CHAMA
cha Alliance Transparency For Change (ACT) Mkoa wa Kigoma, kimeahidi
kumlinda na kumtetea Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe
(CHADEMA), kutokana na changamoto zinazomkumba kupitia watu wachache
wanaotaka kumwangusha kisiasa.
Mjumbe
wa Kamati Kuu Taifa ya chama hicho, Bw. Jaffar Kasisiko, aliyasema hayo
juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Cine Atlas,
kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Alisema
chama hicho hakipo tayari kuyafumbia macho matatizo yanayomkuta Bw.
Kabwe na kumshauri mbunge huyo aachane na CHADEMA badala yake ajiunge na
ACT ili aweze kukusanya wanachama kuanzia ngazi ya kitongoji, vijiji,
kata na wilaya.
Aliongeza
kuwa, uongozi wa CHADEMA una hila ya kusambaza maneno kwa umma dhidi ya
Bw. Kabwe ili kulinda masilahi yao binafsi badala ya kutetea haki za
wanyonge.
“Kabwe
asipoteze muda wa kulumbana na uongozi wa CHADEMA, huu ni wakati
mwafaka kwake kufanya uamuzi makini wa kwenda kuifuta kesi dhidi ya
chama chake mahakamani na kujiunga na ACT,” alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Msafiri Wamalwa.
Katibu
Mwenezi Wilaya ya Kigoma kutoka chama hicho, Anzoluni Kibela, alisema
ACT imeandaa kadi kwa ajili ya Bw. Kabwe ambapo kuna wabunge 18 wapo
tayari kujiunga na chama hicho kwenye uzinduzi rasmi ulipangwa kufanyika
mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.
Naye
Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. Shaban Mambo, aliwasihi
wananchi wamuunge mkono Bw. Kabwe atakapojiunga na chama hicho ili
aboreshe hali ya usafiri wa reli ya kati kwa kuwaletea treni inayotumia
umeme kwa gharama zake.
Baadhi
ya wanachama wapya wa ACT akiwemo aliyekuwa Mweka Hazina wa CHADEMA
Kigoma Ujiji, Bw. Hamidu Hamis na Katibu wa ACT wilayani humo, Bw. Haji
Idd, walisema wamejiunga na chama hicho ili kuleta uwazi na
uwajibikaji
No comments:
Post a Comment