatumia maonyesho hayo kwa kujifurahisha. Amewasihi sana kutembelea Banda la kilimo nanenane mkoani Mbeya na wao wako tayali kwa moyo mkunjuf ili kuwasaidia wakulima, na baada ya maonyesho pia waweze kufika kituoni uyole kwa msaada zaidi. Pia ametoa wito kwa vyomba vya habari kuwaunga mkono wataalamu wa kilimo kote nchini kuwaelimisha wananchi njia ya kilimo bora na matumizi ya mbegu bora.
MWANAMKE ALIYEJERUHIWA KWA BOMU LA POLISI AKATWA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA
Mkazi wa Mbagala Zakhiem, Mwanaharusi
Hamis amepoteza kiganja chake cha mkono wa kulia baada ya kulipuliwa na
kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu lililorushwa na polisi wakati wakitawanya
wananchi. Mwanaharusi alilipuliwa na bomu hilo Agosti Mosi 2014,
saa 3:00 usiku alipokuwa anatoka ndani kwenda msalani.Akizungumza na
mwandishi jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wodi ya Mwaisela
namba mbili alikolazwa, alisema tukio hilo limebadilisha kabisa
mustakabali wa maisha yake.Mwanaharusi, ambaye ni mama wa watoto wawili
alisema alikumbwa na madhila hayo wakati polisi walipokwenda mtaani kwao
kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki.
Alisema walipofika, vijana waliokuwa maeneo hayo waliwarushia polisi
mawe, ndipo polisi walipofyatua mabomu ya machozi na risasi kuwatanya
wananchi hao.
“Ilikuwa saa 3:00 hivi mimi na watoto wangu tukiwa ndani hatujui nini
kinachoendelea nje, ghafla tulianza kusikia milio ya risasi na mvumo wa
kitu kuelekea upande wa ilipo nyumba yetu. Wakati huo nilikuwa natoka
ndani kwenda msalani, nikaona kitu kimenipiga na kunichana sehemu za
mkono na miguuni, baadaye nikagundua kilichonipiga kilikuwa bomu,”alisimulia Mwanaharusi.
Alisema baada ya tukio hilo polisi walimpelekea kituoni kwa ajili ya
kupata fomu namba ya tatu ya matibabu (PF3) na baadaye Hospitali ya
Temeke, alikopewa rufaa ya kwenda Muhimbili kwa kuwa alikuwa akitoka
damu nyingi.
“Nimechanganyikiwa. Mimi ndio mtafutaji wa familia, mwanangu wa kwanza amemaliza kidato cha nne na wa pili ana miaka tisa,” alisema.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema ufafanuzi utatolewa leo na kamanda wa Kanda ya Dar
es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Friday, August 1, 2014
TGT NA MBINU YA MKULIMA MWEZESHAJI KUKOMBOA KILIMO CHA PAMBA NCHINI
Lydia Mapunda
Katika
maisha ya sasa mkulima ni mtu pekee anayetakiwa kuheshimiwa kutokana na
kutokuwa na historia ya kugoma na kuendelea kufanya kazi hata katika mazingira
magumu yasiyostahili. Japokuwa serikali imekuja na misemo mingi ihusuyo kilimo
ambayo kwa wakati mwingine imekuwa ikimtia moyo mkulima katika kazi yake lakini
amebakia kuwa mtu mwenye kipato cha chini kisichoendana na msemo wa ‘kilimo
ndio uti wa mgongo Tanzania’.
Katika
kipindi cha miaka ya 70 hadi 80 mwishoni mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Singida,
Mara, Kagera na Tabora ilikuwa maarufu sana kwa kilimo cha pamba ambapo ilikuwa
ikizalisha asilimia 95 ya zao hilo.
Lakini kwa upande wa mikoa ya ukanda wa mashariki ya Morogoro, Manyara, Tanga na Kilimanjaro uzalishaji wake ulikuwa ni asilimia tano. Kitu ambacho ni tofauti na hali ya sasa ambapo imefikia wakati wakulima kukata tama ya ulimaji wa zao hili katika mikoa hiyo.
