MTOTO
Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alizua
kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu
na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo
kimaajabu.Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye
Happiness alianza kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye
uwanja wa ndege kisiwani humo wiki iliyopita.
Alisema
maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo
uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa
nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali
vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.
Kwa mujibu wa mama huyo,
aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake
alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu
yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo.
“Akiwa
nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia
maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa
ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna
muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na
kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na
wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma
kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule
msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa
jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa
mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.
“Baada ya kushuhudia vituko
hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii ambako nako
wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na kuwaambia kuwa
angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu ya paa na
kutaka kutoka.
“Yaani kwa muda mfupi waliokaa
naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema amewahenyesha vya kutosha
ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi nikaenda kumfuata,”
alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua bandarini Dar.
Paparazi
wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya
bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini
hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama
Happiness.
Akizungumzia
historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na
mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana
mawasilino mazuri.
Mama huyo alisema alimpeleka
mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani na kutorokea
anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba
wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika
hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu
mtoto wake.
No comments:
Post a Comment