Habari ambazo zimethibitishwa na facebook page ya kanisa la Ufufuo na Uzima zinasema kuwa Helkopta hiyo imewasili nchini tayari na sasa inafanyiwa assembling kwaajili ya kuanza kuruka jumatatu hii. Tukio ambalo limelifanya kanisa hilo kuandaa ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kupokea helcopta hiyo itakayotumika kusambaza injili Tanzania.
Hii inakuwa Helkopta ya kwanza kutumika kuhubiri injili ikiwa ni mali ya kanisa. Ibada ya shukrani kanisani Ufufuo na Uzima ilihudhuriwa na waimbaji kama Munishi akiwa na Malebo (ameokoka), Rose Muhando, Bony mwaitege, John Lisu, Upendo Nkone, Flora Mbasha, Christina Shusho na wengine wengi..
na hivi ndivyo ilivyokuwa katika picha
No comments:
Post a Comment