Wednesday, August 27, 2014

MANISPAA YA IRINGA WAIPIKU MANISPAA YA MOSHI KWA USAFI



14tngfst
Manispaa ya Iringa imefanikiwa kuwa ya kwanza kwa usafi na kuchukua tuzo kwa kuipiku manispaa ya Moshi ambayo ina tuzo lukuki kwa usafi na kuwa mfano wa kuigwa na manispaa zingine nchini. Ingawa mwaka huu imepata upinzani mkali kutoka kwa Manispaa ya Iringa ambayo ndiyo imefanikiwa kuwa namba moja kwa usafi lakini manispaa ya Moshi imesema kuwa wao bado washindi.
Victoria Simakundi ambaye ni Afisa Afya wa Manispaa ya Moshi amesema kuwa vigezo viliyoweka vya usafi havihusu usafi tu moja kwa moja kuna masuala ya bajeti pamoja na masuala ya kuweka vitu vipya vya usafi.
7tngfst
Ameongeza kwa kusema Manispaa ya Iringa walikua chini hivyo kuna vitu ambavyo wameweza kuvipata kwa sasa na vinaonekana vipya lakini vitu kama hivyo Manispaa ya Moshi walishavifanya siku za nyuma.
Kuhusu watu wanaochafua Manispaa ya Moshi kuna adhabu amabazo wameziweka ambazo zinaanzia kiasi cha 10,000 hadi 50,000,Manispaa ya Moshi imeshika nafasi ya pili mwaka huu baada ya Manispaa ya Iringa.
2tngfst
Tangu mashindano haya yaanzishwe mwaka 1984 Manispaa ya Moshi imekuwa ikishika nafasi ya kwanza na katika miaka yote,ingawa imeshika nafasi ya pili mara mbili  katika miaka hii 30 ya mashindano haya.
Picha za tuzo zilizopata manispaa ya Moshi mpaka sasa.
10tngfst

11tngfst


No comments:

Post a Comment