Thursday, September 18, 2014

MASKINI NDOA HII JAMANI IMEFIKIA HAPA

Stori: Richard Bukos
PAMOJA na kutumia nguvu nyingi kukanusha kwenye mitandao kwamba ndoa yao haijavunjika, mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.

Tukio hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Bongo Fleva.

WALIVYOKAA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye meza na watu wengine watatu,  baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.

JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.

WALICHOTAKA WATU
Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda  kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.

No comments:

Post a Comment