Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha
wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake.
Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti
ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o
katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo
ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.
Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu
kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa
huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria
za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba
wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza
kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.
No comments:
Post a Comment