Ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa eneo la Makao Makuu ya Polisi wakati Freeman Mbowe akiwasili kuhojiwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha), Halima Mdee akiwasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar leo.
Wananchi wakiwa Makao Makuu ya Polisi.
Mbowe
amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake
aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima
kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Katika
tukio hilo, baadhi ya waandishi wa habari wamekimbizwa na polisi
waliokuwa na mbwa wakitakiwa kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika
makao makuu hayo ya polisi.
Mmoja wa wanachama ambaye alibishana na askari na kujikuta akipata kibano kidogo na baadae kuachiwa
Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN
MBOWE leo amefanya shughuli za jiji la Dar es salaam kusimama kwa muda
baada ya kufika makao makuu ya polisi jijini akiwa na wanasheria wa
chama huku mamia ya wanachama wake wakiwa nyuma yake kutaka kujua
kinachoendelea hapo ikiwa ni kuitikia wito wa jeshi hilo waliomtaka
kufika kwa maelezo zaidi.
Baada ya mh MBOWE kufika makao makuu ya polisi aliingia ndani na
kuhojiwa zaidi ya masaa manne na kisha mwanasheria wa chama hicho mh
TUNDU LISSU kutoka na kauli kuwa mwenyekiti huyo ametuhumiwa kuwa makosa
ya uchochezi alioufanya juzi jumapili wakati akihutubia wanachama wake
ambapo alisema kuwa wataandamana na kufanya migomo nchi nzima kupinga
bunge la katiba linaloendelea.
Hata hivyo kwa taarifa ya TUNDU LISSU ni kuwa mh MBOWE ameachiwa kwa dhamana kwa ajili ya kusubiri kesi yake hiyo.
Hata hivyo mh MBOWE alionekana kufichwa sana kiasi cha kutoikuwa rahisi kuonekana na wafuasi wake
Nje ya ofisi za jeshi la polisi wananchi ambao ni wafuasi wa CHADEMA
walionekana kuwa na hamu ya kumwona mwenyekiti wao ambapo kwa mara
kadhaa walisikika wakiimba na kupiga kelele ambapo polisi walianza
kuwasukuma na kusogeza silaha zo karibu ila hali ikawa shwari.hadi
mtendao huu unaondoka katika eneo la tukio wafuasi hao walikuwa
wameondoka kwa maombi ya mwanasheria tundu lissu kuwa waondoke hapo ili
kuepusha vurugu zisizo na msingi
Viongozi wa chama hicho walikuwepo kuhakikisha kuwa hali inakua shwari
Mh TUNDU LISSU akizungumza na wananchi pamoja na wanahabari ambao
aliwataka kuondoka katika maeneo hayo ili kuepusha vurugu ambazo
zingeweza kuwaharibia zaidi katika kesi hiyo
No comments:
Post a Comment