Saturday, September 6, 2014
JOHN MNYIKA KUMSHITAKI PINDA MAHAKAMANI
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Jijini Dar es
Salaam Mh. John Mnyika anakusudia kumshtaki mahakamani Waziri Mkuu Mh.
Mizengo Pinda kwa kosa la ofisi yake kushindwa kutangaza tarehe pamoja
na maadalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam huku akiwa ameambatana na mwanasheria wake, Mh. Mnyika amesema moja ya hoja zilizomo katika shauri watakalofungua kuwa ni kutaka mahakama imlazimishe waziri mkuu Mh. Pinda, atoe kanuni pamoja na kutangaza ni lini uchaguzi huo utafanyika baada ya kile alichodai kuwa ni kuwepo kwa kimya kirefu kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huo.
Mh. Mnyika amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatakiwa itangaze pamoja na kutoa kanuni za uchaguzi huo miezi miwili kabla ya mwezi Oktoba na kwamba kitendo cha ofisi hiyo kukaa kimya hakileti tafsiri sahihi juu ya hatma ya uchaguzi huo.
Mbali ya kutaka waziri mkuu atangaze kanuni na siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, Mnyika amesema katika hoja zake ataiomba mahakama iitake serikali ibadilishe taratibu na sheria zinazosimamia uchaguzi huo ili uwe huru na wa haki.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam huku akiwa ameambatana na mwanasheria wake, Mh. Mnyika amesema moja ya hoja zilizomo katika shauri watakalofungua kuwa ni kutaka mahakama imlazimishe waziri mkuu Mh. Pinda, atoe kanuni pamoja na kutangaza ni lini uchaguzi huo utafanyika baada ya kile alichodai kuwa ni kuwepo kwa kimya kirefu kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huo.
Mh. Mnyika amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatakiwa itangaze pamoja na kutoa kanuni za uchaguzi huo miezi miwili kabla ya mwezi Oktoba na kwamba kitendo cha ofisi hiyo kukaa kimya hakileti tafsiri sahihi juu ya hatma ya uchaguzi huo.
Mbali ya kutaka waziri mkuu atangaze kanuni na siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, Mnyika amesema katika hoja zake ataiomba mahakama iitake serikali ibadilishe taratibu na sheria zinazosimamia uchaguzi huo ili uwe huru na wa haki.
Friday, September 5, 2014
DUUUUUU
FREEMASON WATOA TAMKO KUHUSU MWISHO WA DUNIA HII..!!
WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet,
sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali. Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani. DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).
WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu. Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru). Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu. Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia. Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba. Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja. Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo). Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea
RAIS KIKWETE AONGOZA UFUNGAJI WA ZOEZI LA MEDANI LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50
.jpg)
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia madhara ya mapigo ya
silaha mbalimbali wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho
ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo
Septemba 5, 2014.
.jpg)
Sehemu ya
askari wakitoka katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani
la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
.jpg)
.jpg)
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakisimama kwa wimbo
wa Taifa wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka
50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba
5, 2014.
.jpg)
Askari wa
kikosi cha mizinga akichukua taswira meza kuu wakati wa ufungaji wa
zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
.jpg)
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakipata picha ya
kumbukumbu na sehemu ya wapiganaji wakati wa ufungaji wa zoezi la medani
la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
.jpg)
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza askari wanawake
walioshiriki katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la
maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli,
Arusha, leo Septemba 5, 2014.PICHA NA IKULU
ZAIDI YA WATU 30 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA MKOANI MUSOMA. TAFADHALI PICHA ZINATISHA

Basi
la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa
likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana
baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA
COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini
Musoma mchana huu.Watu 25 wamepoteza maisha papo hapo na wengika
kujeruhiwa vibaya sana.kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio
hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo
lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja
linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo
lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo
ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia
na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa
itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine
linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi
kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu
watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad
Michuzi,Musoma.

Basi
la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4
EXPRESS.


Umati
wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya
na kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio
hilo la ajali.

Guldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia
mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na
mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.


Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.

Uokozi ukiendelea.

Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

Mabasi hayo yakiwa yamegongana 








Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Waandishi wa Habari mkoani Mara Frolence Focus wa Mwananchi na Pendo Mwakembe wa Raia Tanzania wamenusulika kwenye ajali hiyo wakiwa kwenye basi la Mwanza Coach kutokea Musoma.
Akizungumzia kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba 4 hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mra, Frolence amesema walishangaa kuona abiria waliokuwa wamekaa mbele wakisimama na kurudi nyuma na ghafla akasikia mlio mkubwa.
Akizungumza na Redio kahama fm nje ya chumba cha (ICU) kwa niaba ya Mganga Mkuu, Dakatari Martini Khani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa wamepokea idadi kubwa ya maiti na majeruhi huku idadi kamili ikiwa bado haijafah
Miili ya Abiria waliokufa ikiwekwa vizuri ili kutambuliwa
Mahututi wakikimbizwa wodini
| wanainchi wakiwa kwenye simanzi |
Watu wakitambua miili ya marehemu
Basi la
Mwanza coach limepata ajali eneo la sabasaba likiwa njiani kuelekea
mwanza na kuua watu zaidi ya 30 na majeruhi wengi,Taarifa kamili
inakujia punde kaa nasi.
UKATILI KIASI HIKI
UKATILI WA KUTISHAMAMA ADAIWA KUMSULUBU MTOTO, APEWA KIBANO
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi
zilidai kwamba, Teddy alimchukuwa mtoto huyo jijini Arusha kwa lengo la
kumsaidia kukaa na mwanaye kwa kuwa familia ya mtoto huyo haina uwezo na
ameishia darasa la tatu kwa kukosa vifaa vya shule.
Kwa mujibu wa Teddy, bila kujua kwamba
ni kosa kumwajiri mtoto, aliamua kumwadhibu mtoto huyo kutokana na
kutomsikiliza bosi wake hasa alipokuwa akionywa kuachana na tabia ambayo
haikuwa ikimfurahisha.
Kwa upande wake Magdalena alidai kwamba
alikuwa akipokea kipigo kila siku hasa wakati mama huyo alipokuwa
akirejea nyumbani kutoka ‘jobu’ na kukuta mwanaye analia.
“Alikuwa akinipiga kila siku akikuta mtoto (wa miaka miwili) analia. Pia kuna siku alinipiga
sana asubuhi, nikaona nikimbilie kwa mjumbe, ndiyo tukaenda kituo cha
polisi, tukakutana naye akiwa anatoka polisi kutoa taarifa kuwa
nimepotea, mimi naomba nisaidiwe nirudi kwa mama yangu Arusha,” alisema
Magdalena na kumfanya bosi wake huyo apewe kibako na vyombo vya sheria.
WABUNGE KUGOMBEA UBUNGE NA ELIMU YA DARASA LA SABA.
Dodoma. Pendekezo la Rasimu ya Katiba kuwa wabunge walau wawe na elimu ya kidato cha nne limetupiliwa mbali na wajumbe wa Bunge Maalumu, baada ya Kamati karibu zote kulikataa.
Kamati hizo zimependekeza kigezo cha elimu kuanzia walau kidato cha nne kama sharti muhimu la mtu anayetaka kugombea Ubunge kiondolewe, badala yake mgombea ama ajue tu kusoma na kuandika, au ajue kusoma na kuandika Lugha ya Kiswahili au Kiingereza kama ilivyo kwenye Katiba ya sasa.Mbali na pendekezo hilo, kamati hizo zimegawanyika kuhusu Ibara ya 129 ya Rasimu ya Katiba inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao madarakani kabla ya miaka mitano kumalizika.
