Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa.
Kipimo Abdallah
ALIYEKUWA
Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(BAWACHA) Jimbo la Kawe, Batuli Kivuma ambaye amejiunga na chama cha
Alliance for Change and Transparent (ACT-Tanzania amesema kilichomuondoa
CHADEMA ni ukabila ulioota mizizi kwa muda mrefu.
Kivuma
ambaye awali alikuwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi CUF alisema
aliamini kuwa chama hicho kinasimamia demokrasia jambo ambalo
limeshindikana hasa ukiwa hotekei mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema
tangu ajiunge katika chama hicho amekuwa na juhudi za kukijenga chama
hasa Kata ya Msasani na jimbo zima la Kawe ila juhudi zake zimekuwa
zikikwamishwa kwa misingi ya ukabila.
Katibu
Mwenezi huyo wa zamani wa BAWACHA alisema katika kudhihirisha hilo
alishiriki kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya Udiwani viti maalum
mwaka 2010 ambapo alishinda ila aliondolewa kwa kigezo cha yeye ni Mdigo
na wakapewa nafasi hiyo Wachaga.
“Kusema
ukweli suala la kuhama vyama sio zuri ila inafikia mahali unashindwa
kuvumilia kwani nimekuwa nikionewa mara kwa mara katika chaguzi na
ukiangalia vizuri msingi wake ni ukabilia ambao unawabeba Wachaga” ,
alisema.
Kivuma
alisema alikuwa akikipenda sana chama hicho lakini ubaguzi uliopo
amefikia mwisho wa uvumilivu na kwamba anahitaji kuonyesha jitihada zake
kwingine.
Alisema
suala hilo la ukabila lilikidhiri katika uchaguzi mkuu ambao ulifanyika
hivi karibuni hasa katika upande wa BAWACHA ambapo juhudi zilifanywa
kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.
Mwenezi
huyo wa zamani wa BAWACHA alisema hata upatikanaji wa Mwenyekiti wa
BAWACHA wa sasa Halima Mdee ulitawaliwa na ukabila ikiwa ni agizo la
Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe.
“Unajua
hili neno demokrasia wanalielewa je bwana kwani kwa ufahamu wangu ni
kuhakikisha kuwa jamii inaacha pale inapofanya maamuzi yake ila huku ni
kinyume”, aliongezea Kivuma.
Kivuma alisema atahakikisha kuwa anakibomoa CHADEMA hasa katika Jimbo la Kawe ambapo amefanya kazi za kisiasa kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake aliyekuwa Mjumbe wa Mtaa Serikali ya Mtaa wa Matofalini
Ujiji Kigoma Yassin Mohamed alisema ni vema vyama vikatambua kuwa hakuna
uadui baina yao na kuhama chama ni haki ya mtu.
Alitolea
mfano hali ya kisiasa ilivyokuwa siku za nyuma kati ya chama na CHADEMA
na CUF hali ambayo kwa sasa haipo na vinafanya kazi pamoja.
Mohamed alisema ameamua kujiunga na ACT-Tanzania na kuondoka CHADEMA ili kupata uhuru wa kupigania demokrasia ya kweli.
No comments:
Post a Comment