Vijana wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao hawakufahamika
majina yao, wanaodaiwa kuwa ni vibaka alfajiri ya leo wameuawa kwa
kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpora pochi dada
mmoja mkazi wa Tabata Liwiti.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada
ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka kutoweka na bodaboda
ndipo wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora pochi hiyo akaanguka
chini wakaanza kumpa kipigo huku mwenzake akifanikiwa kuondoka.
Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo aliyekuwa
akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata
pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa
pamoja wakavishwa matairi na kuchomwa moto.
No comments:
Post a Comment