Wednesday, August 27, 2014

MWANAFUNZI ABAKWA DAR


Denti wa darasa la saba aliyebakwa na muuza genge anayefahamika kwa jina la Juma Athumani (30)

 Kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala, Dar kuna faili la kesi namba MBL/RB/ 9817/2014- KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI ambalo linamsaka kijana Juma Athumani (30), mkazi wa Charambe, Mbagala kwa kosa la ubakaji wa mwanafunzi wa darasa la saba. Habari za kiintelijensia zilidai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ni muuza genge, alitenda kosa hilo Agosti, mwaka huu ambapo mwanafunzi huyo alikuwa ametumwa na mama yake gengeni.Ilisemekana kwamba jamaa huyo alimuomba denti huyo wazungumze kidogo ndipo akampeleka gesti kwa lazima. 

Akizungumza na wanahabari za mastaa na kijamii, mwanafunzi huyo alisema kuwa alipofika gesti, jamaa huyo alilipa fasta na kumvutia chumbani ambapo alianza kumshika maziwa yake kisha akamtupia kitandani na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake.
Mama wa mwanafunzi aliyebakwa.
 Alisema kwamba, jamaa alipomaliza shida zake, alimpa tsh elfu tano (5,000/=) lakini alipokataa huku akilia ndipo mwanaume huyo akamuongezea hadi ikafika elfu kumi (10,000/=).
“Niliporudi nyumbani mama aliniuliza kwa nini nimechelewa kisha akaziona hela, akaniuliza nimezipata wapi, nikamwambia amenipa Juma ndiyo tukaenda hadi gengeni kwa Juma kuuliza ndiyo mama akagundua kuwa nimebakwa. 
“Baadaye mama alikwenda kuripoti polisi ndipo Juma akakamatwa na mimi nikapelekwa hospitali na kugundulika kweli nilikuwa nimebakwa,” alisema mwanafunzi huyo.
Habari zilizotufikia punde zilidai kwamba uchunguzi wa polisi unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

No comments:

Post a Comment