Wednesday, August 20, 2014

MAMA AMCHANA MWANAWE WA MIEZI MIWILI NA VIWEMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA BAADA YA MTOTO KUZALIWA AKIWA HANA



Vitendo vya baadhi ya wananchi kujitibu pasipo kufuata maagizo na njia za kitaalamu vimeendelea kukithiri nchini ambapo hapa jijini Mwanza mama mmoja ameamua kumchanja kwa viwembe mwanae mwenye umri wa wiki mbili baada ya
mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya Haja kubwa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya mama huyo aliyefahamika kwa jina la Anastazia Ngilitu kumchana kwa wembe zaidi ya mara tatu ili kumsaidia mwanae kupata haja kubwa kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu
ya haja kubwa.

Akiongea kwa uchungu mama huyo mkazi wa Tabora aishie jiini mwanza kwa sasa amesema kuwa alijifungua watoto mapacha watatu ndani ya Mtaro kisha wawili kufariki alipofikswa Hospitali na kusalia mtoto mmoja aliyekutwa na tatizo la Kutokuwa na sehemu ya haja kubwa.

Sambamba na hayo mama huyo amesema kuwa sababu za kumchana na wembe mwanawe ni baada ya kumuona mtoto wake anashindwa kupata haja kubwa hali
iliyopelekea tumbo kujaa na kulia.

Ameongeza kuwa wakati wa kujifungua mtoto huyo walimfanyia upasuaji katika hospitali ya Bugando ila hali ya kuziba ilijirudia tena na kuamua kumchana kwa
kutoakana na kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama za upasuaji hospitali.

Katika hatua nyingine Mama huyo amesema kuwa kwa sasa hali yake ya Maisha siyo nzuri kwani watoto wake wanaishi kwa kunywa maji na kwamba hapo awali alikuwa anafanya kazi ya kufua nguo kwenye nyumba za watu ila kwa sasa hawezi
kutokana na kuwa na mototo mdogo.

Sambamba na hayo mama huyu anasema kuwa licha ya kuolewa na wanaume watatu kwa wakati tofauti na kila mmoja kumnyanyasa kwa kumpiga na mwingine kumdhurumu pesa zaidi amesikitishwa na kitendo cha Mume wake wa sasa hivi kumtaka kufanya mapenzi ikiwa tumbo la uzazi halijakaza hali anayotaja kumsababishia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi baada ya mumewe
kumpiga.

 
Kitendo cha mama huyu kumchana mtoto wake kwa wembe kinatoakana na hofu ya kwenda hospitali kwani anasema hana uwezo wa pesa kwani kwa sasa yeye mwenyewe anasumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto na alipoenda Hospitali ya SEKOTURE aliambiwa gharama za upasuaji ni shilingi elfu 30 na
alipokosa alirudi nyumbani na kuendelea kujitibu kwa dawa za kienyeji.

Kwa upande wao baadhi ya kina majirani ambao wamekuwa wakimpa msaada mama huyu mara kwa mara,Wamesema kuwa mama huyu ana maisha magumu kwani mume wake humpiga na kumfukuza mara kwa mara hali inayomfanya aishi kwa kuomba omba na wakati mwingine kulala na watoto wake
bila kula.

 
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mama huyu aliolewa na mume wa kwanza mkazi wa eneo la maji moto mkoani Mara na waliachana baada ya kupigwa na kuchomwa kisu tumboni ikiwa ni pamoja na kupigiliwa msumali wa nchi sita katikati ya mkono
wake wa kushoto ikiwa ni sambamba na kumvuta hereni akimwambia kuwa ni dalili za kuwa malaya hali iliyomsababibishia masikio yake kuvimba.

Mume wa pili aliyemuoa mama huyo inaelezwa kuwa yeye alimdhurumu kiwanja walichouza milioni moja na laki saba kilichokuwa eneo la makaburi Bwiru kisha
kuzichukua na kuaga kwenda kuzifanyia biashara.

Kuhusu ndugu Bi Anastazia amesema kuwa wazazi wake wote wamefariki na kwamba aliyebaki ni bibi yake ambaye naye anamtaja kuwa ni mchawi kwani wakati alipoenda Tabora,bibi yake alimwambia ampe mkono wa mtoto ili usiku wa manane
amuamshe kwa kumpiga nao kichwani ili aende kazini.

Anastazia anasema kuwa kutokana na matatizo hayo aliwahi kushauriwa kumtupa mtoto huyo eneo la vichakani soko la sabasaba,ushauri aliopewa na rafiki yake mkazi wa Ilemela aliyemtaja kwa jina moja la Amina ambaye alimwambie mtoto wako hatapona,Jambo ambalo yeye alikataa na kusema kuwa anaogopa mkono wa Sheria.

Tatizo linalomsumbua mama huyo kwa sasa ni chakula na matibabu kwa mwanaye na yeye mwenyewe anayesumbuliwa na uvimbe katika titi la kushoto na kuwaomba wasamalia wema kumsaidia ili aendelee na shughuli zake aondokane na
kuombaomba.


MWONEKANO WA MASIKIO YAKE BAADA YA KUVUTWA HELENI NA MUMEWE WA KWANZA.

No comments:

Post a Comment