Hayo yalijitokeza bungeni Dodoma jana, wakati kamati hizo zikiwasilisha taarifa zake kuhusu Sura ya 9 na 10 ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Akiwasilisha maoni ya Kamati Namba 10, Mjumbe wa kamati hiyo, Dk Dalaly Kafumu alisema suala la kugombea nafasi yoyote ni la kidemokrasia, hivyo haipaswi mtu yeyote kuzuiwa kwa kigezo cha elimu.
“Haki ya kuamua iwapo mgombea anafaa au hafai ni ya wapigakura. Wasizuiwe kikatiba kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua mtu wanayemtaka,”alisema na kuongeza: “Utaratibu huu haupo duniani kote hata nchi zilizo na demokrasia iliyokomaa. Hivyo ibara hiyo isomeke tu ajue kusoma na kuandika na si kiwango cha elimu kama sifa ya msingi.”
Mapendekezo hayo yaliungwa mkono na Kamati Namba 8 kupitia kwa Mjumbe wake, Juma Alawi aliyesema kuweka kiwango cha elimu kwa wagombea ubunge ni ubaguzi.
Kuondolewa kwa kigezo cha elimu ya kidato cha nne pia kumeungwa mkono na kamati namba 10, 4, 12, 9 na 12 za Bunge hilo zilizowasilisha taarifa zake jana asubuhi.
Kamati namba 12 ndiyo iliyokwenda mbali zaidi na kudai kuwa ibara hiyo itasababisha ubaguzi kulingana na elimu wakati kiwango cha chini cha elimu kwa Tanzania Bara ni darasa la saba na Zanzibar ni darasa la 10.
Hata hivyo, ni Kamati Namba 2 tu inayoongozwa na Shamsi Vuai Nahodha iliyokubali pendekezo la Rasimu la kutaka kuwapo kigezo cha elimu. Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo, Vuai alitaka ibara hiyo ifanyiwe marekebisho na kufuta maneno “anajua kusoma na kuandika Kiingereza na Kiswahili” na badala yake isomeke, “ana elimu isiyopungua kidato cha nne”.
Wakati kamati karibu zote zikikubaliana kuhusu kuondoa kigezo cha elimu katika kuwania ubunge, zimetofautiana kuhusu Ibara ya 129 ya inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao asiyewajibika kwao.
Mapendekezo ya Tume ya Jaji Warioba yalitaka wananchi wawe na haki ya kumuondoa mbunge, endapo ataunga mkono sera zinazokwenda kinyume na masilahi ya wapigakura wake au iwapo atashindwa kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero zao au ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka jimbo lake kwa miezi sita bila sababu.
Kamati Namba 12 iliafiki wananchi kupata nguvu hiyo ya kumuondoa mbunge endapo tu atakuwa ameunga mkono sera ambazo zinakwenda kinyume na masilahi ya taifa na si ya wapiga kura waliomchagua.
“Kimsingi hakuna namna bora ya kumtathmini mbunge kuwa ameshindwa kutekeleza na kutetea hoja na kero za wapigakura,” alisema Jaffo kwa niaba ya kamati.
Kamati namba 8, 2, 10, 4 na 9 zilipendekeza ibara hiyo ifutwe isipokuwa kamati namba 9 iliyoenda mbali zaidi na kupendekeza kutungwa kwa sheria ya kumdhibiti mbunge anayeshindwa kutekeleza majukumu yake.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walio wachache katika kamati zao walipendekeza ibara hiyo ibaki kama ilivyo kwenye Rasimu. Maoni ya kamati mbalimbali za walio wachache waliounga mkono kubaki kwa ibara hiyo yalisomwa na Dk Tulia Ackson na Elizabeth Minde ambao wote ni wanasheria kitaaluma.
Wakati huo huo, suala la kuwapo au kutokuwapo kwa Mahakama ya Kadhi katika Katiba Mpya jana liliibuka tena Bungeni baada ya wajumbe walio wachache kutaka liingizwe kwenye Katiba.
Subscribe to:
Posts (Atom)






