KWA mara ya kwanza Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na
mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ na kufuta uvumi mzito
uliokuwa ukizagaa kuwa wawili hao ni wapenzi.
Zitto alifunguka hayo juzi kupitia
kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Televesheni ya East Africa ambapo
alikanusha kuwa hana uhusiano wowote wa mapenzi licha ya kudaiwa
kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama ishara ya penzi lao.“Mh! Kama
yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa
kimapenzi,” alisema Zitto.
Katika mahojiano hayo, mheshimiwa huyo
alifungukia skendo nyingine inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo
Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.
Alisema anaumia zaidi kusikia watu
wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia mitandao ya kijamii wakati
hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo wanaheshimiana na kufanya naye
kazi kwa karibu ili kumsaidia katika harakati zake za muziki.
“Naumia sana kusikia wakinisema na
Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa
mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu
kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.
Aidha, mheshimiwa huyo mbali na
kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana
kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Jack,
wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.
No comments:
Post a Comment