Wakati hayo yakitokea Kenya hapa Tanzania kanisa lingine la ajabu limegunduliwa ambapo linafanya ibada zake
kwa utofauti mkubwa na makanisa yaliyozoeleka na wengi.
Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam
lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake
Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.
Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hilo ni kupinga jina la Biblia Takatifu. Muumini mgeni anayefika kwenye kanisa hilo hulazimika kukabidhi Biblia yake kwa uongozi ambapo wao hutoa ‘kava’ ya nje yenye jina la Biblia na kuweka kava nyeupe yenye maandishi ya Kitabu Cha Bwana.
Kama vile hayo hayatoshi, kanisa hilo linaamini siku za mwezi ni 28 na si 29, 30 au 31. Wanasema Mungu alipanga hivyo na ndiyo maana aliwapa hata wanawake mzunguko wa siku 28 kuingia katika hedhi.
“Kinachotuingiza
kwenye majira halisi ya Mungu ni kufuta tarehe 29, 30 na 31 za Julius
Kaisari katika kila mwezi wa kalenda ya Gregori kwa mamlaka ya Mungu wa
Majeshi ili kuondoa uovu ulioambatana na tarehe hizo za ziada kwenye
miezi 12 ya mwaka,” alisema muumini mmoja kanisani hapo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo lilichapisha kitabu ambacho kinaonesha kuwa mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi (wao huita Abib au Aviv). Na mwisho wa mwaka si Desemba, bali ni Februari (wao huita Adari).
Kwa ugunduzi wao huo, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo hawafanyi ibada
ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Desemba 25, yaani Krismasi kama
madhehebu mengine ya Kikristo kwa vile wanaamini Yesu alizaliwa
Februari 28.
Aidha,kiongozi mmoja alijitambulisha kwa jina la Daudi alimtaja kiongozi mkuu wa kanisa hilo kuwa ni Mchungaji Elia wa Pili Mungu wa Majeshi Mtume na Nabii wa kizazi cha nne na akabainisha kuwa, awali alikuwa akifanya kazi Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kama mhandisi.
“Aliacha kazi ya uhandisi na kuanza kumtumikia Mungu wa kweli kuanzia mwaka 2003, kazi ambayo amekuwa akiifanya hadi sasa ambapo kanisa limesimama na kuenea Tanzania nzima na duniani,” alisema Daudi.
Aliongeza kuwa, Mungu alimwambia nia ya kumteua afanye kazi za kiroho
ni kuvunja misingi mibovu ya kumuabudu na kuiweka inayofaa.
Mchungaji huyo ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya kiongozi mkuu, alisema kanisa hilo limekuwa na maagizo ya kweli ambayo Mungu aliagiza yafanyike.
Kiongozi huyo akizungumzia namna ya kujiunga na kanisa hilo alisema kuwa, sharti la kwanza ni mtu kubadili jina lake la awali na kupewa lingine ambalo ni matakwa ya Mungu kisha kubatizwa upya.
Alisema kanisa hilo halikubaliani na mambo ya dunia kama vile kuwa na Siku ya Kifua Kikuu, Siku ya Ukoma, Siku ya Ukimwi na kadhalika kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ufalme wa Mungu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaoishi jirani na kanisa hilo walipohojiwa kuhusiana na nyumba hiyo ya ibada walisema wana wasiwasi na nguvu za kishirikina ndiyo zinaratibu mwenendo wao.
“Huwezi kuchana ‘kava’ la Biblia na kukataa jina la Biblia Takatifu
kwa sababu kufanya hivyo ni kama uchawi ambao kwa Mungu haufui dafu,”
alisema muumini mmoja ambaye alikataa kutaja jina.
Waumini wa makanisa mengine husema “Hawa wanaosema namba za mwezi mwisho tarehe 28 ni mambo ya Freemason. Sisi tunaona hivyo,” alisema muumini mmoja ambaye naye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Hivi karibuni gazeti hili liliibua kanisa lingine liitwalo Brotherhood of the Cross and Star la jijini Dar ambalo waumini wake husujudu na kuingia kanisani wakiwa pekupeku huku mabikira wakipewa kipaumbele cha kupelekwa nchini Nigeria, makao makuu ya kanisa hilo.
Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hilo ni kupinga jina la Biblia Takatifu. Muumini mgeni anayefika kwenye kanisa hilo hulazimika kukabidhi Biblia yake kwa uongozi ambapo wao hutoa ‘kava’ ya nje yenye jina la Biblia na kuweka kava nyeupe yenye maandishi ya Kitabu Cha Bwana.
Kama vile hayo hayatoshi, kanisa hilo linaamini siku za mwezi ni 28 na si 29, 30 au 31. Wanasema Mungu alipanga hivyo na ndiyo maana aliwapa hata wanawake mzunguko wa siku 28 kuingia katika hedhi.
Uchunguzi unaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo lilichapisha kitabu ambacho kinaonesha kuwa mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi (wao huita Abib au Aviv). Na mwisho wa mwaka si Desemba, bali ni Februari (wao huita Adari).
Aidha,kiongozi mmoja alijitambulisha kwa jina la Daudi alimtaja kiongozi mkuu wa kanisa hilo kuwa ni Mchungaji Elia wa Pili Mungu wa Majeshi Mtume na Nabii wa kizazi cha nne na akabainisha kuwa, awali alikuwa akifanya kazi Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kama mhandisi.
“Aliacha kazi ya uhandisi na kuanza kumtumikia Mungu wa kweli kuanzia mwaka 2003, kazi ambayo amekuwa akiifanya hadi sasa ambapo kanisa limesimama na kuenea Tanzania nzima na duniani,” alisema Daudi.
Mchungaji huyo ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya kiongozi mkuu, alisema kanisa hilo limekuwa na maagizo ya kweli ambayo Mungu aliagiza yafanyike.
Kiongozi huyo akizungumzia namna ya kujiunga na kanisa hilo alisema kuwa, sharti la kwanza ni mtu kubadili jina lake la awali na kupewa lingine ambalo ni matakwa ya Mungu kisha kubatizwa upya.
Alisema kanisa hilo halikubaliani na mambo ya dunia kama vile kuwa na Siku ya Kifua Kikuu, Siku ya Ukoma, Siku ya Ukimwi na kadhalika kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ufalme wa Mungu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaoishi jirani na kanisa hilo walipohojiwa kuhusiana na nyumba hiyo ya ibada walisema wana wasiwasi na nguvu za kishirikina ndiyo zinaratibu mwenendo wao.
Muonekano wa kanisa hilo kwa nje.
Waumini wa makanisa mengine husema “Hawa wanaosema namba za mwezi mwisho tarehe 28 ni mambo ya Freemason. Sisi tunaona hivyo,” alisema muumini mmoja ambaye naye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Hivi karibuni gazeti hili liliibua kanisa lingine liitwalo Brotherhood of the Cross and Star la jijini Dar ambalo waumini wake husujudu na kuingia kanisani wakiwa pekupeku huku mabikira wakipewa kipaumbele cha kupelekwa nchini Nigeria, makao makuu ya kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment