Tabasamu la matumaini baada ya kupata ahueni ya Ebola
Hospitali moja nchini Marekani imewaruhusu wamisionary wawili wa kimarekani ambao walikua
wakipata tiba kutokana na kuathiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, na
imethibitishwa hawana athari kwa afya ya jamii.Dr Kent Brantly na
mtabibu mwenziwe Nancy Writebol ambao waliruhusiwa mapema wiki hii
walipata maambukizi ya ugonjwa huo wakati wakiwasaidia wagonjwa wa
ugonjwa huo nchini Liberia.Kutokana na maambukizi walopata watabibu hao
walipata maambukizi walipewa dawa ya majaribio ambayo haikuwahi kupewa
binadamu hapo kabla,na dokta aliyekuwa zamu alishindwa kuthibitisha juu
ya nafuu yao kama imetokana na dawa hiyo ya majaribio.
Kufuatia matokeo mazuri ya dawa hiyo ya majaribio dokta huyo wa zamu alijinasibu kuwa kituo
chake kimejifunza namna bora ya kumsaidia mgonjwa wa bola na mazingira
alimokuwamo, na kuahidi kushirikisha utaalamu huo kwa watabibu kutoka
katika nchi za Kiafrica.
Nalo shirika la afya ulimwenguni W.H.O linaandaa mkutano utakao fanyika mwanzoni mwa mwezi huu katika mji wa Geneva nchini uswiss, utakaoangazia namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.
Takwimu za hivi karibuni zaonesha
kwamba zaidi ya watu elfu kumi na tatu wamekufa kwa ugonjwa huo hasa
kutoka katika nchi za Africa Magharibi Liberia,Sierra Leone na Guinea.
No comments:
Post a Comment