Chande Abdallah na Deogratius Mongela FUNDI
ujenzi aliyefahamika kwa jina la Omari Mkulu (25) amedaiwa kuuawa na
kutupwa ndani ya bwawa baada ya kudaiwa kutoweka nyumbani kwa takriban
siku tatu.
Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Omari Mkulu (25)ambaye alikuwa fundi wa ujenzi.
Tukio hilo lilitokea maeneo ya Mabwawa
Saba, Mabibo jijini Dar ambapo majirani wa eneo hilo walidai kuwa
waliiona maiti ya Omari ikiwa inaelea kwenye moja ya bwawa eneo hilo
lakini kutokana na maiti hiyo kuvimba haikuwa ikitambulika.
Mmoja wa ndugu wa marehemu Omari Mkulu akilia kwa uchungu.
Kwa mujibu wa marafiki zake ambao walifanya
jitihada za kusafiri hadi Chanika kwa baba wa marehemu ili kuhakikisha
kama kweli maiti ile ilikuwa ni ya Omari na kuthibitisha kuwa ni kweli,
walidai kuwa kabla marehemu hajatoweka, alilipwa fedha zake za ujenzi
ambapo ilidaiwa kuwa alikwenda kuzitumia kwenye pombe mpaka usiku wa
manane.
Bwawa lililopo eneo la Mabibo (Mabwawa Saba) ambapo maiti ya marehemu Omari Mkulu ilikutwa ikielea.
“Siku ile marehemu alikuwa amelewa sana kwa sababu alikuwa amepata
fedha zake za malipo, tangu siku ile hakuonekana tena mpaka leo hii. Kwa
kuwa sura na mwili wake umevimba tumezitambua nguo zake alizovaa,”
alisema mmoja wa marafiki hao aliyeiomba hifadhi ya jina.
Waandishi wetu walipofika katika eneo la
tukio, waliishuhudia maiti hiyo ikitolewa kwenye bwawa hilo ambapo umati
wa watu waliofika katika eneo hilo walipewa nafasi ya kumtambua ambapo
mmoja wa watu waliofika alidai kuwa mtu huyo ni jirani yake,
akawaelekeza waandishi nyumbani kwa marehemu.
Marehemu Omari Mkulu (kushoto) akiwa na marafiki zake enzi za uhai wake.
Waandishi wetu walifika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na mama
mkubwa wa Omari aliyejitambulisha kwa jina la Zainabu Omari ambaye
alisimulia kwa uchungu kuwa mwanaye huyo alitoweka nyumbani Agosti 10,
mwaka huu baada ya kumpatia shilingi 2,000 alizomuomba.
“Siku hiyo alikuwa na shilingi 5,000 mimi akanipa shilingi 2,000
halafu akaniambia kuwa jioni ya siku hiyo kuwa akipata hela ataelekea
kwa baba yake Chanika, sasa tulishangaa tu kikapita kimya hakurudi
nyumbani kuaga wala kuchukua nguo zake mpaka sasa tumesikia amekutwa
amefariki dunia bwawani,” alisema kwa uchungu mama huyo.
CREDIT: GPL
No comments:
Post a Comment