Thursday, October 2, 2014

KIJANA AFUMWA GESTI NA MKE WA KIGOGO


Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.

Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa kuserebuka.
Akisaini  kulipishwa faini
“Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika wasishtuke, walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo wakazama ndani.”

Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya wanahabari zikiwamulika, alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama adhabu ya kutembea na mke wake.
 
Kutokana na hali ya uchumi ya kijana huyo kutokuwa nzuri, hakuweza kulipa kiasi hicho cha pesa badala yake aliomba kupewa muda wa kulipa pesa hizo.
 
Chini ya uangalizi wa mwenyekiti, Marck aliandika barua ya makubaliano jinsi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa kwa kigogo huyo na iwe kama fundisho kwake kuachana na tabia za kutembea na wake za watu.
 
Kwa upande mwingine, mwenyekiti Patroba alikiri kumfahamu Marck na kudai ni kijana wa mtaani kwake na kumuonya asirudie mchezo huo mchafu.
“Namfahamu huyu kijana nimeshangazwa na kitendo hiki anachokifanya kwani ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii hivyo kama kiongozi wa mtaa huu nitaendelea kutoa ushirikiano ili kuukomesha tabia kama hizi za kuvunja miji ya watu,’’ alisema Patroba.

No comments:

Post a Comment