Spika
wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa
kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa
Jumuiya.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
Spika
wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa
vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leoNaibu
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah
Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya
ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika
Mashariki, Phyllis Kandie (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri
kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni
Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo Wilbert KaahwaNaibu
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala
akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya
ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es SalaamWabunge
wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba
ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment