MKAZI wa Kijiji cha Lupili wilayani
Misungwi Mkoa wa Mwanza, Tecla Kazimili (24), amejifungua watoto wanne,
watatu wa kike na mmoja wa kiume kwa njia ya kawaida katika hospitali
mbili tofauti na siku mbili tofauti.
Katika
hospitali ya kwanza, ambayo ni zahanati ya Kijiji cha Lupili Agosti mosi
mwaka huu, Tecla alionekana ana ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja ambapo
wakati wa kujifungua, alizaliwa wa kiume akiwa na kilo 1.6, lakini kwa
bahati mbaya alikufa.
Hata hivyo, wakunga walishuhudia mzazi
huyo akiendelea kuwa na dalili ya kujifungua mtoto mwingine, lakini
akawa amegoma kupita katika njia.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Marko Mwita, alisema
baada ya kutokea kwa hali hiyo, alipigiwa simu kuombwa msaada.
“Baada
ya kupokea taarifa hiyo majira ya usiku, nilituma gari la wagonjwa
kukimbilia kwenye zahanati hiyo iliyopo umbali wa kilometa 60 na kumleta
mama huyo katika Hospitali ya Wilaya kwa huduma zaidi,” alisema.
Alisema alipofikishwa hospitalini hapo, Tecla aliendelea kujifungua mpaka kesho yake hatimaye idadi ya watoto ikafikia wanne.
“Hili
ni tukio la kwanza katika hospitali hii ya Wilaya, mtu kujifungua
watoto wanne, ni matukio yanayotokea mara chache, lakini tunamshukuru
Mungu mzazi anaendelea vizuri huku watoto wake watatu, wote wa kike kila
mmoja akiwa na uzito wa kilo mbili,” alisema.
Dk Mwita alisema
watoto hao wanahitaji uangalizi na msaada wa hali ya juu, kwani ni
rahisi kupata maambukizi. Alitoa mwito kwa jamii kumsaidia mama huyo,
kwani watoto hao wanahitaji msaada wa hali na mali kwa kuwa maziwa ya
mama pekee hayatawatosheleza.
Akizungumzia historia yake ya
uzazi, Tecla alisema watoto hao ni uzazi wake wa nne na katika ule
uliopita, watoto wote aliowazaa walifariki dunia katika umri tofauti,
lakini wa utoto.
“Kitendo cha watoto kufa baada ya kufikisha
umri fulani, kilimfanya mume wangu anifukuze, nikalazimika kurejea
nyumbani kwetu ambapo nilipewa ujauzito na kijana mwingine,” alisema.
Alisema
wakati anahudhuria kliniki, alielezwa kwamba alikuwa na zaidi ya mtoto
mmoja baada ya kutoa taarifa kuwa anaona tabia ya ujauzito huo ni
tofauti na uzazi wake uliopita.
“Namshukuru Mungu kwa kunipatia
watoto hawa na naiomba Serikali inisaidie kuwatunza ili wakue vizuri
kwani peke yangu siwezi,” alisema. Kwa mujibu wa Tecla, aliumwa uchungu
kwa siku tatu na alimaliza kujifungua Agosti
No comments:
Post a Comment