Lakini kwa upande wa mikoa ya ukanda wa mashariki ya Morogoro, Manyara, Tanga na Kilimanjaro uzalishaji wake ulikuwa ni asilimia tano. Kitu ambacho ni tofauti na hali ya sasa ambapo imefikia wakati wakulima kukata tama ya ulimaji wa zao hili katika mikoa hiyo.
Hata
hivyo pamba ilitoa ajira nyingi kwa wantanzania wakiwemo wa vijijini na mijini,
na pia ilikuwa chanzo kizuri cha mapoato ya nchi ya fedha za kigeni kutokana na
kiasi kikubwa cha pamba kuuzwa nje ya nchi. Pamba iliyokuwa inapatikana kwa
miaka ya nyuma ilifanyika matokeo ya kuwepo kwa viwanda kama vile Urafiki,
Mwatex, Mbeyatex, Kilitex, Mutex na vingine vingi nchini ambavyo kwa sasa
baadhi ya viwanda hivyo vimebakia kuwa historia kutokana na kubadirika na kuwa
magofu kwa kutokufanya kazi kutokana na uhaba wa pamba nchini.
Tanzania Gatsby Trust (TGT) ni shirika lililo anzishwa na Lord David Sainsbury wa Turville, ambaye ni mwanzilishi wa Gatsby Charitable Foundation. Shirika hili ambalo makao makuu yake kwa hapa Tanzania yapo jijini Mwanza lina nia ya kukiinua kilimo cha pamba katika mikoa inayojishughulisha na kilimo hicho. Hata hivyo shughuli ambazo zinafanywa na TGT ni kuwaelimisha wakulima kutumia mfumo wa kilimo cha kisasa ili kumkomboa mkulima katika hali ya umaskini
Bwana
Ruyemerya ambaye ni mshauri wa TGT amesema kuwa Mbinu kubwa wanayoitumia TGT ni
kuanzisha kilimo hifadhi (conservation agriculture), ambapo wao kama
TGT walitafuta wakulima wachache kutoka sehemu mbali mbali za ukanda wa ziwa na
kuwapa mafunzo ya kilimo hifadhi na kuwapa uhalali ya kwenda kuwafundisha
wakulima wenzao kitu ambacho kinafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kurudisha
matumaini kwa wakulima wa pamba kwamba
wanaweza wakarudi katika hali ya zamani ya kuliingiza zao la pamba kwa mara
nyingine tena katika ramani ya dunia kwa kutumia kilimo hifadhi.
Kwa kupitia elimu ya mkulima mwezeshaji Finias
Rafael wa kibondo mkoani kigoma ambaye ni mkulima mwezeshaji wa kilimo cha
mahindi pamoja na pamba alisema kuwa tangu ameanza kazi hiyo aliyopewa na TGT ana uzoefu wa miaka miwili sasa na ameshuhudia
kuwa kilimo cha pamba changamoto zake kubwa ilikuwa ni bei ya kuuzia pamba
ambapo amedai kuwa kwa sasa bei si hoja kutokana na uzalishaji anaoupata
kutokana na kanuni za kilimo bora ambapo alidai kuwa wakulilma wengine
walimfuata ili awape mafunzo naye bila hiyana anafanya hivyo kwasababu hiyo
ndio kazi kubwa ya mkulima mwezeshajia aliyopewa na TGT.
Nae
Enock nyambui mkulima mwezeshaji kutoka Musoma alisema kuwa kutoka kilo 300 au
250 kwa hekta alizokuwa akipata hapo awali lakini kwa sasa huvuna kilo 1000
mpaka 1200 kwa hekta na pia amewasihi wakulima wengina kuachana na kilimo
tulicho achiwa na mababu zetu na tubadirike kutokana na sayansi na teknologia
ili kuachana na malalamiko ya kila siku kwa serikali.
Wote
kwa ujumla wameipongeza TGT kwa Elimu yao kwani hata wananchi wameonyesha
mwitikio mkubwa katika kilimo hifadhi baada ya kuona mafanikio kutoka kwa
wakulima wawezeshaji.
Bwana
Enock aliwakosoa wakulima wanaokataa kutumia dawa ya kupuliza shambani kwa
madai ya kuwa yanaharibu afya, na kusema kuwa ni upotofu na ni ufinyu wa mawazo
na elimu. “me nashangaa sana wanatumia vipodozi vya kubadiri ngozi na nywele
bila woga lakini wanaogopa kutumia dawa ya kuuwa wadudu shambani eti inaharibu afya, na wanaovuta sigara pia nao wanalalamika
wanasahau wanatumia kitu ambacho paketi yake too ina onyo juu basi tuache vitu
vyote vya viwandani.”
Kwa
upande wake mkulima mwezeshaji kutoka mkoa wa Simiu Bwana Lupande Nila amesifia
sana matumizi ya jembe la liper ambayo amepata kutoka TGT. Jembe hilo limefanyika
mkombozi mkubwa kwa mkulima kwakuwa hutumia mda mfupi kufanya kazi kubwa sana
na matumizi wa jembe hili huruuhusu maandalizi ya shamba mapema sana na huepusha
usumbufu kwa udongo na huuwezesha udongo kuhifadhi unyevu shambani tafauti na
kilimo cha jembe la mkono au plau.
Waandishi wa habari wakiwahoji wakulima wawezeshaji
Hata
hivyo Bi Everina Lukonge ambaye ni mtafiti wa zao la pamba kutoka UARI
(Ukiriguru Agricultural Research Institute) amesema kuwa, Wanatoa mbegu nzuri
zinazostahimili hali ya hewa ya ukanda wao ili kuwapa wakulima mbegu ambazo
zitawafanya kupata pamba bora na ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa pamba mbegu
kwa kumrahisishia mkulima ghalama ya mbegu kwa msimu unaofuata. Pia amewaomba
wakulima kutoa ushirikiano kwao kama watafiti ili kuweza kupata mrejesho bora
kutoka kwao ili kuweza kurahisisha kazi ya utaafiti kuwa bora zaidi.
Pia
Bi Everina amewatoa wasiwasi wakulima kwa kusema kuwa ukiriguru ina kitengo cha
Agronomia ambacho kinasimamia utafiti wa mbegu bora, aina bora ya kilimo,
utafiti wa udhibiti wa magonjwa ya pamba pamoja na kutoa elimu kwa wakulima ili
kufikia malengo ya kilimo bora Tazania hivyo kuwataka wakulima kutokusita
kuwafuata pale wanapohitaji msaada kutoka kwao kama wataalamu.
Pembejeo
za kilimo muhimu yaani mbolea, madawa na mbegu bora ni changamoto
inayowakabilil wakulima wengi nchini iwapo
zinaendelea kupatikana kwa mawakala binafsi ambao huleta kufuatana na
mahitaji na ununuzi kutoka kwa wakulima. Hata hivyo pembejeo nyingi
zinapatikana makao makuu ya mikoa na wilaya, na chache katika maeneo ya
vijijini. Japo ipo sababu ya kuendelea
kuhamasisha wakulima kutumia pembejeo ili kuongeza tija katika kilimo. Vilevile
kuhamasisha wafanya biashara wenye uwezo kifedha maeneo ya vijijini na vyama
vya kuweka na kukopa kuwa mawakala wa pembejeo kwakuwa asilimia kubwa ya
wakulima wapo vijijini na si mjini. Serikali pia itoe kipau mbele kwa mawakala
waishio vijijini kupata pembejeo kwa wingi na kwa haraka ili kwenda sambamba na
msimu wa kilimo.
Hata
hivyo, mabadiliko ya sayansi na teknolojia pamoja na sera ya uchumi wa huria
duniani ambayo Tanzania haikuwa imejiandaa kikamilifu ilifanya viwanda vyake
vishindwe kuhimili kishindo. Kitu ambacho kimewaacha watu wengi kupoteza ajira
zao hata kwa upande wa kilimo ambacho mapaka sasa bado ndio mkombozi kwa
watanzania. Hivyo serikali inatakiwa kujipanga na kujidhatiti katika kilimo
ambacho ndio tegemeo la wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)



