Friday, September 12, 2014

PATROBAS PASCHAL: MWENYEKITI MPYA BAVICHA TAIFA


PATROBAS Paschal amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, (Bavicha).

Mwenyekiti huyo alichaguliwa katika uchaguzi uliyofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kunakoendelea uchaguzi mkuu wa chama hicho Taifa.

Akitangaza matokeo hayo jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi wa vijana, Hashim Issa, alimtangaza Patrobas kuwa mshindi  kwa kura 173..Mwenyekiti mpya wa BAVICHA, Patrobas Paschal

Hata hivyo, uchaguzi huo ulifanyika katika awamu mbili ambako ya kwanza Upendo Peneza alipata kura 68 na Patrobas Paschal 61

Alifafanua kuwa kufanyika kwa uchaguzi wa awamu ya pili ni baada ya mshindi kutopata asilimia 50 ya kura alizopata.

Issa, alisema katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara ilikuwa ikiwaniwa na wagombea 11 ilichukuliwa na Patrick Ole Sosopi aliyepata kura 128 dhidi ya mpinzani wake Jesca Kisikwa aliyepata kura 110.

Alisema kwa upande wa Zanzibar Makamu Mwenyekiti iliyokuwa na wagombea watano, mshindi ni Zeudi Abdallah aliyepata kura 126 dhidi ya Shabani Omary Shabani kura 69.

No comments:

Post a Comment